Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKARIMU wa KUMPIGA mgeni ili MWENYEJI apone.JIFUNZE kitu fulani kutoka South AFRICA ya LEO.

>> Monday, May 19, 2008

USIJIDANGANYE!
Si kweli ukarimu wa mwenyeji wako ndio ushahidi kuwa anakukupenda au anahusudu umemtembelea chobisi.

Nadhani inawezekana umewahi kusikia kamsemo; Mgeni njoo , MWENYEJI apone!

Mgeni akija, kuna uwezekano yule jogoo wa krismas akachinjwa mapema, na pesa za kununulia nguruka wa kesho, zikanunua soda.

Lakini mgeni akiendelea kuwepo, kuna watu watapata muda wakubadili mkao , kutoka mkao wa jamaa mgeni hatuwezi kumpa jembe tukaenda naye leo kulima, mpaka mkao wa ; HIVI WEWE UTAONDOKA LINI?

Kwa walioko nchi za watu wenye rangi tofauti ni rahisi mpaka kusingizia kuwa ni ubaguzi tu wa rangi ufanyao mtu kutokukutaka kwake au hata katika choo cha jirani.

Lakini, kuna watu hawampendi tu mgeni kutokana na sababu moja kubwa kuwa,YEYE ni MGENI.

Binadamu tunaudhaifu wa kutoelewa vigeni.

Lakini...
......Kitu kigeni tusichokielewa, tunaweza tukajikuta tu.... ...

  • Tumekiabudu kama MUNGU
  • Tumekiogopa kama Shetani
  • Tuna wasiwasi nacho kama kuonja nyama ya MBWa
  • AU KAMA KAWAIDA yetu TUTAKISINGIZIA hasa kwamba ndio SABABU ya YOTE mabaya yanayotutokea.

Nakubali, umasikini, ujinga, na mengine mengi yanaweza kusababisha mgeni awe nishai!
DUH!

JIHADHARI tu kama uko SOUTH AFRICA sasa hivi na si Msauzi, unaweza kupigwa kibano.
Jihadhari kama hauko Nchini kwako, au hata mtaani kwako, unaweza kupigwa kibano.

Nimebanwa kidogo!
Labda nitaendelea na topiki hii badaye kama bado iko mawazoni!

Angalia HAPA
au soma HAPA kama unataka kujua fununu ya yawatokeayo walio SOUTH AFRICA


KAMA unanafasi....
Hebu pitia kidogo UMASAINI kama kulivyorekodiwa wakati jamiii inawakarimu Familia ya GARSON(Tahadhari:Kama hupendi kuona damu au mnyama akichinjwa usiangalie!)


Au tukatike viuno kama SOUTH AFRICA tu, ambako hatutakiwi kuwepo..katika kibao kiletwacho na TSHE-THSA BOYS

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Egidio Ndabagoye 11:44 am  

Dah ishu hii inasikitisha sana afu sasa hii ishu iko njiani kutokea bongo maana sasa hivi hapa idadi ya wagweni wanaochukua kazi hata zile "bluu kola" wanachukua wageni.

KUna siku kadhaa jamaa f'lani alitukana matusi ya nguoni baada ya kumcheki jamaa wa kigeni akikatiza na gari la kifahari anasema jamaa wanachukua nafasi zao....naona ni kama hii ya kwa Madiba.

Simon Kitururu 1:17 pm  

@Egdio:Hii kitu rahisi sana kutokea Tanzania kwa mtazamo wangu!Nasikitika kuwa sina uhakika kama viongozi wanaiona !:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP