Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kilema cha MAANDISHI , PICHA, TV,sinema au KUSHUHUDIA , hata katika kusaka habari za MPENZI KIBOGOYO.

>> Friday, May 16, 2008

Nasikitika kuwa maandishi , picha na hata ushuhuda wa macho inaweza kuwa si msaada kwa binadamu katika kukabiliana na ubinadamu au dunia hii, ingawa unawezakusema unajifunza kitu kwa kuangalia picha za nanihii au kusoma maandishi.

Ubinadamu nishai!
Karibu kila agusacho au kutumia kama binadamu, kina udhaifu.

Ndio maana hata kama huamini Mungu, ni vigumu kuwa na uhakika kuwa hakuna Mungu au angalau LIKIUMBE ambalo linasababisha binadamu huyu mwenye mapungufu, pamoja na mende, wawepo hapa duniani.

Usitishike sana!
Inawezekana nilivyovitaja vinakusaidia.
Na ni ukweli naheshimu maandishi, picha , picha zitembeazo na pia , ushuhuda wa macho.

Naandika hapa leo hii kwa sababu nimeshangaa kujikuta nabishana na watu kuhusu umuhimu wa vitu hivi, kitu ambacho sikudhani kinaubishi.

Au nisemee...

Naamini kabisa kujisomea hasa vitabu, ni bomba la ujanja katika kutekenya akili.
Ila sipingi umuhimu wa picha au picha malaya(moving pictures, TV,Videos,etc.) kwa jinsi zisaidiavyo uelewekaji wa jambo kwa kutumia kona nyingine. Pia sisahau msaada wa maswala ya shuhuda za kuona papo hapo.

Nachojaribu kusema ni.......

1. Maandishi huhifadhi taaluma vizuri sana, ingawa stori za paja la kuku, kama hujui kuku yukoje, akilini lawezakufanana na paja la kicheche uliyemzoea baada ya kumalizia kusoma stori za kuku.

Utamu wa kusoma maandishi ni pamoja na jinsi ukupavyo uhuru wa utalii wa ubongo
( imagination).
Katika maandishi na kama hujawahi kuonyeshwa michoro ya picha za shetani mwenye mapembe, basi shetani anaweza kuonekana anasura kama yule kidume au kijike umuogopaye, ambaye anaweza hata akawa ni mwalimu au mme wako.

Swali:

  • Kama usingeonyeshwa michoro ya kubunia ya shetani au YEsu , unafikiri mawazoni kwako Yesu na Mkwawa wangekuwa wanasura au wamevaa ulimbwende aina gani?
  • Tukiachana na maandishi katika barua kwa Baba:Wakati unaongea na simu na LIMTU lako , ushawahi kufikiria unayeongea naye ananukaje mdomo?


2. Maswala ya video na picha ni kiboko pia!
Usipoangalia unaweza kusahau kuwa si lazima yarahisishe kwako kuelewa kuwa hiki ni KIJIJI cha MATOMBO au hivi ndivyo jinsi BATA wafanyavyo MAPENZI.

UKiona picha au video ya kijiji ,ni mpaka uambiwe kuwa hiki ni kijiji cha MATOMBO ili uelewe kuwa hapa si kijiji cha KIABAKARI.
Ukiona picha au video za Bata wanafanya mapenzi, kama hujui kinachoendelea, unaweza kufikiria kuwa BATA wanapigana.(Kwani hujawahi kusikia waliofumaniwa na mtoto wao wakati wanafanya mchezo wa baba na mama halafu mtoto akalia kuwa BABA ANAMPIGA MAMA?)

Swali:
  • Ushastukia kuna watu duniani , picha ipigwayo Tanzania au GINI ya Ikweta(Equatorial Guinea) kwao ni sawa tu, hasa kutokana na kufikiria Afrika ni nchi moja?

3. Mwisho ....
Nakiri tuko tunaohusudu taaluma na ujinga tuufyonzao kwa kushuhudia jambo kwa macho yetu wenyewe.Lakini swala la kushuhudia jambo, ni rahisi kujidanganya kuwa utaelewa au hata kuweza kuwa mtoa ushuhuda mzuri zaidi kwasababu ulikuwepo wakati kitendo kinafanyika. Cha ajabu ni kwamba, kama hujui mchezo wa Kriketi , hata uutolee macho kama bundi, huwezi kuelewa daktari anafanya ninikatika operesheni yako ya jando, kama huna taaluma husika.

DUH!

Kuelewa ni nini kinaendelea kunahitaji tetesi za kujua unachoangalia ni nini, la sivyo ,UTABUNIA.

Katika vita zetu za kutumia SILAHA za mkuki na mapanga , hili likitu ambalo jamaa anakunyoshea bila kulirusha au kwa jina jingine BUNDUKI , mtu unaweza kulidharau kuwa si SILAHA na wala haliui kirahisi tu kama au kuliko mshale wako wenye sumu ya nyongo ya kenge, kama hujawahi kusikia duniani kuna hata kitu bomba kama GOBOLE.

Sasa cha kujiuliza tu ni kwamba.....
.....Haya yote tuyatafutayo au kuhifadhi katika maandishi , picha au ubongoni baada ya kushuhudia,si ni maswala tu yasaidiayo tu kujazia muda wa binadamu hapa duniani akiwa safarini kutoka kuzaliwa kuelekea kufa?
.......Haya mavitu tuhangaikayo kuyatafuta hata kwenye dini , pombe au moshi wa majani ya mpapai, si ni majivitu ya kujaribu kujazia tu haya maisha ladha tamutamu kunoga ili katika ujazo, yazidi kupunguza kusikia kwetu uchungu au yajaribu kurahisisha kutupatia kanjia kakuendeleza tamutamu kunoga baada ya wewe ,mimi na yule kukata roho , kufa au kuanza?


EE BWANA EEH!Naaacha basi kitopiki!
Kumbuka Mimi Nawaza tu hapa!

Hebu twende KANADA tukamsikilize tena RUSSEL PETERS akishauri WAZUNGU waanze KUPIGA WATOTO WAO.....

Au Ngojea twende NIGERIA tuangalie mambo ya KIDUNIA kama VILE ya akina DADA wakipigana....

Tulia tu na ERIC SERMON akija na kibao REACT

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP