Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ASIYETUKANA ukimsachi unaweza kustukia naye anamatusi tu NDANI YAKE!

>> Wednesday, July 28, 2010

Uwezo wa  WATU kusema chochote kile UPO,.....
..... ingawa sio kila MTU mwenye kibezi cha kusema chochote kile ANACHO kifikiria.


Na ingawa kuna WATU lukuki  wasingiziao KUJIHESHIMU, walivyooshwa ubongo na dini au tu tabia nzuri ndio kiwasababishao washindwe kupata FARAJA ya kukutukana  au KUKUSENGENYA hadharani wapo,...
.... ukichunguza unaweza kustukia WAPO PIA WASIO SEMA  kwa kuwa hawajui tu jinsi kuwakilisha MLOLOMO  kimswano HADHARANI  ingawa wanavyo kufananisha na watu watengenezacho MSALANI bado ndivyo wanavyo kufikiria.:-(




Swali:
  • Si unajua labda LEO asilimia kubwa ya ULIYOYAFIKIRIA hujayasema?
  • Umewahi kujichunguza JINSI wewe mwenyewe unavyojinyima FARAJA ziletwazo na kusema chochote kile?


Ndio,....
.....hata PADRE au SHEKHE anayekutolea macho ukimsachi anacho kifikiria unaweza kustukia ANACHOKUSEMESHA sio anachokifikiria kwa kuwa labda anacho kifikiria kikitendwa kuna atakaye pata ujauzito.:-(


Ndio,...
..... unaweza KUFUKUZWA kazi kisa umesema chochote kile na hata kama KIBUSARA kina bonge la tani kiuzito.:-(

KWA bahati mbaya naachia hapa WAZO!:-(

Hebu The Kilimanjaro Band walete -Kachiri



Au tu JACOB F. DESVARIEUX anlete ndude -Goree



Au tu Jacob Desvarieux , Jocelyne Labylle & Cheela warudie mdinyo -Laisse parler les gens


Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP