Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KAWAIDA- kwa kuwa ni kawaida kupitisha siku bila KUFANYA matusi!:-(

>> Saturday, July 31, 2010

[Tahadhari: Katika tararila HII neno matusi halina uhusiano na vitendo vitendewavyo sehemu za siri.:-(]




NDIO,...
... kwa kuwa ni kawaida kupitisha siku bila kufanya MATUSI,....
... bado hilo halibadili kuwa ni kawaida PIA kama siku ikipitishwa kwa kufanya MATUSI.:-(



Swali:
  • Unabisha?

KAWAIDA ni KIDUDE bonge la kigeugeu kwa kuwa labda KAWAIDA,....
..... huhitaji tu UNAVYOTAFSIRI nini ni KAWAIDA na uzoefu wako wa KURUDIARUDIA KITU ,....
.... kitu kifanyacho kumuwezesha BINADAMU MWINGINE kwenda CHOONI kabla hajabanwa kwa kuwa ni kawaida kwake akiamka tu cha kwanza ambacho kwake ni kawaida ni kwenda kunya.:-(


Swali:
  • SI mpaka kuna atakaye kula NANIHII wakati hana njaa ya NANIHII kisa kazoea tu na kwake akiona tu KINONO anafikiri ni lazima aonje?

  • Umewahi kuchunguza UWEZEKANO kuwa labda KAWAIDA kwako inaweza ikamchubua uchi wa FIKIRA mwenzio?


Na kama kwako ni KAWAIDA kupitisha siku bila kula kwa kuwa UMEZOEA,....
... unaweza usimuelewe aliye FUNGA hata RAMADHANI kwa kutafsiri kutokula ni KUFUNGA.:-(

NIMEACHA!
NA ni wazo tu hili MHESHIMIWA wala usikonde!:-(

Hebu RICHIE SPICE  akiwa na CLINARK walete kitu - Living In A Concrete Jungle



Richie Spice na J BOOG wanyokolishe pambio-Got to be STRONG



Au tu RICHIE SPICE amalizie mkuno kwa ndude- MORE LIFE




Au tu J Boog alainishe ujumbe kwa -LETS do it again

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 5:11 pm  

Kuna bahati nzuri na nyingine kwakuwa watu hawafanikishi azma inaiywa BAHATI MBAYA. Na kwakuwa huzuni unaweza kuishtukia kuwa ni bonge la mnururisho kimyani na kitulizo cha tabia.... kumbe ni ngoma ya watu wenye imani mbili ya wewe na yule eti mnajuana ninyi na nyinyi.

sijaelewa...... wazo limeteguka kichwani ghafla mkuu

chib 10:05 pm  

mada hii si ya kuingia kichwa kichwa, mambo ya Kamongo na Pegele

Maisara Wastara 2:20 pm  

Chib, usijitie hamnazo wakati umelielewa wazo hili kimtindo...LOL

Kwa kuwa katika kutumia tafsida neno matusi likapewa maana ya vitendo vitendwavyo sehemu za siri, sina budi kusema wazo lako hili lililopinda limebeba maana ile ile ulioikanusha tangu mwanzo....

kaka fumbo mfumbie mjinga....

emu-three 12:35 pm  

Hii ni kawaida kwa asiyejua kuitwa mjinga na akiuliza ni kawaida kukebehiwa na hata yule asiyejua nini kinachoulizwa.
Na ni kawaida kuuita mkono mkono, lakini sio kawaida kuziita sehemu za siri kwa maneno yake ingawaje kila siku unavishika na kuviona, kwako ni kawaida, sasa iweje kuwa kawaida kwako na kwingine kusiwe hivyo.
Ndio ni kawaida, kama ni kawaida kwako kutenda hilo na usiliite tusi kwanini akitenda mwenzako unaliita tusi.
Kuuliza si ujinga, ila asiyejua anaitwa mjinga, kwahiyo wote sisi ni wajinga kwasababu hatujui kila kitu, labda Maisara anajua vyote

Yasinta Ngonyani 8:10 pm  

Mmmmhhh!.-( leo ueleo umepiga chenga...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP