Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tatizo liwezalo KUJITOKEZA kwa kuwa NYOKA huwa HAWAKOJOI,......

>> Friday, July 30, 2010

.....labda ni kuwafanya WASISTUKIE viumbe  wengine wanakojoa na kwao KUKOJOA ni muhimu.:-(





Na labda ni kweli  kwakuwa NYOKA hawakojoi,...
.....labda kwao sio muhimu kujua kama ni kweli kwa BINADAMU kukojoa ni muhimu.


Swali:
  • Kwani huwa unakumbuka YASIYOKUHUSU labda NI MUHIMU kweli kwa WENGINE?

  • SI unajua ya WENGINE  yanaweza kuwa ni MUHIMU SANA tu KWAKO ingawa hujastukia UHUSIANO wa YA WENGINE na WEWE?

  • SI unajua kama wewe ni mpenda MAUA ingawa HUWAHUSUDU NYUKI labda nyuki ndio wasababishao furaha zako za MAUA ya pendezayo hasa ukikumbuka halihalisi kuwa LIBWANA lako LINA SURA mbaya na halipendezeshi NYUMBA?



Na kwa kuwa BINADAMU anaweza kuhisi ya NYOKA hayamuhusu,....
.....kitendo hicho kinaweza kusababisha BINADAMU aishi bila kustukia NYOKA hakojoi.:-(

Na wakati unafikiri  BINADAMU WENYE MAJI YA KUNYWA  ya watu  yanawahusu,....
..... kumbuka BINADAMU huyohuyo anaweza kusahau kuwa MTU mwenzie kwa kuwa hana MAJI ya kunywa  leo anaweza kuwa anakosa  FARAJA KAMA ZAKE za  kutoa mkojo kwa kuwa  KUTOKANA NA UHABA wa maji , hakojoi.:-(

Swali:
  • Wakati BONGO FLEVA inakuhusu  unauhakika BONGO FLEVA haina uhusiano na MDUNDIKO?

  • SI unajua UFIKIRIAYO hayakuhusu LABDA yanauhusiano  nawe na kukuhusu kuliko UFIKIRIAVYO ?
  • SI unajua labda hata kilimo cha PAMBAufikiriacho kuwa hakikuhusu kwa kuwa HULIMI PAMBA labda kinauhusiano wa karibu sana na CHUPI YAKO uipendayo ambayo kwa inavyo kuhusu  unaivaa siku  maalumu tu ambayo unahisi utachunguliwa kwa kupenda mwenyewe?


  • SI una JUA labda URAIS wa Rais KIKWETE una uhusiano na wasukuma MKOKOTENI wasababishao URAIS wa RAIS KIKWETE uwezekana kwa kuwa tu  azungumziavyo vya wasukuma MIKOKOTENI vinakuhusu?

NI WAZO TU HILI na ni ruksa kutolielewa!:-(

MIE naanza kivyangu na nakutakia IJUMAA  na wikiendi KIBONGE!


Hebu twende Ivory Coast mtoto mdogo  BB DJ waanzishe siku kwa -Enfant POLI



 Hebu tupitie Guinea ili  Mory Kante arudie mkuno-Touma




Au tu twende Senegal ili  Daara J Family walete ndude- Bayi Yoon

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 6:06 pm  

mmmhhh! Ijumaa njema nawe pia!

nyahbingi worrior. 9:56 am  

Mkuu nimepita kukusalimu na kupata elimu mkuu.

Amani.

Simon Kitururu 3:52 pm  

Asante Da Yasinta!
Asante RASTA!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP