Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Chaguo la LEO: Katika kutibiwa NANIHII, ungependa NESI kipofu au DAKITARI kipofu ?

>> Wednesday, May 26, 2010

[Tahadhari:Kuna uwezekano wazo limepindia kushoto zaidi ya kulia katika taralila hii!]


Katika kuchagua,...
... unaweza kuwa unatishika NA MAJINA yaambatanao na wenye taaluma kuliko hata TAALUMA yenyewe waliyonayo kwa kuwa ukifikiria UNAWEZAKUSTUKIA ,...

.... kuna uwezekano NESI na DAKTARI vipofu wenye utaalamu na GOVI wanaweza wakawa wazuri katika tibabu lako LA KUKATWA JANDO kuliko NESI na DAKTARI waonao lakini utaalamu wa kucheza na GOVI kimatibabu hawana.:-(


Swali :
  • Si unaweza kutishika tu kwa kusikia NESI na DAKTARI watakaokutibu ni vipofu wakati gonjwa lako  linahitaji ajuliaye kupapasa na wala sio aonaye?
  • Unauhakika ni asilimia ngapi ya magonjwa uliyowahitibiwa  NESI au DAKTARI alikuwa anatumia macho kuyaona ili upewe KLOROKWINI?

Ndio,....
.... labda MAHUBIRI mazuri ambayo yatakufanya uende mbinguni  MWENYE NAYO ni yule umkwepaye kumsikiliza ukiwa na nyege za kutishwa kuhusu JEHANAMU  au SHETANI kisa KIUTAMBULISHO  anaitwa tu  KIBAKA , kiruka njia, MPAGANI  au tu  KIDUME anajulikana kwa kupenda kukuna sehemu za siri wakati anaongea na WATU hadharani kitu ufikiriacho kuwa si sahihi kufanyika kwa akuhubiriaye kuhusu MUNGU hadharani.:-(

Ndio,...
... inawezekana moja ya kimsaidiacho MGONJWA kupona ni imani yake tu  kuwa ANATIBIWA  vizuri na MTU au  MADAWA yanayoaminika  kitu ambacho kinasababisha  pia KWA IMANI  hata manabii wa uongo wanao watu LUKUKI wakirio kuwa waliponywa nao HADHARANI .:-(


Swali:
  • Si unajua nesi akuchomaye sindano aliyevaa glovu anaweza akahatarisha imani yako ya kupona ugonjwa kwa VIDONGE alivyokupa ukigundua wakati anakupa vidonge alitoka haja kubwa na hakunawa mikono vizuri baada ya MTAWAZO  ingawa mikono yake haijagusa vidonge kwa kuwa kavaa gloves?
  • Si umeshawahi kusikia eti hata YESU alikuwa anasema ``IMANI YAKO IMEKUPONYA´´? 
  • Sitanii, wewe kwako ni afadhali Nesi au Daktari wako ndio awe KIPOFU?
  • Kama wewe sio kipofu umeshawahi kufikiria KIPOFU anakuaminije wewe bila kukuona au tu anastukiaje unabonge la makalio?

IMANI nishai,...
.... inaweza kusababisha uamini mke wako ulimkuta bikira wakati unamjua mtoto wake ULIYEMKUTA NAYE  alelewaye na wazazi wake.:-(

Imani NISHAI,....
.....kwa kuwa inawezajengwa bila USHAHIDI kama vile tu UDEKUVYO KWENYE MASWALA YA  DINI ila kwa imani tu UKAAMINI  UNESI au UDAKTARI haumfai KIPOFU   kwa kuwa kwa imani unaamini ILI DAKTARI akutibu malaria inahitajika AKUONE  ili ustukie kama anakuelewa hasa kwa jinsi wakati anakudadisi ili kujua ni GONO au MALARIA ndicho kinachokusumbua UMDEKU anavyokuuzia kwa huruma na upendo LISURA lake.:-(

NI wazo tu hili  USINUNE Mheshimiwa!
Cheka basi kidogo !AU?

Basi bwana NIMEACHA!:-(




Au tu tupate mnyumbulisho kutoka kwa GILBERTO SANTA ROSA anyuke kwa - VUELA LA PALOMA



Au tu Machel Montano na Xtatik wanyuke tena - Big Truck



FIKIRIA hii spichi ingekuwa ni ya RAIS mmoja wa TANZANIA na asemacho hapa Martin Luther King Jr kiwe kinamaa kuwa huyo Rais wetu MTUKUFU kashaona TANZANIA ielekeapo KUNAUNAFUU kwa MTANZANIA MNYONGE na kunanukia bonge la pilau[hasa kama wewe ni mpenda pilau] hebu sikiliza kwa mkao wakumtafakari HUYO Rais wa TANZANIA kuwa anaongea kuwapamoyo WATANZANIA

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 7:27 pm  

Mkuu taralila ya leo kubwa kuliko. Imenikumbusha enzi zangu kijana mdomo nilipokuwa nikipelekwa hospitali kuchomwa sindano, nilikuwa nachagua nesi wa kufanya hivyo. Duh! Hatari mbona!

MARKUS MPANGALA 7:00 am  

mtani naungana na wewe HII NI KUBWA KULIKO YAANI KIGAWO KIKUBWA CHA SHIRIKA

Christian Bwaya 12:26 pm  

Hoja imesimama wima

Maisara Wastara 4:24 pm  

Wazo hili halijapinda bali limepindishwa....!!!

Nimejifunza humu jando na unjago...kama kumtoa mwali wa kizaramo

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 3:19 pm  

imani yako wazo halijapinda

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP