Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LEO ukiwa na hamu!

>> Friday, May 21, 2010

....na mwenye HAMU,...
... inasemekana ni kawaida anataka.:-(


LEO na HAMU...
... na mwenye HAMU,...
....kama tu wasio hamu ukiwachunguza nyuma ya kitunza kinyeo labda wana TAKA.:-(



Leo na HAMU...
...taka na TAKATAKA na kwa kuwa LEO laweza kuwa jina la MTU labda ni taka ,.....
.....katika kitakiwacho KWA WATAKAO LABDA ni TAKATAKA.:-(

Leo katka tamu ya HAMU,...
... labda vyote VITAKIWAVYO kwa ASIYETAKA ni takataka.:-(


Swali:
  •  Ushawahi kuwa na hamu NA KITU  halafu wakati hupendi mabiringanya ukaona biringanya na kufikiria labda BIRINGANYA tamu?
  • Umeelewa?
  • Si unajua si lazima uelewe?
Wazo la leo NI HAMU  na hamu inawezekana ikawa ni ya BAGIA katika siku ya tamanio la mishikaki kwa mwenye chachandu  ambaye ukimpa MSHIKAKI  kwa kujivunga anaweza kusema anataka ingawa atakacho sio CHACHANDU wala MSHIKAKI.:-(




NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA KIFALSAFA na usijali kama huelewi hii KINDEGATENI!:-(
NI wazo tu hili kwako AJUZA!:-(
Ndio NI WAZO TU HILI  MKUU WA WAJANJA  na sitaniii hata kwako  Mdada mwenye HAMU UIFICHAYO KIJANJA  na PAPAA mwenye HAMU ambayo ina kufanya uchovye cha hausigeli KIJANJA !:-(
NIMEACHA!:-(

Hebu nibadili kwa kumpata The great MIKE TYSON atukumbushe ni nini waheshimiwa wasio wajanja wakumbukavyo katika ya -Mike Tyson's




Au tu Richie Spice anyutrolaizi lawalawa na MKITO - Uptown Girl




Au tu Richie Spice akiwa ni miongoni wa watu wavutao wakisifiao na hakuna siku nimekutananaye kimemzingua avutachokimemzingua aendelee halafu jiulize ni wangapi UWAJUAO  watumiao wako fiti hivi kuanzia kutunga vyombo mpaka kuimba  walivyovitunga kama afanyavyo huyu katika ndude- MVUKE



Au tu nimuachie huyu hyu Richie Spice asifie  katika kitu -Brown Girl

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 7:25 am  

Ama fikiria unapokuwa na HAMU halafu jinsi uvutiwavyo na yule mkata kiu ya hamu ambaye NYODO zake zinaifanya hamu yako kuwekwa PENDING hadi apatikanapo binti MARIDADI aijuaye MIKITO bila nyodo ila akiwa amesheheni MANJONJO kiasi cha kukufanya kumwagia CHAPAA zako zote huku ukijisahau kuwa FAZA HAUSI kagoma kukuongezea kamshahara.

Ni wazo tu CHEKIBOBI uliye gradueti kutoka kindegateni juzi kati tu.

Yasinta Ngonyani 2:08 pm  

Leo ukiwa na hamu:-)

MARKUS MPANGALA 9:38 pm  

RUKSA KULIBISHIA); si unajua hata ukichomekea unaweza kuwa na HAMU ya kujamba kama mvaa suti halafu anatembea kindekulendekule.
WAKATI unafikiria una HAMU, unasahau kuwa kuna HAMU upande wa pili itolewayo baada ya KINDAGATENI kushtukia kuna HAMU itekewayo HAMU ili ipate HAMU. MSELA naye ana HAMU hata akiona michirizi ya vinyweleo na mirindimo ya shamukwale ya bolingo. hongera kwa kuwa na HAMU ya kugradueti HAMU

o'Wambura Ng'wanambiti! 2:20 pm  

Duh! Mbona hatujaalikwa hiyo graduation jamani?...lol

Mzee wa Changamoto 3:13 pm  

Duh!!!
Wazo kibonge

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP