Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUNA uwezekano MJANJA sio YULE AJAMBAYE KISIRI!

>> Monday, May 17, 2010

KWA binadamu,...
.....kitendo kidogo ambacho kila mtu anajua kila mtu anakifanya inaweza kuwa ni ujanja kukifanya siri.:-(



KWA binadamu,...
... haki ya nani hata KUJAMBA kama nia na malengo yako huna uhakika na wakuzungukao wana kuathiri vipi inawezekana kama umejaliwa USHUZI WAKATI HUO  na ukautoa kwa neema na furaha labda weye ni MJANJA na unaweza kutajirika kwa kuwauzia waliokusikia ukijamba kwa furaha mbele za watu hiyo SIRI.:-(



Swali:
  • Unabisha?

Ndio,...
... kuna ambao walistukia tokea UTOTONI kuwa kujamba HADHARANI SIO USTAARABU na wakaanza hapohapo mazoezi ya KUJAMBA kwa siri.

Swali
  • SI unajua sikuzungumzii wewe?

.....na HAKI YA NANI TENA,...
... kama hao watu kama WANANUKIA PAFYUMU NZURI unaweza usistukie wakati umekutananao WAKINUKIA VIZURI kuwa wakati huo labda wametoka KUJAMBA au kwa lugha ya kitaaalamu ,...

....wametokea kuachia USHUZI.


Swali:

  • Unauhakika ni mara ngapi katika uwaaminio kama vile , PADRE, mchungaji , SHEKHE, RAIS ... wakati wanakupa hoja zinukiazo vizuri bila wewe kustukia walikua wanaachia ushuzi  wakati huo WAKIKUPA HOJA MWANANA au walitoka kuachia ushuzi wenye undugu na mayai yaliyooza kitu ambacho huwahusianishinacho wakati msikilivu  na wakati huo una busara?

  • Si unajua kuna uwezekano hapa siongelei KUJAMBA aka USHUZI ?
  • Unauhakika wewe MJANJA?

NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA.:-(


Hebu tusikilize ya Valentin Abe



Au ngojea watu wajaribu kutuchekesha..

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP