Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MIPANGO ya NCHI IITWAYO TANZANIA kama aiendeshayo angekuwa ni yule aandaaye KICHENI PATI!:-(

>> Monday, May 17, 2010

Mipango ya HARUSI,...
......ambao wanaandaa HARUSI hufanikisha HARUSI TANZANIA.:-(


Aandaaye bajeti ya KICHENI PATI Tanzania kabla ya HARUSI,....

.....  bonge la profesa wa bajeti za KITANZANIA kwa kuwa KICHENI PATI  zina tako kubwa kweli kwa mpenda matako makubwa  KIUFANIKISHAJI   katika mtikiso  TANZANIA.

Swali:
  • AU?
  • Si unajua Harusi hufanikiwa  BONGO ila kujenga zahanati ni shughuli TANZANIA kama tu kutafuta hela za kuchangia ada  ya shule?


Ndio,..
... kuna walipa kodi BONGO.:-(

Ndio ,...
...tuna RAIS , wabunge, diwani  na mpaka .... BONGO.:-(

Swali:

  • Hujawahi kufikiria  kama TANZANIA ingeendeshwa kwa umakini wa waaandaa HARUSI  wa TANZANIA hata kama ITAENDESHWA kama kile  kikao    cha kuhusu chupi ya bibi harusi haijalipiwa  labda TANZANIA ingeshakuwa imefanikiwa  kwa kuwa kufanikiwa kwa tendo linuiwalo KWENYE HARUSI huwa  ni muhimu kuliko  chupi YA BIBI HARUSI ni bei gani katika kulifanikisha?


  • Si unajua kutonielewa ni RUKSA?
NIMEACHA!

Hebu SADIKI arudie - Do You Hear What I Hear

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 7:13 am  

Hapo umemaliza yote mkuu. Maana harusi na kitchen party zinafanikiwa sana humu ubongoni...kwa hiyo wale waandaa bajeti wangepewa kusimamia bajeti ya hii inji basi mambo yangekuwa tirarira sana..
Nimeruhusiwa kuendeleza wazo hili kivyangu..

Upepo Mwanana 11:09 am  

Mtakatifu vipi? Yaani post zilikuwa zimejam au...., maana zimefumuka huko zilipokuwa na kujaa hapa kibarazani utazani hazina akili nzuri.. he heee
Nimepata uhondo wa habari na kucheka

Yasinta Ngonyani 9:20 pm  

KWA KWELI KAMA HIZO KICHEN PARTY ...NDO INGEKUWA KUJENGA ZAHANATI AU VIJISHUGHULI KWA WASICHA TUNGEFIKA MBALI SANA...!!Ahh! karibu tena mt. maana ulipotea kidogo...

MARKUS MPANGALA 10:39 pm  

Moyo unasema safiiii,
weka na hadharani basiiii,

Nilimiss sana haya mambo. Hoja hii mkuu ninaomba kuitengeneza kimakala flani kuiba aidia hii ya bongo la mdundiko wa ALMASI

malkiory 11:20 pm  

Kitururu unanikumbusha mbali sana,wakati nakujua kusoma huku ulaya, nilitakiwa kuonesha Euro 6 kwenye account yangu kama bank statement. Ni hapo nilipogundua urafiki na undugu wa kweli. Chakushangaza ni kwamba watu hao hao hawachoki kutoa malaki kadhaa kwenye michango ya arusi, ngojea sasa uombe kuchangia hata hela ambayo unatarajia kuirejesha baada ya siku moja, wote watakukimbia. Hapa inabidi tubadlike na tuigi mfano wa wenzetu wakenya, wao wanatoa harambee ya elimu na si arusi tu.

Simon Kitururu 1:24 am  

@Fadhy:SI utani Mkuu!

@Upepo Mwanana: :-)
@Yasinta: Asante Dada kwa kunikaribisha.

@Markus: Ruksa kuiendeleza hoja hii Mkuu!

@Mkuu Malkiory: Yani inasikitisha sana ukichunguza nini tunakipa kipaumbele Bongo.:-(

o'Wambura Ng'wanambiti! 11:00 am  

angalia hata nauli usijeimaliza kwa kuchangia CHICKEN pati na harusi za bongo...lol

Unadhani mwaka huu tutachagua viongozi wa kuongoza kamati ya arusi au wagidaji baa kama mie kwenye ulanzi?...lol

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP