Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Sehemu ZA SIRI!

>> Sunday, May 23, 2010

Sehemu za siri maana yake sio KIJAMBIO,...
...na kama ni siri kuwa una kula uyoga  mbele ya wanywao mbege  kisiri labda hiyo si siri.:-(

Na kuna wenye sehemu za siri ambazo zinanuka kwa kuwa wanazichukulia ni sehemu za siri na sio KIJAMBIO,...

......kitu ambacho kinafanya KUNA waaminio leo hawatasababisha mtu akazinusa  SEHEMU AMBAZO LABDA NI  siri.:-(


Swali:

  • Unauhakika  unakumbuka sehemu za siri labda hazikuumbwa ili zinuswe?
  • Unafikiri una sehemu za siri wakati  Binadamu  hana siri?

Ndio ,...
...kuna uwezekano hata jasho la tako sio siri ya akimbiaye hasa kama anaonekana  kwenye mbio ana KIKWAPA..:-(


NAACHA HII TOPIKI!:-(

Hebu DDC Mlimani  Park wanyuke-SHEMEJI ISSA





Au ngojea Di Gaza na Vybz Kartel waongee kitu katika BICHI PATI



Au tu Vybz kartel aje na Popcaan & Vannessa BLING katika MNYUKO- Clarkes

11 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 9:49 am  

Sehemu za siri....kuna waaminiao lazima chapaa ilipwe kwanza kabla mtu hajapewa ruksa ya kuiparanganyua sehemu ya siri.

Yasinta Ngonyani 11:22 am  

Fadhy:-(
Mie sikujua kama kuna sehemu za siri:-(

Simon Kitururu 11:40 am  

"Papaa Fadhy: Nimelipenda neno ``KUIPARANGANYUA``.

Ila kitu kikiparanganyuka kwa kawaida si kitaharibu UTAMU katika MPARANGANYUKO?

@Dada Yasinta: katika kukufundisha , sehemu za siri kwa wachezao sindimba na sidilia ni TITI pia. Halafu eti kikojoleo pia ni sehemu za firi kwa wajifichao wakikojoa vichakani.:-(

Mzee wa Changamoto 3:11 pm  

Tatizo la tafsiri ya SIRI ni kuwa inatambulika kwa aitambuaye pekee. Ina maana ukijua SIRI hutakiwi kumwambia mwenzako na hii haimaanishi kuwa yeye hajui, ila labda kaamua kutokwambia ili iwe SIRI.
SWALI:
Kwani ni sehemu ngapi za mwili wako ambazo ni wewe pekee uliyewahi kuziona? Ama sehemu ngapi duniani ambazo umeziona wewe pekee?
NDIO:
Labda wasema ni siri kwa kuwa hakuna mwingine aliyekwambia ameiona sehemu hiyo, lakini labda mji mzima umeiona lakini hakuna anayetaka kusema kwa kuwa wanataka iwe siri.
LABDA:
SIRI ni mtazamo wa kifikra kukufanya ujione wa kipekee bila kuwa na namna ya kuthibitisha kuwa ni wa kipekee na ni mridhisho binafsi kujiona uko mbele ya wengine ambao ki-ukweli wamekutangulia.
TATIZO
La siri ni kuwa hutojua kuwa ni siri mpaka uifanye kutokuwa siri. Kwa maana nyingine ni mpaka umuulize mtu kama anajua kuhusu SIRI yako na akisema hajui, basi wajua kuwa ilikuwa siri kwani si siri tena baada ya kuisema ili kuhakikisha ni siri.
NA HATA:
Yule atokaye kufanyiwa upasuaji na rundo la madaktari na wauguzi anatoka kajifunga "taulo" akisema hataki watu waone sehemu zake za siri.
ATI NINI?
Ni sehemu za siri ambazo zimehudumiwa na watu makumi kidogo?
PENGINE:
Siri ni tafsiri binafsi kukufanya ujione wa kipekee
SAWASAWA
Na yule anyaye porini akidhani amejificha ilhali kuna wawindaji ambao kwa kuwa wanamuheshimu hawataka ashitukie kuwa wamemuona "akichojoa" na kushusha "kago"
NA
Huyo naye akitoka atasema "kafanya siri"
HIVI KUNA SEHEMU AMA KITU CHA SIRI???
TATIZI LA SIRI NI KUWA PUNDE UTAKAPOJUA KUWA NI SIRI, INAKUWA SI SIRI TENA KWANI NI LAZIMA UISEME KWA MTU NA MTU ASME "HAKUJUA" NA HAPO UTATAMBUA KUWA ILIKUWA SIRI, NA SASA SI SIRI TENA.
Na je!! Kama anakudanganya na kuku-enjoy je?
Basi hata maoni haya yaweke sirini.
Naacha
Tuonane NEXT IJAYO

Markus Mpangala. 3:43 pm  

NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA USITISHIKE......

hivi kuna SIRI na sehemu za SIRI ambazo tujuazo ni SIRI? Aise Mkuu Mzee wa Changamoto, umemaliza WAZO LOTE.....

Hivi rksa kubishia SIRI?

Markus Mpangala. 3:43 pm  

NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA USITISHIKE......

hivi kuna SIRI na sehemu za SIRI ambazo tujuazo ni SIRI? Aise Mkuu Mzee wa Changamoto, umemaliza WAZO LOTE.....

Hivi ruksa kubishia SIRI?

chib 3:51 pm  

Mzee wa Chngamoto katoa pointi zangu zote, yaani mimi nilikuwa na asilimia 5 tu ya yoooote aliyosema

Maisara Wastara 5:05 pm  

Mungu aliumba mwili lakini hakuumba sehemu za siri.

binadamu ndio waliotengeneza hizo sehemu za siri kwa sababu ya upofu wao....

jamani mie ni mgeni hapa....naomba kubisha hodi...

Yasinta Ngonyani 5:46 pm  

Simon :-( Ndio maana wanasema mficha uchi hazai..:-(

EDNA 10:39 am  

Mzee wa Changamoto umeongea yote hadi nakosa la kuchangia wajameni....Ila mie naamini hakuna sehemu za siri kama hujabahatika kumuonyesha mtu hiyo sehemu yako ya siri ukubwani basi wazazi wako walishaiona kitaaambo ukiwa mtoto mdogo....

Simon Kitururu 2:15 pm  

@WOTE: mmmh!

@Maisara: Karibu sana kijiweni!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP