Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tukiangalia uwezekano kwanini WIZI , uuzaji uchi au tu UCHAWI kwa kawaida INASEMEKANA auwezaye HUWA ni mtu MWINGINE na sio WEWE!:-(

>> Wednesday, May 26, 2010

[Tahadhari: Wazo katika taralila HII  limepinda !:-(]


Ukifikiria utastukia kuwa  katika kila uliogopalo kuna MWINGINE  anashamiri katika hilo bila UOGA uliokuwa nao KUHUSU HILO  wewe.:-(


Swali:
  • AU?
Ndio maana,...
..... uchochoro UUOGOPAO  kuupita  kuna ambaye hauogopi na kageuza hapo makao a.k.a OFISI  yake ya KUKABIA watu ambaye kwa jina la kitaalamu huyo ni mjanja kwako.:-(


Ndio maana,....
.... kwa  uogopaye WACHAWI  unajua kuwa kuna watu ambao hawaogopi uchawi  kitu ambacho kimewasaidia zaidi ya kutoogopa uchawi kuliko aogopaye uchawi wamekuwa wenyewe WACHAWI  labda HATA katika eneo lako.:-(

Ndio maana,....
.... katika ujasilimiamali weye ukichacha hata kama ulishawahi kujichungulia ukastukia unasehemu nyeti kisura ambazo zinauzika MTAANI na unawajua  waliojenga nyumba na kupandishwa vyeo kwa UFUNDI wa tumizi la NYETI  waweza kujikuta unaogopa kufanya mauzo ya NYETI ZAKO NONO kama wengine ambao walitatua tatizo lako  katika eneo lako kwa mauzo ya kiungo kitu ambacho unaamini hakiwezekani kwako.

Swali:
  • Sasa kwanini wengine na sio wewe?
  • Unafikiri wengine wanakuzidi nini mpaka wanafanikiwa kuwa mafisadi  katika UFISADI uushindwao , wakati wewe unadai unamuogopa Mungu hata kuonjesha watu uzinzi kama wenzio wafanyao UZINZI ambao vifaa vyake vya tumizi kama hamu na pembejeo za kazi unazo?


Ndio,....
.... inasemekana MAKUZI ya mtu yanaweza kumsaidia mtu kutokuwa na tabia ya kudokoa MBOGA JIKONI hasa akihisi hakuna watu.


Ndio,...
.....inasemekana  MAZINGIRA yanasaidia  kurahisisha baadhi ya MDADAZ  kutoa nyonyo kwenye umati KIRAHISI ZAIDI katika swala muhimu la kucheza SINDIMBA KIFUA WAZI  hata kama tukiachilia mbali lile swala la KUTOA NYONYO  kirahisi zaidi kwa baadhi ya mdadaz HADHARANI katika kunyonyesha TU toto  lenye njaa ambalo limeanza kulilia NYONYO a.k.a HOTELI YA MTOTO mbele za watu.:-(


Ndio,...
....inasemekana ELIMU inaweza kusababisha MTINDIO WA AKILI usababishao  TOFAUTI YA WASOMI WAWILI  usababishao aliyeelimishwa KIKRISTO akubaliane na MTINDIO WA AKILI wakuwa UKIPIGWA KIBAO SHAVU MOJA geuza na jingine UBWENGWE TENA na aliyeelimishwa KIISLAMU au KIYAHUDI  apate MTINDIO WAAKILI umsababishao UKIMBWENGA KOFI SHAVU la kulia  akurukie kichwa halafu kabla hujatulia akukabekabali ifuatwayo na gonge la ngwala  na kama unamakende labda ayasigine wakati  anakutukana PAMBAFU WEYE mbele za watu.:-(


Swali:
  • Unabisha?

Cha kusikitisha ni kwamba,....

.... labda weye kisa sio MWIZI, malaya na UNAOGOPA WACHAWI,  giza na unatabia pia ya KUTOPENDA ukitoka tu chooni mtu MWINGINE aingie baada yako kwa kuwa unajua unautaalamu mkubwa wa kunukisha choo HARUFU MBAYA  kitu ambacho hupendi watu wajue,...

... tabia zote hizo  labda ni zako tu kwa kuwa kama ni MALEZI , mazingira  hata elimu , vyote vinalingana na wengine kwenye familia yako BABA mmoja na MAMA mmoja  mliokulia nyumba moja mkaenda shule moja   WASIO NA TABIA HIZO  na pia hata katika  MTAA WENU pale kijijini  JANGILI, mwizi wa mapera  na FISADI wote ni ndugu zako wa damu ingawa baba aliwazaa nje NA WEYE eti  ni ASKOFU ambaye mtoto wako wa pili wakike atakuwa mchawi baadaye akikua vizuri baada ya jitihada zako zote za MALEZI mazuri ya staili za kumfunza kumuogopa MUNGU vizuri.:-(


Cha kusikitisha ni kwamba,....

.....labda WENGINE wanaonekana wanaweza ndio maana ni MAPROFESA siku hizi ingawa wewe ulikuwa unawazidi akili darasani na  bado weye ni mesenja kwa kuwa tu HUJARIBU KITU  hata katika kusawazisha tu maisha yako kitu ambacho kimekusaidia kutogeuka MALAYA au mchawi  au tu kisababishacho watu usiue,...

.....ingawa pia kimesababisha usijaribu kwenda shule  ANGALAU YA MASWALA YA JANDO zaidi angalau ikusaidie kumridhisha umjaliye zaidi hapa duniani ambaye ni MKE WAKO angalau katika tendo lililobarikiwa na SHEKHE liwasaidie kuujaza ulimwengu hata wakati lengo la tendo ilikuwa liwe ni KIBURUDISHO MURUA TU, wakati MKEO ANARIDHIKA  vizuri.:-(



Swali:

  • AU?

NDIO,...
..... ni kweli KADODA sio KADALA,.....

......na labda hiyo ndio sababu kubwa ingawa GIZA lisilo mdhuru  KADALA  hilo halimdhuru KADODA,...

...ila KADODA anaweza geuka JAMBAZI ajifichaye GIZANI na KADALA akageuka aogopaye GIZA kwa kuhofia ajifichaye gizani ingawa kiukweli KADALA hamuogopi KADODA  mchana.


Swali:
  • Ushawahi kujiuliza kwanini aogopaye MAJINI  hajiulizi inakuaje kuna mwingine kazi yake ni kwenda kwenye wenye MAJINI ili kuyaagua na kuyafukuzilia mbali?

  • Ushawahi kujiuliza kwanini UOGOPACHO kukifanya na hapa siongelei swala la kujamba hadharani wengine wanakifanya hilo KIRAHISI kama wanafyonza AISHIKIRIMU YA UKWAJU vile kitu ambacho weye huwezi?


Ndio,...
..... WEWE sio WAO na labda ndio maana LIMPENZI lako baya NA HULIPENDI VIZURI  ingawa lenyewe LINAKUPENDA SANA kitu kilichorahisisha ukonalo  kwa kuwa ulipendalo kikweli lile ZURI  KINOMA UNALIOGOPA KULIAMBIA kitu ambacho wenzio wanafanikiwa KUFANYA ndio maana wana LIMPENZI ZURI ingawa limpenzi lenyewe eti HALIWAPENDI VIZURI.:-(

Ndio,...
.... labda MALEZI, elimu, MAZINGIRA na.......
.... vyote vinategemea wewe ulizaliwa ni MTU WA AINA GANI na kuna uwezekano pamoja na KUKULIA MAZINGIRA ambayo UZINZI ni DHAMBI ukifanya mazoezi vya kutosha unaweza kujikuta weye ni PROFESA WA UZINZI kama tu wengine ambao wamefanyia mazoezi UFISADI, KABUMBU, au hata kubulogi walivyogeuka MAHIRI ingawa hawakuzaliwa  kukiwa na KOMPYUTA na wala BLOGU hazikuwepo.:-(


Swali:
  • Hivi si kuna uwezekano kila mtu kazaliwa na chembechembe za UFISADI kwa hiyo klihitajikacho ni NAFASI ya KUFISADI na MAZOEZI ya kunoa jinsi ya KUFISADI vizuri bila kudakwa kama MAFISADI mahiri wajulikano ila ushahidi hakuna?

  • Unauhakika kwanini ni WENGINE na sio wewe MALAYA wakati mchakato wa maisha ni uleule kwako na kwao?
Ndio,...
....Nakubaliana na WEWE,...
...kunyoshea wengine vidole KUNA utamu wake.:-(


NAACHA WAZO hili nikishukuru uwepo wa MIMI na WEWE, wao na WALE kitu kisaidiacho uwepo wa MAFISADI kwa kila uwepo waogopao KUFISADI, uwepo wa MALAYA kwa kila awapo mchoyo wa kuuza tendo la unyumba, UWEPO wa WENYE IMANI KALI kwa kila WAWAPO WASIO AMINI kitu ambacho kinaifanya DUNIA HII iko ilivyo kitu ambacho naaamini  hakiko HIVI au HAKIKUUMBWA KIWE HIVI KIBAHATI MBAYA  !:-(

Nakutakia SIKU KIBONGE Mheshimiwa hasa ukikumbuka hili NI WAZO TU!:-(

Tubadili MUSHKELI kwa kumsikiliza YOUSSOU N'DOUR anyuke mkito-Bamba



Afroman abadili kidogo kwa -Because I got High



Au tu Warrior King aje live katikakurudisha ustaarabu mkuno -Education

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 2:56 pm  

Mweee! kazi kwelikweli siku hizi nilikuwa nazimiss maandishi haya nanukuu " WEWE sio WAO na labda ndio maana LIMPENZI lako baya NA HULIPENDI VIZURI ingawa lenyewe LINAKUPENDA SANA kitu kilichorahisisha ukonalo kwa kuwa ulipendalo kikweli lile ZURI KINOMA UNALIOGOPA KULIAMBIA kitu ambacho wenzio wanafanikiwa KUFANYA ndio maana wana LIMPENZI ZURI ingawa limpenzi lenyewe eti HALIWAPENDI VIZURI.:-(" hapa nimepapenda Ahsante Mtakatifu

Fadhy Mtanga 3:37 pm  

unaweza tu kujishtukia kuwa kile ukiogopacho kukifanya OFISINI ndicho kilichosababisha MSELANONDO malavidavi awe na ubabe wa kujenga BANGALOO lake babkubwa kule mitaa ya MBEZI bEACH wakati wewe na sera zako za kijamaa bado unaishi nyumba ya kupanga ya chumba kimoja pale KIGOGO huku mselanondo huyohuyo ambaye sasa anageuka na kuwa MCHIZENI bila woga wowote anaamua pia kumkimbiza LIGWARIDE mkeo mpendwa aka sweet heart huku akimfanyia MAMBO makubwa ambayo wewe kibonge uliyenogewa na mafundisho ya dini yako kuwa ni HARAMU kwa sababu tu wewe ni mtu uogopaye kuyafanya hayo huku ukiwa hufahamu mkeo anayeufahamu WOGA wako ni mshabiki mzuri wa KAMCHEZO hako huku akijitia hana habari kabisa ukiwepo na saundi nyingi za kuchoka kumbe ukienda tu kazini naye anakutana mahali na KIJANA braza huyo ambaye anampakulia MAVITUZI yote bila kubakiza.

Woga bwana!

Fadhy Mtanga 3:37 pm  
This comment has been removed by the author.
Fadhy Mtanga 3:37 pm  
This comment has been removed by the author.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP