Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAONYO ya kileo kwa adhaniwaye anatafuta POOZEO au MCHUMBA !

>> Wednesday, May 19, 2010



``SIMON eeh, MSICHANA ana kesi huyo!´´- ni moja ya onyo hasa marafiki zangu wa MOROGORO hunipa pale wakihisi kuna ZALI aka MTOTO MZURI ananilenga au tu kinamna imetokea mie mwenyewe nimelisifia ZALI kitu nikimaanisha labda mwendo, dimpozi au tu miakili ya kimwana katika kunyambulisha hoja za kitu zikatokea kustua marafiki zangu kuna kunafununu ya kaudhaifu napandikiza kwa ZALI  ,....

.... kitu ambacho kinawafanya wawe na wasiwasi nini kitatokea bila miye kuijua HISTORIA ya KIMWANA.

Na wakisema MTU ana kesi MAANA YAKE huwa kuwa inajulikana kashafiwa labda na MME wake, Mke wake, poozeo, au tu shughuli zake vitani wengi wanamuhusisha na mauaji ya MPENDWA mtoto wa mtu ambaye anaitwa marehemu siku hizi kutokana na gonjwa wajanja walihisio lilipewa ujanja na busti ya mashambulizi kwa kuwa mwilini alikuwa hana KINGA YA MWILI.:-(


Kwa kifupi,...
... katika pitapita zangu hasa MOROGORO na ARUSHA nimekutana na mazingira yanikumbushayo stori nilizokuwa nasikia kutoka kwa BABU upareni jinsi utafiti ulivyokuwa unafanywa katika kuhakikisha KIDUME anaopoa ZALI lililotafitiwa ili kuhakikisha KIDUME huingii zali katika kujipatia KIMWANA.


Kwa kifupi zaidi hasa kama wewe hujatokea BONGo kwa muda mrefu,....
......siku hizi SI JAMBO LA AJABU  ukimchekea mtu wakujalio KUKUSHUSHIA BONGE la historia ya UMCHEKEAYE hasa katika mrengo wa  ana KESI NGAPI.:-(

Swali:
  • Unafikiri leo hapa BONGO kama hupuuzii mambo unaweza kujiamini KUPENDA mtu?

Samahani NAANZA UPYA taralila hii kwa mwendo wa kusuasua!

UKIMWI UPO!

....Ila UKIMWI wa watu kumtungia mtu nao UMESHAMIRI maeneo kibao niliyokatiza TANZANIA na KENYA mpaka sasa.


Lakini MAPENZI yapo!

... labda pia ni kitu kizuri HICHO kuwa bado MAPENZI YANASHAMIRI hata kwa wale ambao kwa kuwa WAMEWAHI KUFIWA basi ukiwachekea WANAOKUJALI hata kwa sauti ya zaidi ya ile ya TISHA TOTO watakustua kuwa TOTO ZURI lina kesi a.k.a LIMESHAFIWA tayari na limpenzi lake.:-(



NA ile sifa ya PESA kuwa ni sabuni ya roho bado IPO!

... na PESA  katika uwajibikaji wake hasa UKIDHANIWA UNA PESA unaweza kujikuta kuwa kuanzia MALAYA, wababaikaji wa kawaida au mpaka mchumba wa ASKOFU  wote wamekulenga na kama unajali TAMUTAMU ZA GHAFLA unaweza kujikuta umejitafutia kesi KILAINI wakati wala hupendwi wewe ila ni POCHI lako tu ambalo wala halina kitu kihivyo hasa ukizingatia pesa zilizotunisha POCHI labda ni kodi ya nyumba kwa kuwa kujenga NYUMBA  pesa huna.:-(


Swali:
  • Unafikiri ni wangapi wametungiwa kuwa wanamdudu BONGO nyoso na wapiga taralila tu?
  • Hivi wewe hujawahi kutishika na LIMTU  zuri kisa maonyo ya watu ?
  • Unafikiri watu wanatoa wapi historia na siri  za watu ukizingatia  ukiulizia unaweza ambiwa mapaka ya chumbani kwa watu  na watu ambao hata sebuleni kwa huyo mtu hawajawahi kuingia?

Ni STORI FUPI tu nazokutananazo safarini MHESHIMIWA na wala usijali kwa kuwa NAACHIA HAPA.
Ngojea miye niende zangu BAA kufanya mazoezi ya kuacha kunywa POMBE unajua tena wikiendi bado.:-(
BAADAYE!

Hebu tujikumbushe Loon wa enzi za Badboy akiwa na Mario Winans katika mnyuko- Down For Me


Au ngojea tujikumbushe Loon aongeleye UISLAMU na Allah baada ya kugeuka

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Faith S Hilary 1:31 am  

Yote uliyosema ni kweli kabisa kaka, watu wanamuongelea mtu, yawe ya kweli ama uongo basi tu watu wataongea. Hii inaweza kusababishwa na tabia ya mtu anapoonekana pale "mtaani" au mmoja kati ya wanaoongea au mtu tu katongoza then katolewa nje then anaamua amchafue mtu so ndio wanasema "chuki binafsi"...watu hatari si mchezo! hehe

Fadhy Mtanga 8:18 am  

Taralila ya leo ni FUNGA kazi kwa kuwa tu aliyeiandika taralila hii ni YULE ambaye alikuwa na UKAME a.k.a ugwadu wa warembo wa kibongo aka VICHUNCHUNA kiasi kwamba jamaa akawa anakodolea macho a.k.a kutokwa na udenda kiasi cha kuwashitua marafiki zake pale mji kasoro hata wakaamua kuanza kuwabambikia kesi VISHTOBE hao kwa kuhofia jamaa yao RASTA kutoka majuu anaweza kujisahau na kuhonga pesa zote a.k.a KUMWAGA MPUNGA kiasi cha wao kukosa pesa ya kwendea BAA kufanya mazoezi ya kuacha pombe!

o'Wambura Ng'wanambiti! 10:52 am  

"Unafikiri leo hapa BONGO kama hupuuzii mambo unaweza kujiamini KUPENDA mtu?"

Kupenda ama kutaka kuonja? :-(

Enhee! hivi yawezakuwa nawe ukishaambiwa hivo ya kwako nayo yataelezwa kuwa UMESHADATA ndo sababu uko hapo na majuu ushafukuzwa na jivu la volcano liloahirisha ndege huko ulaya? :-(

chib 1:27 pm  

Mt... umenena ukweli, lakini tahadhari nayo ni muhimu....
Yote kwa yote, uliposema unaenda BAA katika harakati za kuacha unywaji, tena katikati ya wiki umeniacha hoi na mbavu zinauma ile mbaya kwa kucheka.
Sijui kwa nini sikukuta Dar nikacheka.
Denge... juuuuuu

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 4:34 pm  

Utaambiwa karibu kila mtu ana KESI...Cha ajabu ni kwamba karibu kila mtu anajua kwamba fulani ana KESI lakini "mdundiko" unaendelea bila gogoro. Mimi nadhani tumefika mahali sasa watu wameshachoka au pengine hawajali tena. Ndiyo maana UKIMWI unazidi kupeta tu.

Jana nilisikiliza mahojiano marefu katika redio moja makini hapa (NPR) na walikuwa wanamhoji daktari mmoja kutoka Uganda ambaye anashughulikia na mambo ya UKIMWI. Alisema kwamba yanayotokea Afrika yanakinza karibu vitu vyote tunavyojua kuhusu uzuiaji wa kuenea kwa magonjwa. Eti watu wakihabarishwa sana basi maambukizi yatapungua. Alisema kwamba baada ya muda mrefu wa kushuka kwa maambukizi ya UKIMWI Uganda, sasa maambukizi yameanza kupanda tena na hii inashangaza kwani karibu kila mtu anaujua jinsi ugonjwa huu unavyoenezwa, kinga, madhara yake n.k.

Kama watu wamechoka - na kama kila mtu ana KESI watu wafanye nini moto unapoanza kuwaka viunoni?

Ngoja nami nikimbilie hapa McDonalds nikajaribu kupunguza uzito!

mdoti Com-kom 1:02 pm  

Am back! nitembelee!Nadhani tuwe wawazi japo kwa tahadhari. Kuna haja hata ya kufanya edition ya biblia ili kuwanusuru hasa makasisi.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP