Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Daraja!

>> Wednesday, May 09, 2007


Ni Kiungo.....
Kiunganishacho kulia na kushoto....
mwa kulia na mwako shoto

Ni Kivuko.....
Kikuvukishacho ukikimbilia hata moto....

Ni Maisha....
yalo shwari ,tulia kama bahari....
kwani waweza lia kabla kuona pwani..

Mwisho wa mwisho daraja ni daraja

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 6:28 pm  

Daraja,daraja inaweza kuwa kiunganisha cha pande mbili tofauti.kwa mfano daraja kubwa kati ya inchi tajiri na inchi zinazo endelea.

Daraja si kiunganishi,kwamfano familiambili tofauti,familia A inapata kila kitu na familia B inakosa hata mlo mmoja.

Daraja ni ubaguzi kwa mfano pale rangi ya mwili inatawala.

Mwisho kabisa Daraja libomolewe na kutupiliwa mbali,wote ni binadamu kama ni kuishi katika nyumba ya aina moja au kulala kitandani au kula chakula cha aina moja.Kama wote tuvae Suti kama Mzee Simon au?

Daraja linabaguwa,linajaza chuki na wivu,daraja linazaa majambazi na kujima haki.

Daraja lobomolewe.Jah Rastafarian.

Mjengwa 9:59 am  

Simon,
Unanikumbusha daraja la kule nyumbani Moro! Asante sana kwa kazi nzuri.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP