Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika Mwaka Umelala Miezi mingapi?

>> Wednesday, May 16, 2007


Usistuke!Najiuliza tu! Si unajua tena kale kamchezo ka nusu kufa tukafanyako?
Duh!Na maanisha kulalaaaaa!Samahani , nimekumbuka kuna watu mwiko kusema kufa!
Sasa ......
Si umestukia mwaka unavyotoweka wakati huu mradi wa kuishi hauonyeshi sana mazao yake?
Usistukeeeeeee!
Wote tulikuwa macho miezi kadhaa tu!Mingine tulikuwa tumelala kwa kisingizio usiku umeingia.
Halafu katika miezi tuliokuwa macho tuli:

  • Enda kwenye kitchen party
  • Hatukumisi kisimani kungojea kama Zubeda atatokea ,ili apatiwe ile kauli
  • Tuliugua kichwa na kuchoshwa na kua macho
  • Tukatumia muda kujifunza mambo yasiyotusaidia kitu
  • Tulichukua njia ndefu badala ya fupi kumkwepa Abdallah ,tuliye mkopa
  • Tukachukua kale kamda kengine , tumepoa tu kwa kukosa kujua tufanye nini
  • Tulifanya pia nanihiii,... na zile kadhalika kadhaaa.......
Duh!
Umestukia kama unasoma hapa, maana yake uko macho eeeh?

Siku njema!


Lakini ngoja nimuache anonymous anizinguaye Lagbaja

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP