Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUHUSU ile LAWALAWA ichocheayo UKIMWI

>> Friday, May 11, 2007


Kabla sijasema......
Mcheki DANY ENGOBO


Binadamu tu wadhaifu!
Na vichocheo vya maswala ya ngono ndio vinazidi kujaa.Sababu kubwa ni sisi wenyewe binadamu kupenda au kushindwa kuepuka matamanio ya kimwili ambayo tumezaliwa nayo.Kuna kipindi matamanio ya kimwili yalikuwa ni kuhakikisha tunaendelea kuzaliana,lakini jinsi muda unavyokwenda, ngono imekuwa ni starehe zaidi ya uzazi.

Hata kwa wale waonekanao watu wa dini, mara nyingi hakuna tofauti sana. Nakumbuka enzi zangu wakati sikosi katika maswala ya dini. Nakumbuka wakati naimba kwaya kanisani, ilikuwa ni balaa! Huwezi kuamini jinsi watu wanavyoweza kusikiliza neno la Mungu wakati wakijiandaa kwenda kufanya ngono mara tu baada ya kutoka kanisani. Si unajua tena kuna watoto wa geti kali huruhusiwa kwenda kanisani tu.Hivyo muda huo huo inabidi utumiwe kufanyia shughuli ili arudi nyumbani bila kustukiwa alikuwa kapitia geto.

Tukiachana na kamfano hao juu...

  • Nilikua tu nataka tukumbushane hii ijumaa kuwa ni ukweli kwamba UKIMWI upo na unaua.
  • Na matamanio yapo na yataendelea kuwepo.
Najua ni jambo tulijualo!Lakini najua pia pamoja na kwamba wote tunajua , huwa tunatetereka mara nyingine!Hivyo hakuna haja ya kusahau kuwa huyu mdudu atatuondoa tukijisahau.

Haya tena!Tucheze kwa uangalifu!

Ijumaa njema!
Nakuacha na majaribu mengine ,yajayo kwa mtindo wa wimbo huu-KIUNO

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MTANZANIA. 6:56 am  

Simon,
Wengine wanasema bila Sukari Mungu labda tungepona. Lkn sukari hii ilikuwepo toka zamani. Cha msingi ni kulamba sukari kwa adabu,utii na heshima kubwa kama inavyoelekezwa.

Wikiendi njema.

Anonymous 10:53 pm  

Umenikumbusha Princess Farida ambaye kaacha kuutingisha kiuno kisha 'kaokolewa' na kuolewa na pastor...maisha hayo!

Simon Kitururu 1:22 am  

@Mtanzania:Kweli tupu usemalo
@Serina:Maisha simchezo.Hukawii kukuta Askofu kawa jambazi na jambazi kageuka muhubiri.Watu hugeuka

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP