Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ee Bwana eeh!NAKUTANIA TU!

>> Wednesday, May 30, 2007

Si ushagundua utani unahitaji muwe zaidi ya mtu mmoja eeh?

Nafikiri ni kwa sababu kama nakutania basi lazima awepo atakaye chekeshwa na utani wangu.Nikikuita kwenye kona tukawa wawili tu halafu nikaanza kukutania , hainogi.
Labda mpaka nikutishie kuwa nitawashtua washkaji kuhusu hako kakitu nakokatumia kama kigezo cha kukutania.

Duh!
Inasemekana asilimia kubwa ya wachekeshaji ni watu wenye huzuni!

Lakini hili neno utani
...... na hiki kisentensi, nakutania
vinamambo yake!

Eti utani mara nyingi hufikia kwenye hiki kisentesi:Ee bwana eeh !Mimi sitaki utani, nitakubamiza wewe!Ohooo!

Au unakumbuka haka kasentensi:
Mimi sio mtani wako utalia sasa hivi!

Basi,
kautani kakifikia hapo, watu wengi hudai kuwa kameingiliwa na kaukweli ndani yake!

Swali:
Hivi utani ni uongo eeh?

Duh!
Uongo si dhambi lakini?

Lakini eti nasikia kuna uongo na uongo. kamoja ni haka kauongo keupe(white lie),haka eti sio kabaya sana.

Swali:
Hivi kale kauongo kengine kabaya kanaitwaje vile?

Sasa tukirudi kwenye utani.......

Ukifuatilia utani na haka kasentensi; nakutania tu! Utastukia nakutania tu, inatumika kupunguza makali ya utani ili usichukie.

Kwa hiyo jihadhari na kasentensi nakutania tu kwa sababu kanamaanisha mtaniaji kakuweka kwenye kona tayari.

Duh!
Kwahiyo utani una uhusiano na vichekesho lakini hauko mbali na huzuni au chuki.

Swali:
Ushawahi kuchekeshwa na kitu cha kuhuzunisha?

Usistuke sana!
Nadhani hakuna aliyeshuhudia ukicheka mtu akianguka!
Duh!
Lakini hivi ni kweli ulitaka kumcheka kilema siku moja katika dansi?
Duh!Basi bwana, hiyo siri yako!


Ngojea umsikie Chris Rock akichekesha hapa kuhusu mahusiano ya mwanamke na mwanaume!(kama hujakatiza miaka ya kumi na nane labda usimsikilize lakini)

Okei labda anatania......


Msikilize Eddie Murphy hapa akiongelea matatizo ya kusubiria nanihii....Duh!(kama ukochini ya miaka 18 labda usimsikilize)....


Duh!
Ngoje turudi kwenye NAKUTANIA TU.........!
Au kwenye Utani!

Swali:
Hivi utani ni nini?
Nakuacha na Eric Clapton

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP