Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hivi Jirani Kala nini?

>> Tuesday, May 08, 2007


Kuna mambo mengine ni binafsi utake usitake.Lakini cha ajabu kuna mambo ya binafsi ya watu tunapenda sana kuyafuatilia. Na wengine tunapenda vile vile kuwashirisha watu katika mambo ya binafsi.Hilo lisisahaulike!

Cha kujiuliza ni , kwanini kuna habari muhimu ambazo haziwavutii watu kama habari za ajabuajabu za watu fulani?

Ukipitia katika tovuti mbalimbali , utakuta mpaka Afrika takwimu zinaonyesha watu walikuwa wanafuatilia sana habari ya Clinton na Monica Lewinsky kuliko habari za Clinton na maendeleo ya nchi zinazoendelea.
Hivi sasa Tanzania ni rahisi kustukia watu wakijadili Amina Chifupa
na matatizo yake ya ndoa kuliko ugonjwa wa Tetanasi , urudio kwa nguvu.

Lakini hili jambo linasababu zake !

Ukiniuliza mimi kwanini karibu dunia nzima umbeya una afya sana, naweza kusema sababu kubwa inatokana na mapungufu yetu binafsi.

  • Wengi hufarijika kustukia kuwa kumbe na wengine wanamatatizo kamasisi
  • Wengi hufarijika kujua kwa kujilinganisha na wengine tumewini au ndo tuko bado palepale.
  • Wengine tunafarijika tu kusikia kuwa na wale tufikiriao wako safi na wamefanikiwa kupita kiasi, nao wana matatizo yao kama sisi.
  • Wengine hutaka tu kujua jirani kala nini bila la msingi zaidi ya kutaka kujua anapataje kitambi.
  • Kwa kifupi ni mchezo wa saikolojia ,uzaliwao katika harakati za kutaka kujua sehemu yetu katika jamii na pia kutaka kujua yale tunayofichwa kujua, na hivyo kuyafanya yawe yanavutia.
Sasa ....
Utaniuliza kwanini nia ya kutaka kujua mambo fulani ambayo umbea hutusaidia majibu unanguvu kwa wengi kuliko kutaka kujua serikali ya Tanzania inatumiaje kodi.

Jibu:
sijui!

Lakini, nacho jua ni kwamba kufuatilia kodi zimeenda wapi ni jambo gumu. Ukikumbuka kuwa sisi binadamu ni wavivu kwa asilia. Ni rahisi kuchukua jambo rahisi kama vile tulivyo kuwa tunataka kufuatilia mwalimu darasani kavaa chupi ya rangi gani, au swala kama ; siku hizi kwa akina Kitururu bado wanakula mlenda tu?

Pili naamini maswala ya umbea kila mtu anaweza kujadili kwa ufasaha. Umbea kila mtu anaweza kwa ufasaha zaidi ingawa baadhi yetu kama vile katika kitu chochote tunaweza tukawa mabingwa zaidi, hasa kutokana na jinsi gani tulivyougawia umbea muda wetu wa wakati tuko macho.

Lakini pia tukumbuke kuwa ni wengi watafuata mambo rahisi, habari rahisi, lakini wapo wapatao kuridhishwa na maswala magumu. Ila wafuatao mambo magumu watakuwa wachache daima. Tufuatayo marahisi tutashinda kura kama mtu ataitisha uchaguzi.

Swali:
Unafikiri umbea na mambo ya umbea si muhimu katika jamii?

Ukiniuliza.......
Nnitasema kuwa umbea na mambo ya umbea ni muhimu katika jamii. Lakini umbea na mambo ya umbea yakitawala kunahatari kubwa kuwa asilimia kubwa ya watu itakuwa haijui kuchambua mambo ya maana.Asilimia ndogo ya wajuao na wenye kujua jinsi ya kutumia muda wao vizuri katika mambo muhimu na ya umbeya watakua katika nafasi nzuri ya kuwashinda wafuatiliao umbea tu.
Kitu ambacho kitasababisha wambea waendelee kutaka kujua vya siri vya wawahisio kutofautiananao katika jamii.

Lakini si ushakutana na apendaye mwenyewe kukuhadithia vya siri?

Hawa lazima watakuwepo.Nao wanakidhi kitu hicho hicho ; kwa kukuambia hujijua na kukujua, na kujipa auheni ya kuongelea jambo ambalo halitaki ujuzi.

Ushastukia unavyojisikia vibaya ukijadili jambo la maana halafu ukastukiwa hujui?Ushastukia hujali sana asilimia ya ujuzi wako wakati unakabiliana na mbwembwe za kusikiliza au kutoa umbea?

Lakini unakumbuka stori ya umbeya inaanzaje?
Hapa na maanisha kianzio kama vile utakapo kusimulia hadithi unaanza:Hadithi hadithi!Hadithi njoo utamu kolea............

Duh!.
Ngoja ni rudi kwenye Jirani kala Nini...................

Hivi jirani kala nini?

Duh!
Sijui!


Amina Chifupa na ndoa yake je?

Duh!
Sijui!

Kodi ya wananchi Tanzania inatumiwaje?

Duh!
Sijui!Ingawa kunakipindi nilidhani najua.

Haya tena!Siku njema!
Namuacha Tracy Chapman


1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 6:32 pm  

luihamu_lui@yahoo.co.uk
AU?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP