Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Raisi Nyerere na Mobutu Seseseko Kama Kurwa na Doto!

>> Wednesday, May 02, 2007



Unaweza kubisha kuwa hakuna cha kufananisha kati ya Raisi Julius Kambarage Nyerere na Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga.
Lakini ukijiuliza sana unaweza kustukia kuwa inawezekana ni aina tu ya nguvu na jinsi ya kujiridhisha, ndivyo vilivyokuwa tofauti, ndivyo vilivyosababisha tofauti ya machaguo yao ya nini muhimu.

Dondoo:
Unajua watu wengi hujiridhisha wenyewe kwa kutumia njia ya kuridhisha wengine?


Ni kawaida kabisa kumsifia Nyerere kuwa alikuwa mtu wa watu na kumkandia Mobutu katika hilo.Sababu kubwa ni jinsi Nyerere alivyojaribu kuwa karibu na wananchi wa kawaida na Mobutu alivyojaribu kuwa Mfalme na kuwa karibu na matajiri.Ukiwauliza famili za akina George Bush , wanaweza kukuambia Mobutu alikuwa poa sana!

Swali:
Hivi Nyerere alikuwa karibu na watu wa kawaida kama mimi na wewe?

Labda........................!

Ni kweli sera zake nyingi zilionyesha moyo wake wakutaka kumuendeleza mtu wa kawaida.
Lakini tusisahau kuwa mambo mengi pia yalikuwa ni majaribio yake mwenyewe ambayo utekelezaji wake na mantiki zake unaweza kuzihoji usipate jibu.Naamini yako mengi tumsifiayo kwakututendea ,alikuwa tu katika mudi yakufanya kimridhishacho binafsi , ambacho kiliwezekana kutimizwa kisaikolojia kwakutufikiria siye.

Sasa tukirudi katika kwanini inawezekana kiini cha Nyerere na Mobutu kuchagua chochoro tofauti za kufuata kinaweza kabisa kuwa kimoja..............................................

  • Mobutu mpaka kuitwa dikteta ilitokana na kupenda kutawala na kuwa na nguvu kwa wengine kwa kutumia kile akiwezacho binafsi.
  • Nyerere mpaka kuitwa Mwalimu na baba wa Taifa , naamini ni kwasababu pamoja na kupenda kutawala, aliweza kutawala na kuwa na nguvu kwa watu tokea kuzaliwa kwake.Alizaliwa kwenye uchifu, aliweza kwenda shule katika kipindi ambacho Tanzania haikuwa na wasomi wakutosha. Baada ya kutawala Taifa nzima likamwita Baba wa Taifa , mwalimu, nk .hivyo alikuwa na nguvu kwa watawaliwa na watawala hata asingekuwa na ofisi.Hivyo kufupisha stori, Nyerere alitawala kutokana na kilichomjiakatika uwezo wake binafsi.

Hivyo inawezekana kabisa kuwa Nyerere hakua na haja ya kujisumbua kuwa dikteta wakati haki yake ya kutawala na nguvu yake kwenye jamii ilikuwa kubwa hata bila ya kujitangaza kuwa Mfalme wa Tanzania.Kisaikolojia kahamu ka ufalme kwake kalishatimia

Mobutu yeye hata Uraisi alipora!Lakini inawezekana kilichokuwa kina msukuma ni kilekile kilicho msukuma Nyerere.Ila yeye hakuwa na nguvu za kama Nyerere za kujifariji hamu yake ya kuongoza na kuwa na nguvu katika jamii yake bila kutumia nguvu za pesa na jeshi lililomsaidia kuchukua Uraisi kwa kupora.Pesa kwake ilikuwa muhimu ili awazidi wengine ili wamuonee gele na kumuogopa kinguvu.

Swali:
Hivi unafikiri Nyerere alikuwa maskini?

Katika kale kahamu kakujifajiri kwa yale tuliyonayo kwenye jamii hasa yanayo tengeneza sura tonekanayo kwenye jamii , kila mtu anastaili yake.

Kama hapa duniani wote tungezaliwa bila macho nafikiri kunawengi wasingeyajali mengi wayajalio sasa hivi.

Swali:
Ushastukia ukisafiri kwenda sehemu watu wasipokujua tabia yako inageuka kidogo?

Wengine tuletutabiatwetu tubaya ndio tunatuachia bila kujali, tukiwa maeneo wasiyotujua.
Si unajua tena ile tabia ya kwani nani ananijua?
Halafu nasikia wengine huko vijijini Tanzania tunapata sana marafiki wa jinsia ya tofauti kutokana na kamba tuwafungazo kutokana na ukweli hawatujui.Nasikia hako katabia kamepeleka sana UKIMWI vijijini.

Duh............!

Tukirudii katika kujulikana kwa Kurwa Nyerere na Doto Mobutu....

  • Nyerere, wote tulikua tunamjua.Na moja ya sifa zake ni kwamba mtu watu, anaakili sana, anajua karibu kila kitu.Halafu usisahau alikuwa na jeshi la masususu , ambao kuna kipindi ukiwa na Colgeti nyumbani wageni wakija inabidi muifiche kuogopa labda utaonekana mbadhirifu wa mali ya umma. Nguvu hii na kisaikolojia alikuwa kajitosheleza.Hivyo wengi hata kumbishia walikuwa wnashindwa hata walipoona anakosea. Duh!Aka kasifa kake kamekaa kidikteta kidogo lakini!

Tukienda kwa Mobutu hata mengi ya kusema hakuna. Ukimuondolea pesa ambazo alikuwa anajichukulia serikalini, na mavazi yake fulani ya ghali ya kimagharibi na ya kiafrika ya kifalme, alikuwa hana mengi ya kukutisha.Hivyo yeye kufikia kastarehe ka Nyerere ilibidi ang'ang'anie nguvu na ajaribu kwa nguvu sana kuhakikisha kuwa unamuona yeye zaidi kuliko wewe....

Lakini kuhusu kurwa na doto hawa(Namaanisha Nyerere na Mobutu) , unaweza kunibishia........!

Lakini nachojua sisi wote pamoja na kutaka kukatishwa tamaa na mengi , bado tunahangaikia U-Utopia!
Na katika hili la kuangalia jamii tuishizo mara kibao watu tofauti huliona swala moja kitofauti.
Si katai mchango wa Nyerere kwa Tanzania na mimi binafsi.

Lakini........

Na sikatai mchango wa Mobutu ambaye pia kama ujamaa wa Nyerere ulivyoonyesha mushkeli katika utekelezaji, na udikteta na ufahari wa Mobutu umetuonyesha mapungufu yake.

Haya basi tuendelee kuutafuta huo U-Utopia!
Lakini naombea hawa Maraisi wetu wa sasa wajaribu kujifunza makosa ya waliopita.Halafu wajifunze kujiridhisha na kupata faraja moyoni kwa kuturidhisha na kutupatia faraja moyoni.

AU SIO ; MUHESHIMIWA KIKWETE!:-)

Sasa tutafanyaje?

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP