Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hivi unauhakika na Tarehe ya Siku yako ya Kuzaliwa?

>> Tuesday, May 15, 2007

Ni kawaida kudhania kuwa kila mtu anajua tarehe ya kuzaliwa kwake.Lakini ukweli ni kwamba asilimia kubwa tu ya watu duniani hawajui siku yakuzaliwa kwao. Vijijini ambako bado watu wengi huzaliwa majumbani kwao kwa msaada wa mkunga, ni kawaida kusahau au kutojua umuhimu wakutunza kumbukumbu ya ni lini mtu kazaliwa.

Lakini KABLA SIJAENDELEA......

NICHOTAKA HASA KUSEMA NI KWAMBA MWAKA JANA TAREHE YA LEO NILIIFUNGUA BLOGU HII.INGAWA NI TAREHE 17/MAY NDIO NILIANZA KUPOSTI KWA WOTE DUNIANI WASHUHUDIE!

Lakini...........

Hivi tarehe ya kuzaliwa labda inaumuhimu. Kwa sababu za kimfumo wa dunia na hata kiafya wakati waganga wanajaribu kupata dozi yako ya PPF.


Sasaaaaaaaaaaaa.......!

Sherehe ya siku ya kuzaliwa unapoisherehekea unamaanisha nini?

Au unasherehekea kuwa umezaliwa?

Je , usingezaliwa kungekuwa na noma gani?


Lakini ukweli ni kwamba nimekutana na watu wengi tu ambao wamebunia tarehe ya kuzaliwa kwa sababu si za kufoji cheti, ila kutokana na ukweli hakuna ajuaye wamezaliwa tarehe gani.

Basi...
Kama hatujui kitu, angalau tarehe ya kuzaliwa tunaijua!
AU?

Duh!
Nisikuzingue!Endeleza tu eundelezacho!
Sasa ngoja nikuache na Yvyone Chaka Chaka

Siku njema!

9 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MTANZANIA. 5:51 am  

Simon!
Hivi kwa wale walozaliwa 29/2 huwa wanafanyaje pale unapokuwa ni mwaka mfupi? Hili suala huwa linanitatiza kiaina.

Hongera kwa kutimiza mwaka. Kupitia huu utandawizi ni rahisi sana kwa sasa kutunza kumbukumbu ikiwa ni pamoja na tarehe za kuzaliwa.

Lkn hata vijijini wana namna zao ktk kutunza kumbukumbuku. Baba yangu aliambiwa na babu kuwa alizaliwa mwaka ambao viwavi jeshi viliteketeza mimea yote hapo kijijini. (Ni kasheshe kweli)

Anonymous 6:21 am  

Heko umetimiza mwaka. Ulianza kwa makali na umeendeleza makali hayo hayo. Unatufaidisha wengi kwa chakula cha mawazo. Maswali yako hutufanya tufikirie na video zako hutuburudisha na kutufurahisha pia. Mbele kwa mbele!

Anonymous 1:33 pm  

Hongera...kanda wa mziki ili nasi tusherekee i wapi???
Serina.

mwandani 3:03 pm  

heko. Endeleza makali.

Egidio Ndabagoye 3:11 pm  

Hongera kwa kutimiza mwaka.Sijapata bahasha kuhusu ile nafasi unayogombea(natania).

Simon Kitururu 3:52 pm  

@Mtanzania:Ee Bwana , hiyo ya tarehe 29/2 hata mimi najiuliza sana.Lakini simjui hata mtu mmoja aliyezaliwa siku hiyo
@Wote: Asanteni!Nashukuru kwa kunipa nguvu kuendelea na haka kaugonjwa ka kublogi.
@Egdio: Ile bahasha ya hongo nimeshaituma:-) Halafu Nitapika pilau katika mkutano wakuombea kura:-)
@Serina: Nimerekebisha hapo juu.Kuna kalekawimbo kakusherehekea

Kibunango 1:01 pm  

Hongera sana Bw. Uliye Mawazoni... Nina hakika kama ningekuwepo huko Hlk Ningefurahia siku hiyo...!

Simon Kitururu 1:15 pm  

@Kibunango:Asante!Vipi London inasemaje?

Anonymous 6:11 am  

Free ebay finally


http://www.BuySellDirect.net free ebay like website is the Future of E-commerce and I think you can make money at home and it will not cost you any money at all. It is FREE


http://www.BuySellDirect.net 100% free service is all you need to make money every month.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP