Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUANDIKA UJINGA!KUONGEA UJINGA!KUFIKIRIA UJINGA!

>> Wednesday, May 30, 2007

Duh!Kumbe ni hawa werevu wanaotambua nani mjinga eeh?

Lakini si utani, ni kweli watu wengi wanaujuzi wa kumnyooshea kidole mjinga au wamdhaniaye kuwa mjinga.Na tatizo langu mimi ndio hilo hilo la kutoelewa jinsi gani watu wanapata uhakika sana kuwa wanaweza kutofautisha ujinga, mjinga na werevu, mwerevu!

Duh!
Usitishikeeee! Wewe na mimi si ni werevu!
AU?????????????


Lakini...........................!

  • Si werevu hawahawa walikuwa wanaamini kuwa dunia ikotambarare kama meza, miaka si mingi iliyopita wakibarikiwa na mpaka kanisa katoliki?
  • Si werevu hawahawa wanaamini kuwa binadamu walitaka kujenga mnara wa babeli kwenda mbinguni, hivyo Mwenyezi akakorofisha lugha iliwasije kufika mbinguni ndio kiyao na kipare kikatokea?
  • Si ndio werevu hawahawa waliotengeneza mabomu ya hatari ya nyukilia kwa malengo ya kulinda amani duniani?
  • Si ndio werevu hawahawa wanaacha watoto yatima mtaani kwa sababu bajeti ni ya kujaribu kufundisha nyani na chimpazii kusoma na kuelewa lugha za wanadamu?
  • Si waerevu wa jamii pia ndio walio kuwa wanashauri wanawake wakatwe kinanihii ?
  • Si ndio hawa wanao.......................ili ku..............................
  • Na kadhalika kadhaa wa kadhaa, si ndio hawa hawa wanafanya.......?
Duh!
Samahani sikutoa mfano unaokugusa wewe!


Lakini......................
Kweli inawezekana wewe na mimi ni werevu leo. Ila kesho kamjamaa kanaweza kakastukia kitu, halafu ukashindwa kuelewa jinsi gani unachekesha kwa gia ya uwerevu tulio uzoea.

Hivi...........
  • Walioamini kuwa mtu anaweza kujenga mnara kwenda mbinguni, hivi leo wakisikia kuna wanasayansi waruka na maspesi shato yao mpaka chobisi, wana darubini zinaona mpaka sehemusehemu bila kupastukia kwa Mwenyezi, watasemaje?
  • Wale waerevu walio kufa wakiamini dunia iko kama meza watasemaje?
  • Wale ambao waliamini ubongo uko moyoni je?
  • Na wale......................................
Duh!
Umestukia naandika ujinga eeh?

Swali:
Hivi ujinga ni nini?
Una uhakika?

Duh!
Basi wewe unabahati!
Siku njema!
Ngojea nikuachie na Frankie Lymon







Duh!
Basi Bwana, nimekuelewa kuwa nimekupeleka miaka ya mbali nakurudisha kwa Ludacris

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 9:49 am  

Si ni wewe na uwerevu wako, umewapa werevu hao kipawa cha kupanga hiyo budget? kwa kuwapigia kura au kwa kupuusa siasa?

Simon Kitururu 12:23 pm  

@Serina:Kweli kabisa!Halafu eti baadaye na werevu wangu naanza kuwalalamikia hao tena :-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP