Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Sidilia kwa Mtoto

>> Friday, May 04, 2007

Kuna ukweli kuwa kabla ya umri fulani sidilia haina kazi kwa mtoto!
Sababu kubwa ni kwamba hajaota matiti.


Inasemekana wakati wa utumwa Marekani , weupe walikuwa wanadai kujua kusoma na maswala ya elimu hayamfai mtu mweusi(Mtumwa).Moja ya sababu waliyokuwa wakiitumia ni kwamba ana ubongo usio mudu maswala ya shule.

Katika dunia ya sasa ambayo mtu mweusi anaweza kwenda shule au kubahatika kwenda shule, pia bado watu wengi wanadai ukitaka kumficha kitu mtu mweusi , andika hicho kitu kwenye kitabu.
Duh!
Inasemekana hata ukiandika mtandaoni , mtu mweusi yeye hasomi!
Kwa sababu inaaminika hana tabia ya kusoma. Matokeo yake hata ukimpa sidilia ya taaluma iwezayo kumsaidia ,kwake yeye ni yanini?Kwasababu hata matiti ya kuvalisha sidilia ya kujisomea hayajaota.

Unajua hilo si kweli kwa sababu mimi na wewe tunajisomea sana!
Unajua tena!Tukimaliza kupitia zile picha na video za ngono ,husoma zile habari fulani fulani nyingine za nanihiii!
AU?


Sasa.....!

Unajua kuwa asilimia kubwa ya Waafrika hawana nafasi ya kujisomea wala vitabu hivyo ambavyo wangejisomea labda.Hili linaeleweka! Ila wale ambao tunabahatika kujisomea tunasoma nini?Si siri, utakacho kukijua na cha muhimu kwako labda si cha muhimu kwangu.Lakini kama kinakusaidia, nakupa tano.Freshi hiyo!
Ndio , nakukubalia kuwa mtu huwezi kujua yote wala kujisomea yote!Lakini?

Ee bwana eeh!

  • Inadaiwa kuwa hata sidilia ya tekinolojia mpya tukiletewa leo , hatuna matiti ya kuvisha.
  • Tunaambiwa hata wasomi wetu wakiafrika wakiamua kurudi Afrika leo wote, hawana nyenzo za kutumia vipaji vyao. Wataota tu ukurutu katika ujuzi wao kutokana na kuwa na sidilia saizi mbovu.

Sasa.......!

Mimi naamini kuwa mambo mengi haya tuyasikiayo si ukweli mtupu! Ingawa sikatai kuna ka ukweli kinamana!
Lakini, mbona wenzetu wamefanikiwa kutatua mambo mengi tu kivyao bila utegemezi ?

Tukirudi kwenye sidilia,..............!
Swali:
Ushawahi kuona mtoto mdogo analilia sidilia akipewa inakuwaje?

Haya turekebishe basi hizo sidilia!Au ni ukweli matiti hayajaota?
Ijumaa njema!
Nakuacha na Procol Harum



0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP