Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika MAJARIBIO ya kufananisha utamu wa MALAYA(Samahani utamu wa CHANGU DOA) na ule UTAMU wa MKE!

>> Wednesday, July 11, 2012

Yasemekana ,...
... kuonja kwa kuibia ,...
... ni tamu zaidi kisa KISAIKOLOJIA tayari uendacho kuonja ushakinogesha TAYARI!:-(

Swali:

  • Kwani unafikiri MWIZI atanogewa KUJIIBIA?
  • Na si MME si sio MPENZI faraja KIMALAYA kama tu ilivyo kuwa MKE si MALAYA na kivyovyote labda tamu zao hazifanani?


Ndio,..
... UTAMU unamaandalizi,...
... na kama weye UNAJUA  ushaandaliwa KIPENYO au hata MWIBA,..
... basi LABDA maumivu yake KIUTAMU yashapunguzwa utamu hayo...
.. kwa kuwa TAMU nyingine ili ziwe tamu sana ,...
.....tamu nyingine zahitaji ya ''GHAFLA!´´:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Nakutakia tamu sana  KIUPENDAVYO siku ya leo AISEE!
Hebu Tshala Muana arudishe mtu - Karibu YanguAu tu Otis Redding ajaribu kuzima  kwa - (Sittin' On) The Dock Of The BayIla tu hebu Arrow azime kwa- Tiny WinyMmmmh!:-(Au tu PRECIOUS amalizie kwa kutoa siri za-Weakness for Sweetness

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 8:26 am  

Duh! nanukuu "Katika MAJARIBIO ya kufananisha utamu wa MALAYA(Samahani utamu wa CHANGU DOA) na ule UTAMU wa MKE!" mwisho wa nukuu...majaribu..utamu..

Simon Kitururu 8:27 am  

MMMMmmmh!

Yasinta Ngonyani 8:32 am  

katika picha hapo unaonekana upo katika bonge la mawazo..nimezipenda picha:-)

ray njau 3:27 pm  

Methali 5:1-23

1 Mwanangu, sikiliza hekima yangu. Tega sikio usikie utambuzi wangu, 2 ili ulinde uwezo wako wa kufikiri; na midomo yako mwenyewe ilinde ujuzi.

3 Kwa maana midomo ya mwanamke mgeni hudondoka-dondoka kama sega la asali, nalo kaakaa lake ni laini kuliko mafuta. 4 Lakini matokeo yake ni machungu kama pakanga; ni makali kama upanga wenye makali kuwili. 5 Miguu yake inashuka kwenye kifo. Hatua zake hushika Kaburi. 6 Yeye hatafakari njia za uzima. Mapito yake yamepotoka wala hajui yanakoelekea. 7 Basi sasa, enyi wana, nisikilizeni wala msiache maneno ya kinywa changu. 8 Itenge njia yako mbali naye, wala usiukaribie mlango wa nyumba yake, 9 ili usije ukawapa wengine heshima yako, wala kukipa kilicho kikatili miaka yako; 10 ili wageni wasijishibishe kwa nguvu zako, wala vitu vyako ulivyovipata kwa maumivu visiwe ndani ya nyumba ya mgeni, 11 wala usije kulalamikia wakati wako ujao, nyama yako na mwili wako vitakapofikia mwisho. 12 Nawe utalazimika kusema: “Nimechukia nidhamu kama nini nao moyo wangu umedharau karipio kama nini! 13 Nami sikusikiliza sauti ya wafundishaji wangu, wala sikuwategea sikio langu walimu wangu. 14 Nimeingia kwa urahisi katika kila namna ya ubaya katikati ya kutaniko na kusanyiko.”

15 Unywe maji ya birika lako mwenyewe, na maji yanayotiririka kutoka katikati ya kisima chako mwenyewe. 16 Je, chemchemi zako mwenyewe zitawanyike nje, na vijito vyako vya maji katika viwanja vya watu wote? 17 Na yawe yako peke yako, wala si ya wageni pamoja nawe. 18 Chemchemi yako ya maji na ibarikiwe, na ushangilie pamoja na mke wa ujana wako, 19 paa mwenye kupendeka na mbuzi wa milimani mwenye kuvutia. Na maziwa yake yakuleweshe nyakati zote. Upendo wake na ukufurahishe sikuzote. 20 Basi mwanangu, kwa nini umfurahie mwanamke mgeni au kukumbatia kifua cha mwanamke wa kigeni? 21 Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele za macho ya Yehova, naye anayatafakari mapito yake yote. 22 Makosa yake mwenyewe yatamkamata mwovu, naye atashikwa katika kamba za dhambi yake mwenyewe. 23 Atakufa yeye mwenyewe kwa sababu hakuna nidhamu, na kwa sababu ya upumbavu wake mwingi yeye hupotea.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP