Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Eti kisa ni kwamba KACHUMBARI huwa haisifiwi kuwa ni CHAKULA!

>> Tuesday, January 24, 2012

KACHUMBARI ni CHAKULA,...
.... ingawa bado kuna wadaio  kama KILIWACHO  sio UGALI kwa kuwa ni WALI basi kiliwacho sio CHAKULA na alaye anapasha tu moto kabla hakijaletwa cha kikweli CHAKULA..


LAKINI  ukikaa mkao wa kuchukulia KACHUMBARI kama CHAKULA,...
.... kachumbari hushibisha  tu pekee hata bila chipsi dume au chipsi mayayi ambayo  kwa wengine ni kifungua kinywa tu  au  kionjo tu cha barabarani kabla hujaenda nyumbani  kwenye FULU KUBUGIA NANIHII kwa watazamavyo baadhi CHAKULA.

Swali:
  • Si umestukia SHUKA ni nguo yakutosha  hata bila chupi kama ukiliangalia kimtazamo wa KILUBEGA Kimasai?
  • Kwani kwako chenye sifa fulanifulani hakiathiri ukipavyo sifa FULANIFULANI? 
  • Unafikiri KACHUMBARI PEKEE haishibishi?

 Ndio LABDA,...
....ukigeuza mtazamo  ,....
.....KACHUMBARI ni chakula tosha TU hata kama hiyo sio SIFA YAKE ,....
.... na hata kama kachumbari yenyewe tuongeleayo hapa NI baiskeli  katika ya wafikiriao usafiri lazima iwe ni wa GARI na yabaiskeli hayaitwi SAFARI!


Ni wazo tu hili kinanihii MHESHIMIWA!
Jumanne NJEMA sana MKUU!


Hebu UB 40 waingilie kati kwa - Please Don't Make Me CryUB40 waongezee dozi kwa -The Way You Do The Things You DoHalafu hawahawa UB 40 wazime kwa -Here I am Baby

Juzijuzi niliwadaka UB40 wakiwa live kama katika baadhi ya picha za juzijuzi zifuatazo...
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mzee wa Changamoto 2:11 am  

Duh!!!
Mzee unaWAZA KWA SAUTI kuu.
Labda waliotukaririsha karirisho la tafsiri ndio wanaoamini kuwa Kachumbari haiwezi kuwa chakula na / ama mboga japo YALIWA na pia YALISHA kiliwacho.
Na hao hao hawakubali kuwa shuka ni nguo japo wanajua ndilo lubega ambayo YAFUNIKA KWA ADABU NA HESHIMA NA KWA MAREFU zaidi ya "kimini".

Labda.......

Duh!!

chib 9:44 am  

ha ha haaa, bado natafakari hiyo kachumbari.
Tisa... kumi ni picha zilizonakshi mada ya kachumbari!

Mcharia 11:22 pm  

Yessssssssssss...

Mcharia 11:23 pm  

Yessssssssssss...

Yasinta Ngonyani 1:00 am  

Duh!! hiyo picha hiyo huku na huku...haaaaaayaaaaa

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

There was an error in this gadget

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP