Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama WANAUME ndio wangekuwa wanapata MIMBA,...

>> Thursday, January 19, 2012

...LABDA  hiyo kitu ingegeuka kuwa KAWAIDA!:-(Samahani nariwaindi na kuanza upya hii TARALILA.


Imetokea mara kadhaa katika michakariko hoja ikajitokeza kuwa kutokana na mfumo dume DUNIANI  wanaume  hujisahau kustukia kazi na majukumu makubwa yabebwayo na WAMAMA ikiwa ni pamoja na MIMBA kwa miezi kadhaa wa kadhaa.


Pamoja na upana wa MADA kama hii ningependa kuchokonoa kipele kidogo tu ambacho labda huchangia ni kwanini hata MWENYE NYUMBA huweza kusahau hata ya HAUSIGELI mwenye umri wa kwenda shule asipoenda shule kwa kuwa anamfanyiakazi mwenyenyumba ,...
.. na hicho ni kipele kiitwacho ``KAWAIDA´´

Na tatizo la KAWAIDA,...
.... ni kugeuza CHOCHOTE KILE kuwa ``KAWAIDA´´,....
.... kitu kifanyacho hata kunyanyasa MKE au hata kutothamini ya MKE huweza kugeuka ``KAWAIDA´´.

Swali:
  • Si unajua kuwa ukizoea kuishi pembeni ya JALALA linukalo hicho kitu hugeuka KAWAIDA kitu kifanyacho hata harufu mbaya USISIKIE kwa kuwa ishakuwa ``KAWAIDA´´?


Ndio,....
.....hata kwa baadhi ya BUIBUI  ,...
...kidume kuliwa na BUIBUI JIKE kama bonge la msosi baada  ya tendo la NDOA nalo KIBUIBUI hao  ni KAWAIDA.:-(


Tatizo/ANGALIZO ni:
  • Hufikiri moja ya TATIZO kubwa lifanyalo HATUTATUI MATATIZO YETU yawe ya NCHI zetu au hata yetu BINAFSI ni kwa kuwa yameshageuka KAWAIDA?

Ndio,...
... ``KAWAIDA´´ ikizidi,...
.... yaweza geuza usistukie kuwa USICHOSTUKIA ni kwa kuwa tu kimeshageuka ``KAWAIDA´´!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu tubadili kwa kumuangalia MIKE KALOMBO akitengeneza muziki katika- Party Everyday
Au tu hebu tubadili na kurudi miaka ya nyuma zaidi katika maswala ya Les Mangelepa katika kibao - MimbaHalafu Don Campbell abadili mchezo na kuzima kwa - Storm Is Over Now


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP