Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

HELMETI ya MOYO uliopenda HATA ingekuwa ni ya CHUMA,....

>> Thursday, January 19, 2012

....LABDA bado  moyo wa APENDAYE ungeuma ,...
..... hasa kwa kuwa MOYO wa APENDAO chuma sio ngao ya kuzuia mishale ichomayo MOYO!HELMETI ilindayo  MOYO uliopenda HATA ingekuwa ni ya DHAHABU kama sio ALMASI,...
.....bado  YA moyo THAMANI yake kipimo kizuri hakipatikani kitu kifanyacho ya MOYO kuwa na thamani kubwa kuliko chochote cha BINADAMU hapa DUNIANI halafu kwa maajabu ya MUSA  YA MOYONI MWA MTU ndio yenye  ULINZI MDOGO zaidi kuliko yote kwa kuwa ASKARI alindaye moyo ULIOPENDA ,...
... kupenda humfanya KIPOFU!.:-(

Swali nanihino kiaina:
  • Unafikiri ULINZI wa moyo wako ili  USIUMIZWE NA PENZI unauimara gani wakati labda hata kupenda kwako KWENYEWE  sio CHAGUO lako KIMAAMUZI kitu ambacho naweza kuamini UKISEMA chanzo chake PENZI LAKO chaweza kuwa ni kitu kidogo tu KILICHOWASHA BARUTI kama vile kile cha  KUCHEKEWA TU kidogo na KIJEBA MUUZA MITUMBA au tu hata kutingishiwa tako na KIGOLI- na wala sio TABIA ya MPENZI wala NINI?

Ndio,...
.....HELMET ni KOFIA,...
... na labda hata HELMET ya mwendesha PIKIPIKI hailindi kichwa kizima!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu MAD ICE aanzishe upya kwa- Te AmoJamhuri Jazz Band waingilie tena kati kwa-Shingo la UpangaHalafu Ndedi Dibango azime tena kwa -Eyo Mè

Tuko Pamoja WADAU!

... nipo na baadhi ya picha kutoka kaskazini ya dunia  ambako nako nilipita mitaa ya hivi karibu ni hizi:
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 5:53 pm  

Ahsante kwa picha ....naoana likizo/kupotea kwako kulikuwa safi.

Yasinta Ngonyani 6:00 pm  

Kama kweli kuna mtu unampenda na ukiusikiliza huo wimbo wa kwanza unatamani kuliaaaaaaaaaa unachoma mno moyo na hiyo ya Hamlet basi naacha...

SIMON KITURURU 6:19 pm  

@Yasinta: Sijui kwanini nahisi unamjua nimpendaye!:-(

Yasinta Ngonyani 8:27 pm  

Hapana Simon, Sijui nimesema hivyo kwa vile najua ni vipi kumkosa umpendaye

SIMON KITURURU 8:45 pm  

Yasinta unamjua amini usiamini na labda nni yule karibu na moyo wako!:-(

Yasinta Ngonyani 8:53 pm  

karibu na moyo wangu? mmhhh

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

There was an error in this gadget

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP