Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ya KESHO kama si MASWALA ya KESHO!

>> Tuesday, January 17, 2012

Ya kesho ,...
.....LABDA karibu kwa asilimia mia huanza kabla ya KESHO,...
.... hata kwa wafikiriao YA KESHO yako KESHO ,....
.... kama ya LEO yakumbwavyo na WATU leo.

Swali:
  • Unafikiri yako yatakayokukumba KESHO mwanzo wake hauko kabla ya KESHO?

Ndio,...
.... hata MIMBA za kesho hata za KIMAWAZO ,...
......labda  mbegu  za KIBABA WATOTO na mayai yake MAMAWATOTO wa SWALA yalishaumbwa kabla ya KESHO katika utekelezaji utakao ipasifa KESHO kwa watakao kuamini LILILOTEKELEZWA kesho lilianzia KESHO!

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na wala USIKONDE!


Hebu tena tuanzie Sierra Leone ili King Masco 
aanzishe kubadili kidogo kwa zilipendwa -Mao Mao
Tuhamie Nigeria ili King Sunny Ade aendeleze kwa zilipendwa - Ja Funmi
Halafu hapahapa Nigeria yule Fatai Rolling Dollar arudie na kuzima kwa zilipendwa-Easy Motion Tourist


5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:46 pm  

Kesho! mmmhh!!

sam mbogo 6:21 pm  

Kunausemi huu rahisi sana,Leo nileo msema kesho muongo. kila kitu kina mwanzo, hata unaposema tuonane kesho ni mwendelezo wa leo. kwani hakuna aijuwae kesho,kesho ni ndoto pana sana,umenikumbusha katika mjoa za hotuba za Nyerere( kwa wale wasiyo mfagilia huyu mzee samahanini) aliwauliza watu pale katika kiwanda cha nguo cha urafiki,kuhusu kesho,alisema nani anaijuwa kesho,kilakitu mnasema kesho wewe unijuwa kwsho. navita ingekuwa inapiganwa kwa ndharia ya kesho ingekuwa safisana. karibu tena mtakatifu.kaka s.

Said Michael 6:58 pm  

Ni kweli! Ya kesho huanza ka bla ya kesho

Mcharia 6:54 am  

Katika Biblia imeandikwa USISUMBUKIE YA KESHO ULE NINI UVAE NINI. Sumbukia ya siku hiyo hiyo sio kesho maana aliyekuumba anafahamu kesho itakuwaje kwako.

SIMON KITURURU 4:51 pm  

@Yasinta: Mmmmh!

@Kaka Sam Mbogo, Mkuu SAID Michael na Mkuu Mcharia: Ndio haaaapooooo!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP