Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ZAWADI ni TAFSIRI- na tafsiri nzuri inamchezo wa kugeuza mavi kuitwa MBOLEA!

>> Wednesday, January 18, 2012

Na kwa TAFSIRI,...
... waweza kuchukia MTU,...
.... kwa kuwa tu UMETAFSIRI kifanyacho asipendeke MTU.

Na kwa tafsiri,....
...... MTU aweza kuua MTU,....
.......kwa kuwa KITAFSIRI kifanywacho ni kupiga MWIZI au tu kuua MWIZI ,...
... kitu ambacho kwa tafsiri za wengi wapiga MWIZI swala hilo  sio LA  kuua MTU.

Na kwa TAFSIRI,....
...... Watanzania waweza MPAKA kukuapia NYERERE hakuwa DIKTETA kwa kuwa WAMETAFSIRI,...
.... na kitafsiri jamaa alikuwa MTAKATIFU ki wake UTU.

Swali:
  • Na siunakumbuka ZAWADI ni uitafsirivyo kitu kifanyacho kuna asiye na CHUPI ambaye akipewachupi atatafsiri kadharauliwa  kwa kuhisiwa hana chupi hata kama aliyenunua chupi kama Zawadi hakujua Mdada kutokana na uhaba wa chupi kavaa kaptula ya KAKA?
  • Na si unakumbuka UKITAFSIRI waweza kustukia MAFISADI nni jina tu lenye maana ileile ya MWIZI kitu kifanyacho kuwa labda NCHI na DUNIA inaongozwa na WEZI hata kama kimajina wapeanayo hutambulika kama WAHESHIMIWA?TAFSIRIIIIIIII!

Na kwa kutafsiri ndio maana LABDA hakuna DINI moja DUNIANI,...
....kama tu ilivyokuwa hakuna ZAWADI ya aina MOJA kitu kifanyacho MAUA ni ZAWADI kwa MWINGINE jinsi ileile ilivyo ZAWADI kwa KIJEBA mwingine achukuliavyo ZAWADI ni ile kitu KIFUKO cha DHAMBARAU  TU ambacho kwa kutojiamini kimegeuka ZAWADI kisa mtoaji ni MDADA ambaye haamini ni LEVO zake aka Katika KIJIJI cha UJAMAA huyo ni Katibu KATA na kwa mkulima wa kawaida kugawiwa vyake ni ZAWADI tu kwa kuwa mgawiwa HASTAHILI kikawaida !:-(Ndio,....
..... tafsiri ndio MSINGI na NGUZO mpaka  ya yote yadhaniwayo kuwa ni MATUSI,...
...... na ukitafsiri vizuri ,...
...LABDA chochote ni ZAWADI hata kama kinamdudu,...
...kama tu ilivyokuwa labda kuna maneno tu ambayo UKITAFSIRI yanaweza kuitwa SALA!:-(


Ni wazo tu hili MKUU!

Hebu ghafla Eduardo Paim aturudishe tena Angola kwa - XinguilaHalafu tupitie Japan kidogo ili Marehemu NUJABE apoze kwa kurudia ndude  -Counting Stars
Halafu Jaziel Brothers wazime kwa sindimba ile - Woza


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 5:59 pm  

Niliposoma kichwa cha habari nikaanza kujisemea ...na baada ya kusoma nikawa najisikia aliyetonesha kidonda kama kweli ametonesha..mmmhh naachia hapa. Au ngoja naweza kweli nikatafsiri visivyo hapa:-)

SIMON KITURURU 8:29 pm  

@Yasinta: Tafsiri ni tafsiri tu mtu wangu na hakuna ulichotafsiri visivyo kimachale yangu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP