Jestina George is a fashionista, blogger, Presenter and a model based in London, from Tanzania the land of Kilimanjaro.
AILTV caught up with her at the the launch of READY TO WARE by Anna Luks. Jestina is speaking.... is expressing her concerns about African fashion and designs.
...... kwa kuwa yasemekana kila kitu hapa DUNIANI huchukuwa MUDA,...
.... na inategemea tu na uharaka wa KIPIMO cha MTU kuhusiana na KITU uwezeshao kugeuza SEKUNDE igeuke MWAKA.
Swali:
Si ghafla tu KIJANA anaweza kujikuta MZEE na anahangaika UZEENI kisa hakustukia UGHAFLA wa UZEE ukaribiavyo- kitu kilicho chelewesha KUJIANDAA?
Ndio,... ....labda inategemea tu na jinsi ulipavyo SWALA umakini,...
.... na kama humakini,...
.... kila kitu chaweza kuwa MITOKO YAKE ni ya kighafla tu,...
.... na hapa wala siongelei MTOKO kishahawa , kibaruti orgazimu ,ughafla wa KUHARIBU URAFIKI, Ughafla wa KUJIMIMINIA dhambi,ughafla wa kuingia ofisini na KUJIFUNZA UFISADI , ufuska kiduchu wa GHAFLA mtu akihisi haonwi......
... au tu HATA jinsi gani ghafla UTAKAVYOSAHAU hii topiki,...
..... baada ya KUNISOMA!:-(
Swali:
Kwani si umeshawahi kubanwa hata na HAJA ghafla halafu baada ya kujisitiri ghafla UKASAHAU ulivyobanwa kabla ya FARAGHA?
Ndio,...
.....labda kitu ``GHAFLA´´,...
...... hutegemea tu na spidi yako katika SWALA.:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Nakutakia SIKU NJEMA!
Hebu Billy Ocean aingilie kati,...
... na kuongelea jinsi PENZI lilivyo leta maana GHAFLA katika kitu-SUDDENLY
.... lakini labda KUZIDISHA ni lakshari za WENYENAVYO tu!
Swali:
AU?
Kwani UNAWEZA kuzidisha kama hakuna vya KUZIDISHA?
Ila labda PIA ,...
.... ``KIDOGO´´ na ``SANA´´´ni vipimo tu binafsi MTU ajifunzavyo KIBINAFSI,...
.... kitu kifanyacho kwangu kilicho KAWAIDA kwako kinaweza kikawa tayari ni kupitiliza na kwahiyo tayari ni UMALAYA ki -SANA TU kiulafi!
Swali:
Lakini si unakumbuka kuwa LABDA wingi wa kitu kama tu UCHACHE WAKE kitu hutegemea SANA kipimo cha kitu kingine ambacho MPIMAJI analinganisha nacho hata bila KUJUA- kitu kifanyacho KILO moja ya SUKARI ni ``SANA´´ kama inalinganishwa na KIKOMBE wakati labda ni ``KIDOGO´´ kama kipimo ni PIPA`?
Ndio,...
.... na kidogo tu KIUJAZO wa NANILII,....
.... inaweza kuwa inatosha kama lengo ni kufanya mtu apate HATA mimba KIIMANI!:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Nakutakia SIKU NJEMA MKUU !
Hebu Burning Spear aingilie kati kwa-AFRICAN TEACHER
.... sio tu wenye UKIMWI ndio wanaodili na MNYANYAPAO!:-(
Swali:
Si si lazima aliyekaa vibaya KWA BAHATI MBAYA ikastukiwa UREMBO wa chupi yake ni UZEE au UCHAFU -ndio tu maswala ya chupi yake- ndio TU yaanzishe mjadala wa kumfanya ajisikie KATENGWA?
Lakini UMESTUKIA jamii ya WASTAARABU ile ya WATANZANIA ambayo hudai hata matusi haitaki kustukia - bado inaongoza kwa kutenga WAATHIRIKA - na hapa wala sigusii MAALIBINO?
Ndio,...
... labda kuna MTU una MNYANYAPAA bila hata kujua,...
... kisa tu ,...
... UNAMTENGA kwa sababu zako tu hata zile ZA kuwa hata KIPOMBE yeye sio MLOKOLE INAFU- na kiukarimu hata wa UJI yeye kwa kugawagawa kisa ni mkarimu ,... ... basi huo ni UMALAYA!:-(
Swali: AU?
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Ndio naenda leo kuwadeku Ladysmith Black Mambazo ....
....hebu waanzishe - Hello My Baby
Au wajaribu kuzima kwa -Homeless
Au tu na Paul Simon wazime kwa -Diamonds On The Soles Of Her Shoes
Au tu hebu tubadili KIDOGO katika majaribio ya KULAINISHA kwa kumsikiliza Asathecomic katika -Will Smith SLAPS Reporter for Kiss!
.... na kisa kuna MPAKA wafikiriao SURA ikikunjwa MSALANI basi hiyo siyo nzuri,....
.... ni LABDA kweli kabisa ni MITAZAMO tu ya WATU ,...
... kama tu isemekanavyo,....
....UZURI wa KIDUDE u-JICHONI tu mwa ATAZAMAYE kidude.:-(
Swali:
AU?
Ndio,...
... labda ukipenda ,....
... weye ushapenda na PENGO hugeuka MWANYA kama tu MATEGE yageukavyo BOMBA tu kivilevile isamehewavyo wanukao maeneo kisa MTU kapenda!:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu ghafla tugewe YA UREMBO kwa VIGOLI- samahani- UREMBO kwa WADADA kutoka kwa MDADA KOKOFEMME akiongelea SHUGHULI ambazo kwetu wengine zimekaa kichina...
... katika ya-BEAUTIFUL FACE!
Au tu Remmy Ongala arudishe zote zisizo na SURA MBAYA...
Unauhakika katika MAADILI kuna mwenye MKE au MME mmoja .... bila kusahau KIPENZI hata kama ni KIKITU tu?:-(
Yasemekana siri ya USAHIHI wa kitu ni MAADILI,....
.... tena ambayo MTU mpaka JAMII hujifunza tu KIMAPOKEO.
Swali:
Lakini si ikumbukwe pia USAHIHI wa MAADILI nayo ni kitu-na sio tu USAHIHI wa KITU ndio MAADILI?
Si ndio maana kwa MAADILI kwa Rais OBAMA katika kitu kama USENGE kwake ni SAHIHI hata kama kwa MWINGINE amzimiaye RAIS OBAMA kwa MAADILI MENGINE - hayo ya OBAMA kutopinga UTOAJI MIMBA sio MAADILI?
Na kikubwa katika MENGI yaonekanayo ni SAHIHI au sio SAHIHI,...
...... labda tukumbuke NI za watu TU za kitu TAFSIRI.:-(
Swali:
Si inawezekana LAKINNI ni KWELI usahihi wa MAADILI ya WATU ni TAFSIRI tu za MTU?
Na ndio,....
.... labda kitu SAHIHI bado ni SAHIHI tu hata kama kimaadili yako,....
......weye hicho kwako ni DHAMBI na UTOVU wa NIDHAMU hata kwa MUME kumfanyia mnyonyo wa kisicho adili kivyako MKE WAKE wa ndoa CHUMBANI kimaadiliyo binafsi ambayo kwao ni SWAFI KABISA.:-(
Swali:
AU?
Ndio,.... .... na usishangae,.... .... katika JAMII hii yetu ya sikuhizi ya KINAFIKI,....
.... labda yaliyo SAHIHI ndiyo yaonewayo AIBU kisa kimaadili ya JAMII hayo yamekaa UCHI na kwa hiyo ndiyo YAAIBU na kwa waungwana inabidi yafungiwe macho na MASIKIO,...
... au ikibidi MSTAARABU ajifanye hatambui kuwa YAPO katika JAMII yake kama sio mpaka kwenye FAMILIA YAKE!:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Halafu hebu GAHAFLA turudi Africa KUSINI ili Abdullah Ibrahim aka Dollar Brand...
.... aingilie kati na kubadili mchezo kwa - Soweto - Sathima (part)
Dollar Brand aongezee-Mannenberg
Abdullah Ibrahim na Ekaya waongezee dozi kwa - The Mountain / Nisa / Mississippi
Huyu huyu Abdullah Ibrahim aongezee - Cape Town Flower
Ila tu tena hapa hapa KUSINI ya AFRIKA hebu Ringo Madlingozi azime kwa -Into Yami
... KUJERUHIWA kwa majeruhi PANZI -kwa mdomo wa KUKU,...
.... LABDA sio mpaka KUKU achubue mpaka chini ya manyoyanyoya ya PANZI ili nako kuwe na MADOADOA yaringiayo wenye macho na wafikiriao ni wajanja KISA NI KWA kuona kwao,...
..... ili tu IWE KUNA ushahidi PANZI asiye na MANYOYA,.....
... chini ya MANYOYA kachubuka ,...
.... ili tu KIUSHAHIDI iwe wazi kwa kuwa INAONEKANA kwa macho kuwa PANZI ni MJERUHIWA basi KAJERUHIWA!:-(
Swali:
Unafikiri sio kweli kuwa kwa ABAKWAYE kikweli -sio mpaka KIKWELI kuwe na waitwao wataalamu huhitajika hata katika hilo ili tutofautishe aliyebakwa na aliyekubali mwenyewe mtalimbo hivyo hajachubuka hata kama kuna KUKU wenye nyuchi PANA ambao kubakwa kwao na mwenye mtalimbo sindano huwa hakuna USHAHIDI hata KIBATA ambaye kimtalimbo yuko kistaili ya MNYOO?
SI ACHUBUKAYE hata kwa KUDHALILISHA KWANGU MTU - si ni SI lazima KIKUCHUBUKA kuwe na alama IONEKANAYO kwa mimacho au tu ki tutegemeavyo?
Na kwa kuwa ,...
.... YASEMEKANA majeruhi wengi MAJERUHI YAO huwa YANATAFUTWA KWA DARUBINI ya MACHO kisa watakao uthibitisho wana MACHO,...
.......labda ikumbukwe tu MICHUBUKO yao WENGI WENGINE huwa haihitaji DARUBINI ili aliyejeruhiwa AWE AMEJERUHIWA NA HATA KAULI YAKO YENYE HARUFU MBAYA ili TUTHIBITISHE kiuhaueni wa KUJERUHIWA kachubuliwa TU kimjeruho ,...
.... kwa hiyo KAJERUHIWA!:-(
Swali:
Si unakumbuka kuwa labda kwa kulamba STEMPU huwa umeijeruhi STEMPU kama kidarubini kabla hujagandisha stempu kwenye BAHASHA yenye BARUA YAKO nzuri kwa MPENZI -bado STEPU imekwaruzwa na liulimmi lako na kwa hiyo ni stempu nlabda tayari ni MAJERUHI?
Ndio,...
....na KUJERUHIWA kwako hata kwa KUNG'Ong'wa,...
... na kugeuke kuwa BARAKA kwako MKUU!
Ni hilo tu MHESHIMIWA! Na ni wazo tu hili MUKULU!
Hebu Eddy Grantarudishe ya-VILLAGE LIFE
Au tu Mkuu Eddy Grant azime tu tena kwa ya - Frontline
WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA SHULE YA MSINGI MAKUMBUSHO KAMA WANAVYOONEKANA DARASANI LEO HII
HAWA NI BAADHI YA WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA KATIKA SHULE YA MSINGI MAKUMBUSHO YA JIJINI DAR ES SALAAM WAKIWA DARASANI, SIJUI WAPO WANGAPI, WATOTO HAWA HULAZIMIKA KILA MWEZI KULIPA Tsh1000 YA MTIHANI WA MWEZI,Tsh 1500 YA MTIHANI WA TERM,Tsh500 YA KILA SIKU YA UJI HAPO BADO TIUSHENI,USAFI, MLINZI,LEBO,VIDUMU,FAGIO, NA MADAFTARI PIA HULAZIMISHWA KUNUNUA HAPOHAPO.
.....labda HARUFU ya ANUKAYE ni dalili za tatizo la ANUKAYE,...
......au tu na ni TATIZO sumbufu kwa wanukiwao na hiyo MIHARUFU,....
.... lakini ngoma iko palepale kuwa HARUFU sio tatizo kwa HARUFU.
Swali:
AU?
SI unakumbuka HARUFU yenyewe KIYENYEWE huwa haina PUA ya kunusia harufu -na ni MIJIVIUMBE tu mingine tu yenye mchezo wakunusanusa hata UVUNDO kisa inaMIPUA ndio imegeuza HARUFU kuwa DILI?
Na WEWE labda sio tatizo kwa WEWE,...
.... ingawa bado LAKO labda ni chanzo cha tatizo LAKO,....
...... na lako ni TATIZO sumbufu kwa wanukiwao wengine na hilo LITATIZO lako,...
....... ingawa ngoma bado iko palepale kuwa WEWE ni WEWE na WEWE sio TATIZO.
Swali:
AU?
Una uhakika WEWE na yako WEWE huwa UNAYATOFAUTISHA hasa ukizingatia labda WEWE na YAKO WEWE ni vitu viwili TOFAUTI?
Na si HARUFU inaweza kuwa ni ile ya KUNUKIA na sio tu ile ya KUNUKA?
Na kama unafikiri MIMI au MTU mwingine ndiye tatizo LAKO,...
....labda ngoma iko palepale kuwa UMEJIONGEZEA tu MWENYEWE yasiyo TATIZO LAKO,...
... na sasa WEYE MWENYEWE unaelekea kuwa TATIZO la wengine!:-(
Swali:
AU?
Kwani ni kweli HARUFU ni tatizo la HARUFU?
Ndio,...
..... labda siri igeuzayo HARUFU kuwa tatizo ni pua za WENGINE tu,...
.... kwa kuwa kama JALALA ni LAKO,....
..... harufu ya jalala lako lazoeleka,...
.... na hilo sio tatizo LAKO bali la WENGINE.
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA,..
...kutolinyaka KIMAANARUKSA!
Nakutakia SIKU KABAMBE MKUU!
Hebu tena Tony! Toni! Tone! waingilie kwa kuriwaindi - Whatever You Want
Au hebu tubaki na Raphael Saadiq katika -Good Man
Halafu Raphael Saadiq ajaribu kuzima kwa - It's a shame
Halafu D'angelo ndio azime kwa - She's always in my hair
..... labda mipaka yake ni tofauti na ya MTU huyohuyo KESHO.
Swali:
SI KIBINADAMU kuna mpaka hata KUZEEKA?
Ndio,...
... labda UNOGEWAVYO na kitu leo ,...
..... ni tofauti na utakavyo nogewa na kitu KESHO.
Swali:
SI unakumbuka hata GLASI ya PILI ya PEPSI inautamu tofauti na GLASI ya kwanza ya PEPSI kama tu utamu wa BIA ya kwanza utofautianavyo na wa BIA ya TATU?
Ndio,...
.... kweli yako hata ya MKE wa KWANZA mwaka huu,...
.... inaweza kuwa ni UONGO kama itakuaminisha kuwa TAMU ni tamu tu kivilevile,...
... kitu kifanyacho ufikirie utamu wa MKE wa nne utakuwa ni uleule kama wa LEO wa mke wa kwanza.
Swali:
AU?
Kwani kwa mama watoto , mme anogavyo leo ndivyo atanoga kesho?
Ndio,...
.... hata tukiacha mengine,....
...... labda kumbuka MAISHA na LADHA zake sio MGANDO,....
........ na uking'ang'ania kuamini hata wali uleule ni MTAMU vilevile kisa unafikiri kwa kuwa ni uleule basi uko VILEVILE,...
......KWELI yako labda imeanza KUKUDANGANYA.
Swali:
Si yasemekana hakuna hata kitu kimoja hapa DUNIANI kibakiacho vilevile (tukiruka MUNGU) na kila sekunde chochote kile ukikiweka kwenye bonge la darubini waweza kustukia MABADILIKO hata kama ni yale ya jicho lako au tu angalau jinsi UONAVYO?
Ndio,...
..... labda KWELI yako jana,....
.....LEO imeshaanza kuwa ``ONGO´´ ,...
.... na ukiibinua waweza stukia imeshaanza kukudanganya.
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu tuachane na hili na moja kwamoja tujiburudishe kwa ushambenga wa walionasiana....