Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UNAPOKOSA UHAKIKA KUHUSU MSIMAMO WAKO KWENYE....

>> Monday, July 30, 2007

Kabla sijasema, kuna haka kawimbo ka Eurythmics kanikumbushako ubinadamu . Hebu kasikilize maneno yake....


Sasaaaa......

Msimamo ni kitu cha ajabu sana kwa binadamu.
Inajulikana kabisa kuwa sifa mojawapo kuu ya binadamu ni kutokujua kila kitu.
Tofauti ya binadamu na malaika(kama unaamini kuna malaika)ni kwamba binadamu si malaika.
Binadamu ana sifa zote zimfanyazo asijue na kuwa na uhakika na kesho.
Kwa hiyo ungeweza kuamini kwanini ni kawaida kabisa kwa binadamu kukosa msimamo.
Swali:
Unafikiri utakuwa hai kesho?

Duh!
Cha ajabu binadamu hujihisi mapungufu pale astukiapo hajui kila kitu lakini anahitajika ..

  • Kufanya uamuzi na.....
  • Kufanya kitendo na...
  • Kusema jambo na...
  • Kukaripia jambo na....
  • Kumpiga mtu na....
  • Kula nyama ya nguruwe na...
  • Kutafuta malaya na...
  • Kuokoka na.....
  • Kuslimu na...
  • Ku...........
  • Nk.
Maswali:
  • Unauhakika umuitaye baba ni baba yako?
  • Mtu na ubinadamu wake, anahitaji kweli kujisikia vibaya akistukia kuwa hana uhakika?
  • Unauhakika na unachotaka kufanya baada ya kunisoma?
Duh!
Kuna watu hawana uhakika hata kwenye kitu ambacho hakina sababu kwao kukosa uhakika.Unaweza kumuuliza mara kadhaa mtu baada ya kula na kuweka sahani pembeni kama ameshiba, akaanza kukosa uhakika kuwa ameshiba.

Nahisi wengine hawana uhakika ili wenye uhakika wawahakikishie uhakika. Wengine wana uhakika kwa sababu wengine hawana uhakika. Wasio na uhakika mara nyingi huwa na imani na waonyeshao uhakika hata kama wenye uhakika hawana ujuzi wala cha zaidi kiwasababishiacho kuwa na uhakika.

Swali:
Unafikiri Nyerere alikuwa na Uhakika na ......,siasa ya ujamaa...., na...?
Je ni sahihi kwa binadamu kukosa uhakika na msimamo kwa kisingizio chakutokuwa na uhakika na msimamo?

Duh!
Basi bwana!
Jumatatu njema!
Nakuacha na Vybz Kartel


Read more...

TUBADILI JINA LA CCM?

Swali:
Chama gani cha siasa, matendo yake yanafanana na jina lake?

CCM=Chama Cha Mapinduzi.
Unafikiri ni chama cha mapinduzi?Mapinduzi gani hayo?

CUF=Civic United Front.
Hapa kuna Civic United front? Hivi kwanini kinaunganisha waongeao kiswahili kwa jina la Kiingereza?
CHADEMA=............................................
Hivi...........................................?

Usitishike!
Niko mawazoni tu!

Read more...

NI NINI SAHIHI KUONGELEA?

>> Sunday, July 29, 2007

Kabla sijasema......
Hebu cheki jamaa wakikufuru kutokana namtazamo fulani.......


Tuna mila na desturi zitufundishazo, ziwekeazo mipaka ya nini ni sahihi na nini si sahihi.
Kuna tamaduni zituhakikishiazo kuwa tufanyayo ni sahihi na wafanyayo si sahihi.

Samahani stori kidogo......

Nakumbuka nilipokuwa katika kozi moja ihusianayo na jinsi ya kukabiliana na watu wa tamaduni tofauti, ambapo ikafikia wakati karibu kila mtu akawa hajiamini kuwa asemacho au akiongea kwa kutumia saini , hamkorofishi mwenzie.Ilifikia pia kuogopa kusema au kuongelea topiki fulani kutokana na ngazi tofauti za uwashawasha wa toki hizi katika tamaduni nyingine. Katika baadhi yatopiki watu wakastukia kuwa nimetahiriwa. Hiki ni kitu ambacho Warusi na Wazungu wengine wengi waliokuwepo kwenye kozi walikishangaa sana.Ukiwatoa wayahudi kwa Wazungu wengi kuwa na govi ni kitu ambacho ni kawaida sana .
(Nakumbuka lakini tuna makabila mengi tu Afrika na duniani, yaonao kitendo hiki ni cha ajabu .Kumbuka katika tamaduni nyingi ni mwiko kufanya govi na vipengele vingine vihusianavyo na sehemu za siri kuwa topiki yakuongelea.)

Duh!
Samahani kwa wale wanaoweza kukwazwa na lugha niitumiayo kijiweni....!


Basi bwana...

  • Tukagundua kuwa kwa Wajapani saini ya kuonyesha pesa , kwa Waperu ni tusi.
  • Uitaji mtu wa kawaida kwa Wafini, Kwa mtanzania ukiitwa hivyo na kidole kimoja, maana yake akuitaye anakudharau.
  • Kitendo cha kupungia gari ilikulisimamisha kwa Mtanzania, sehemu kibao ndio kupungia Kwaheri!
  • Kukataa kwa kichwa Watanzania tulikokuzoea kwa wengine ndio kukubali.
  • Nakadhalika kadhaaa......
Dini nazo zinatufundisha ni nini sahihi.
Tatizo ni kwamba nini sahihi katika dini moja , sio lazima ni sahihi katika dini nyingine.
Ukiwa Muislamu, nguruwe haramu. Ukiwa Mhindu, ng'ombe haliki....nk
Halafu madoido ya binadamu, unaweza kukutana na Vegan mpagani lakini kwake nyama yoyote haramu.
Swali:
Kila mwenye dini , dini yake inamwambia hiki akifanyacho ndio sahihi,
Sasa nani ni sahihi kikweli kweli?
Ushawahi kukutana na asiyeamini dini mpaka kutoamini kwake dini inakuwa dini?

Maswala ya tamaduni nyingi yamekataza sana mambo mengi , lakini kuongelea ngono ni mojawapo. Naamini swala hili limekuwa jambo likwepwalo kuanzia ndani ya famili.

Stori kidogo.....

Nakumbuka baba yangu siku moja alivyokuwa anajaribu kutaka kuongelea swala hili na mimi. Alikuwa anataka kunionya kuhusu kujiadhari na ngono na tatizo la UKIMWI hasa baada ya Zubeda fulani kuwa anakuja sana kunitafuta nyumbani. Jasho lilimtoka , na mimi ingawa nilikuwa najua anataka kuongelea nini, nikawa simsaidii kumpa jinsi ya kutoa somo kirahisi. Lakini alifanikiwa baada ya kutoa jasho kunipa statistics za Ukimwi na jinsi gani nijiadhari nk. Nafikiri kungekuwa na maswala yakupelekwa jandoni angeweza hata kunipeleka huko ingekuwa somo hili liko katika silabasi ya jandoni.

Ombi:
Kama kunamtu alifanikiwa kupelekwa jandoni au unyagoni, ningeomba atushushie silabasi ya masomo ya jandoni au unyagoni.Kwa sababu nina wasiwasi na ufupi wa muda shule hizo zinavyotumia kutoa krashi kozi ya maisha.

Hebu Mcheki Alexyss K. Tylor akiwa na mama yake ayaongeayo....(tafadhani lugha atumiayo yaweza kuwakwaza baadhi na sina uhakika kama uko chini ya miaka yaukubwa ni vizuri kwako kumsikiliza)



Katika tamaduni kibao jambo afanyalo Alexyss haliwezekani.
  • Chakusikitisha ni kwamba maswala haya ya ngono kutokana nakutoongelewa sana na kiuwazi , imefikia kuwa ndio yanayoongoza kwa kutafutwa mtandaoni.
  • Cha ajabu asilimia kubwa ya mambo ya ngono yapatikanayo mtandaoni, hayamfundishi kitu cha muhimu mtafutaji wake, zaidi yakumsaidia katika swala la tule tuhamu.
  • Chakusikitisha maswala haya , kutokana nakutofundishwa vyema, au kutokana na kuwepo habari nyingi potofu juu yake, yamekuwa ni chanzo kikubwa cha uenezaji UKIMWI na ukosaji furaha ya mahusiano ndani yamahusiano ya watu(Iwe ndoa au nanihiii...).
Eti mpaka sasa kunao wanaoamini kuwa ukifanya ngono na bikira unapona UKIMWI, kitu kifanyacho watu hasa kusini mwa Afrika kubaka watoto.

Swali:
Hivi kweli ni sahihi kukaa kimya kutokana na ukweli mambo mengine hatakutamka ni jambo litutialo kinyaa?

Hebu nikukumbushe ule wimbo wa Boku wa .... Wimbo wa doli....



Sasaaa....
  • Hivi ni nini sahihi kuongelea?
  • Je, hayo maongezi ni muhimu kama hakuna yafundishayo jamii kupiga hatua yakimaendeleo, kiakili, kifikira....nk ?
Naamini maongezi yasiyojenga nikupoteza muda, hasa ukifikiria maisha ya binadamu yalivyo mafupi hata kabla hujafikiria muda binadamu autumiao kulala nk..
  • Lakini hivi ni maongezi gani ndio sahihi na yanayojenga na kuchangia kumuendeleza binadamu?
  • Nani yuko sahihi kuliko mwingine ambaye ana haki yakuamulia wengine ni nini sahihi kuongelewa?
Duh!
Ngojea nikuache basi!
Jumapili njema!
Nakuacha na Maroon 5

Read more...

Mambo ya Kufananishwa ......

>> Saturday, July 28, 2007

Duniani kuna watu wanaamini kuwa Wachina wote wanafanana!
Watu weusi wote wanafana!

Nakumbuka kipindi cha miaka ya tisini, ukiwa mweusi ukakatiza nchi kama Finland, watu wanakuwa na uhakika kuwa wewe ni Msomali , halafu mkimbizi. Walikuwa hawawezi kutofautisha watu weusi. Na kutokana na uchumi wao miaka hiyo kuwa mbaya, basi hukawii kutupiwa jicho la chuki kuwa umekuja kuwaongezea shida.
Sasa hivi ukiwa unamandevu ,ukafananishwa na Bin Laden fulani,ukikatiza Airport hukawii kuitwa pembeni wakakucheki zaidi mizigo yako.

Swala la kufananishwa lina mambo yake....

Ngojea nikupe kastori kalikonitokea jana......


Nanukuu nilichoombwa jana....
`Sorry Brother!, I am desperetely in need of Ur help! I see U in this joint often and I am interested in a girl who is into Tracy chapman. I think U.......´

Ngojea nirudi kwenye kilugha........


Jana kuna mtu(hata simkumbuki jina) alikuwa anampa kauli mwanadada mmoja, ilikujiongezea pointi akaamua kumdanganya kuwa yuko na mimi, halafu eti mimi ni mdogo wa Tracy Chapman,nimekuja kumtembelea.Ilibidi niwe naitikia chochote asemacho kuhusu uhusiano wangu na wake na wangu na Tracy Chapman.Kwa bahati nzuri naijua historia ya Tracy, hivyo maswali fulani kuhusu yeye nilitoa majibu.
Hebu cheki picha zangu na Tracy.....

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Tracy Chapman(picha na Steve Granitz/WireImage.com)
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mimi
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mimi
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Tracy(Picha na David Atlas)
Duh!
Je tumefanana?

Ngoja nigusie na....
Kipindi nilichokuwa Tanzania, kuna watu walikuwa wanakuja kunisalimia wakifikiri mimi ni
Q Chifu.
Sasa naanza kuogopa kwa maana siku moja mtu atanifananisha na kibaka aliyemuibia ,halafu nitakula mkong'oto.

Kuhusu jana chakusikitisha ni kwamba ....nilikubali kufanya maigizo. Na si utani , aliyeambiwa hakujali hata kiswanglish changu, aliamini kabisa anachoambiwa kuhusu undugu wangu na Tracy.
Nasikitika kwa kusapoti uongo , lakini ilikuwa ni kaigizo fulani kanakochekesha na kaliniondolea ka-boredom fulani na.............vilevile kalinifikirisha.

  • Chakusikitisha ni kwamba kuna watu wanaweza wakakubali kufanya chochote wakihisi wewe ni mtu Maarufu.
Cha ajabu kumbe hata ukifanana na mtu fulani maarufu , unaweza kupata pointi anga fulani.

Lakini...

Watu maarufu , wanapata raha na pia kusulubiwa kwa kujulikana kwao.
Ukiniuliza mimi , naweza kusema , wale wa karibu na watu maarufu, au wenye kujuana na watu maarufu , mara nyingine ndio wafaidio kuliko hata wale watu maarufu wenyewe.

Kuna mshikaji wangu alitaka kujua kama ningependa kuwa katika nafasi ya Mandela!
Wote tunajua kuwa Mandela ni mtu maarufu, na aheshimikaye sana duniani.Lakini mimi nitakuambia, hata siku moja huwezi kunifanya nitamani kupitia na kuishi aishivyo yeye.Mzee kama yule hana nafasi hata ndogo ya kukosea. Siku akisikika katukana au kapitia mtaa gani sijui, dunia nzima itasimuliana hicho kitu. Na hadithi nyingine kemukemu zitazaliwa za kumpaka matope.
Lakini ukiniuliza kama nataka kuwa rafiki yake, hapo tutaelewana.

Nikirudi kwenye hoja.......

Tatizo ni moja tu!
Huwezi kuchagua nani utafanananaye. Kirahisi tu, unaweza kufananishwa na kibaka fulani.
Ushawahi kusikia kuwa mara nyingi mtu na mke wake hufanana?
Swali:
Kwanini watu huchukia kufananishwa na mtu nishai?
Mbona hatujiulizi ,hivi ni kibaka anafanana na mimi au ni mimi nayefanana na kibaka?
(Unajuatena yale maswala ya kuangalia glasi ya maji na kuiona imejaa nusu na sio imepungua nusu.)
Ee bwana ee Jumamosi njema!


Mpate basi Tracy Chapman na BB King


Najua leo ni Helsinki Vs Tampere kwenye mpira wa miguu!Samahani Ezza , nilipitiliza.Si unajua nilijidanganya kuwa ngoja nilale kidooogo.....Nilipoamka nimechelewa nikajua mchuma utakua umeshaondoka.

Read more...

Mtoto wa Mwenye Nyumba afananapo na hausiboi!

>> Friday, July 27, 2007

Swali:
Hivi Butler si ni hausiboi?

-Mbona sasa hausi boi akiitwa butler watu wanamchukulia kuwa yeye babu kubwa?
Unamkumbuka butler wa Princess Diana?

Tuache hilo.....
Namsikiliza Erick Wainaina hivi sasa wakati naandika. Kuna wimbo mmoja naupenda jaribu kuusikiliza nyuma ya mahojiano yake hapa....

Nikirudi kwenye hoja.....

Uhausiboi ni kazi fulani watu huidharau Bongo ingawa inampatia mtu kitu kidogo.
Lakini nawakumbuka mahausiboi fulani enzi hizo, wa jirani zangu, ambao karibu sisi wengine wote mtaani tulikuwa tunawaonea wivu.

Pata stori fupi basi....

Enzi hizo, mimi, pamoja na karibu kundi langu lote, tulikuwa ni wanafunzi.Pesa usipopewa na wazazi basi kasheshe. Kulikuwa na jamaa aitwaye Joseph, hausiboi wa Daktari fulani na mwingine Laurent, hausiboi wa Mfanyabiashara tajiri fulani, walikuwa wanatufanyia maswala ambayo kwetu ilikuwa miujiza.Hawa jamaa walikuwa na mshahara halafu watundu. Lililoongeza tatizo na wivu kwetu,ilikuwa ukweli kuwa wengi wetu tulikuwa katika umri fulani ambao ,kwetu wanavulana , kulikuwa hakuna kingine cha maana au kipitiacho akilini zaidi ya mademu. Karibu wake za watu wote mtaani wasiokwenda kazini, hawa jamaa walikuwa wanawaneemesha.Halafu wote wawili walikuwa ni chaguo la mama mwenye nyumba, ambaye alihakikisha wanapata kazi. Moja ya shughuli yao ilikuwa ni kuwa wasafi na kunukia vizuri. Tulikuwa tunakaa karibu na hosteli ya wasichana tupu(Hostel ya Moro Sec).Na kwa kawaida wanafunzi hawana pesa sana kama ijulikanavyo. Hivyo hawa jamaa walikuwa wanatumia fursa hiyo kujichagulia yeyote wamtakaye ambaye anashida na pesa na hanatatizo na kuchukuliwa na hausiboi, na afanyaye watakayo. Walikuwa hawafi njaa ya nanihii! Mpaka leo sijui walikuwa wanafanyaje! Kwasababu hawa jamaa pamoja na uhausiboi ambao ulimuhakikishia baba mwenye nyumba kuwa wanafanyakazi, waliweza kumtosheleza mama mwenye nyumba, na wengine wote watakao mtaani. Baadaye nikaja kugundua pia walikuwa na maumbo ambayo wanadada fulani huyapendelea.Ingawa inasemekana wanadada mtaani walisimuliana pia kuhusu nanihii, hivyo kila mmoja akawa anamaswali ambayo hawajamaa walikuwa tayari kuyajibu kwa vitendo.

Tuachane na hako kastori basi.......

Niliwahi kuandika kuhusu hausigeli na kasheshe zake. Leo nilitaka kugusia Hausiboi na kasheshe zake ingawa nime....

Watu tunajijengea kasumba kuwa nani ni zaidi na nani sio. Wengine wengi tunapata maana yakua sisi ni nani au kujitambua, kupitia nini tunafanya.Lakini kumbuka hiyo ni kasumba ya kujijengea tu.
Utasikia mtu akisema, kuwa yule hafai kwa sababu hana kazi, kazi yake ya kipuuzi, mshahara wake mdogo, nk. Lakini huyu bomba kwa sababu........

Kumbuka , mwisho wa siku, mahusiano ya watu na kuvutiana kwa watu kiini chake ni jinsia ya akuvutiaye. Kama waliowengi waaminivyo ilivyo kawaida ,kiini cha kuvutiwa kwao ni lazima kitakuwa mtu wa jinsia tofauti afikiaye mizani ya matamanio na kutimiza yale ya msibuyo kimatamanio katika kipindi hicho.Kama Msenge au msagaji, utavutiwa tu na mwenye jinsia yako, hapa hakuna cha mshahara , kazi yako wala nini kama kiini cha jambo hilo.

Swali:
Unafikiri ,wote uwatamanio cha kwanza kikujiacho akilini ni wanafanya kazi gani?

Nakubali pia kuwa unaweza kuvutiwa na afanyacho mtu au baikeli yake gari na........
Lakini....

Kutokana na baadhi ya utafiti uliofanywa na wanasayansi kibao, unaambiwa kuwa mwanadada ni rahisi kuonja nje pale awapo katika zile siku mayai yako tayari kupokea mbegu za kiume. Inasemekana kipindi hiki vile vile huvutiwa zaidi na wanaume wenye sura za kiume zaidi.Ukiwa na sura fulani ambayo unaweza kufananishwa zaidi na mama au dada yako, halafu hausiboi wako kafanana na babayake, basi kasheshe kama mambo fulani mwanadada uliyenaye huumtimizii.Wanaume wengi wanasababu zao kwa nini wanaweza kuwa na nguvu nje ya ndoa, mahusiano kuliko ndani ya ndoa.
Tafuta kazi za Professor Robert Winston kuhusu Human Instinct kwa stori zaidi kuhusu huu utafiti.
(Kumbuka niongeavyo hapa, sio ndio ukweli asilimia zote kwa wote)

Lakini jiulize, wakati hutimizi, una hausiboi?
Ndio , mamaa ni bomba la mdini, kwa hiyo atajizuia. Si wote tunajua yeye ni Swala tano, sala zote na........ anahudhuria.
DUH!

Lakini........

Duh!
Nisikutishe!

Najaribu kuweka hili wazi kwa mara nyingine.......

Kazi ni kazi.
Jamii tu ndio inatabia mbaya ya kupendelea baadhi ya mambo na kutafsiri nyadhifa za watu kama vile ni muhimu kuliko mengine katika maisha ya binadamu.
Kama unapata kitu kidogo kwa shughuli zako zozote, mimi nakupa tano.
Binadamu kabla ya yote atakutambua wewe kama binadamu , na kwa ubinadamu wako.

Usishangae ni kwanini mtoto wa jirani anafanana na hausiboi lakini!
Kumbuka kabla ya yote , utu wake ndio kigezo cha mama mwenye nyumba kuvutiwa naye, ingawa ni siri.
Lakini, si ni baba mwenye nyumba mvivu au ana kazi nyingi zimfanyazo awe amechoka awapo nyumbani kuwakilisha yahitajiwayo katika mahusiano?

Lakini timiza utakiwacho kwenye mahusiano yako basi!
Wiki Mwisho njema!
Nakuacha na Slum Village wakiwa na Dwele

Read more...

Kwa Mtakatifu Ng'ombe, Msalaba, Sanamu na.........

Napenda binadamu anavyo tafuta na kupata maana ya maisha , imani....katika karibu kitu chochote.

Uhusiano wa binadamu na Vielelezo kama bendera , sanamu , msalaba nk.... hunionyesha kasiri kamoja ka ubongo wa binadamu ufanyavyo kazi.

  • Ukimouona Mkristo aliyebobea aukodoleavyo msalaba...
  • Mkatoliki akodoleavyo sanamu ya bikira Maria na.....
  • Mmarekani mwanajeshi akodoleavyo bendera ya Marekani....
  • Mwanasiasa ya ujamaa akodoleavyo sanamu ya Mwalimu Nyerere...

  • Muislamu a.....
Inamaana kuna kakitu anakaelewa katika hicho kielelezo. Nakumbuka mara nyingi tulivyokuwa tunalazimishwa kusimama wakati bendera inapandishwa, lakini asilimia kubwa ya watu wanasimama tu kwa kuogopa polisi na sio kwa kuheshimu bendera. Kwa hiyo nakubali kuwa vielelezo vingine tunajifanya tunaviheshimu kwa sababu tunalazimika kujifanya tunaviheshi, kuvipenda nani muhimu kwetu.

Kabla sijaendeleaa...
Hebu tu mcheki kidogo Mtakatifu Ng'ombe basi......ambaye analeta maana ya utakatifu kwa baadhi ya binadamu wenzetu.....


Duh!
Sikatai! Vielelezo hivi vinamaana kwa viwahusuvyo. Vinawajenga katika waaminiyo na kuwaunganisha waaminio. Huletea watu kujiamini, na kuwafanya wengine wajitume zaidi kufikia watakako kufikia.

Misri na Piramidi zao ni miongoni mwa baadhi ya vielelezo ambavyo , baada ya muda vimegeuka maana kutoka kuwa makaburi mpaka alama ya busara na ufundi wa wakale. Alama ya kujivunnia Umisri na hata Uafrika. Pia kuwa ni alama muhimu ya nchi ya Misri.

Picha ya Mandela wakati wa kugombea uhuru Afrika kusini ilikuwa ni kielelezo chakuwapa mori na moyo wapiganaji .

  • Kwa hiyo nakubali kabisa kuwa kunavielelezo vingi viwezavyokutumiwa kusaidia watu kufanya vizuri zaidi, watu kufikia wajipangiayo, watu kujiamini nk.
Lakini ni vielelezo gani ambavyo ni muhimu kwa Afrika na Waafrika?

Kwa Tanzania....

-Mbona hatuoni hata Sanamu za akina Filbert Bayi?
Naamini mtu kama yule angekuwa kielelezo kiwapacho matumaini wote watakao kuingia katika riadha.

-Mbona akina Hukwe Zawose, Mzee Nyunyusa hawana vielelezo vyao kama sanamu hata katika anga au nje ya mojawapo ya ofisi za sanaa?Naamini ingekuwa kielelezo kizuri kwa Wanasanaa.

Hivi ni Wanasiasa tu ndio muhimu kujengewa vielelezo hivi?Maana naona ni akina Nyerere , Sokoine nk. ndio tunawakumbuka kwa hilo.
Wengine Je?
Wote tunakubaliana asilimia kubwa ya wanasiasa wetu , wamekuwa si vielelezo vya kujivunia.

Swali:
Unafikiria Watanzania kama binadamu wanatambulika, ikiwa Tanzania inajulikana kwa kuhusianishwa na Mlima Kilimanjaro au mbuga za wanyama tu?
Binadamu , akili zao ,busara zao, uzuri wao viko wapi?

Najua kunamtu atataka kunikumbusha kuwa Watanzania ni watu wa amani na wakarimu.
LAKINI Unauhakika?

Chakusikitisha ni kwamba, bado Afrika kwa ujumla , kielelezo kitambulishacho bara ni matatizo.Njaa,umasikini, magonjwa, uvivu,ujinga na ugumu wa maisha.

Cha ajabu Afrika na watu wake ,hakuna sababu ya maana isababishayo tushindwe kujinasua katika jambo hili.Na ukweli vielelezo vitutambulishavyo hatuhusianinavyo.

Kazi kwetu!
Kwa sababu ni mimi na wewe tunahusika katika kugeuza mambo Afrika.
Sisemi kuwa ni rahisi!
Basi Ngojea Maxi Priest na Beres Hammond watuulize...

Read more...

Sanaa ya Danganya Toto!

>> Wednesday, July 25, 2007

Ukifikiri sana, karibu kila kitu ni uongo.
Binadamu anaakili mpaka imefikia kiasi cha kuudanganya ubongo wake kuwa yamzungukayo ni ukweli.

Swali:
Hivi Uongo ni nini?
Ushawahi kudanganya?

Kuhusu mimi, nahisi unajibu:-)
Kabla sijasema msikilize huyu...


Mtoto anapozaliwa, kabla hatuna uhakika kuwa anaelewa, mimi naamini kuwa anastaili zake za kudanganya.Nilikuwa na mcheki mtoto mmoja wa rafiki yangu juzi. Huyu mtoto anaweza kudanganya kuwa anausingizi ili apelekwe chumbani. Akishaachwa chumbani hafanyi kelele wala nini, lakini baada ya muda utasikia TV imewashwa, ukifika huko unakuta nguo zote kabatini ziko chini, na karaha kibao. Yeye anapenda kuchezea nguo. Hivyo kagundua akiachwa pekee ndio anazichezea bila kubughuziwa.Hivyo akagundua mchezo wa kujifanya amechoka iliapelekwe chumbani ambako anapata uhuru wake.Umri wake mwaka mmoja lakini anajua jinsi ya kuwadanganya wazazi wake ili wampe nafasi. Kuna mifano mingi tu!Nasikia hata mimi nilivyokuwa mdogo , nilistukia kuwa nikiumwa, napewa chakula kizuri zaidi nikipendacho kirahisi.Nafikiri unajua maswala ya kuletewa chakula kizuri ukiwa mgonjwa halafu siku nyingine inabidi ule kile wenzio wanacho kula. Nafikiri unajua kautundu gani kanatakiwa hapo ili upate msosi mwingine bomba!

Sasaaaa....

Si umecheki hiyo video hapo juu? Tunashauriwa eti tuwadanganye watoto, wapenzi wetu, hata ....

  • Lakini kuna yale maswali fulani!Nafikiri unayajua yale........!AU?
Utayajibuje kiukweli ?
Lakini kudanganya si ni dhambi eeh?

Ee Bwana ee!
Kumbe kumdanganya mpenzi wako pia mali sana, kama unajua kuwa ukweli utamzingua tu.

SASAAAA!
  • Wewe mwanadada ukiniuliza kuwa tokea nikonawe simtamani mwanadada mwingine unatarajia nijibu nini?
  • Hivi wewe mwanadada ukinisimulia story zako za mwanamume uliyekuwa naye kabla yangu na jinsi alivyokuwa bomba na alivyokuwa anaku.... unafikiria nini?Hatakama nimekuuliza..! -Si unidanganye tu kuwa alikuwa uchwara au hujawahi kuwa na mwingine kabla yangu, yaishe?
  • Hivi wewe mwanakaka utakapo kujua sana kwanini leo Mamaa anaenda sokoni tu lakini katilia mavazi na pafyumu ile baabu kubwa , unategemea jibu gani?
  • Na kadhalika kadhaa.......
Samahani sijagusia kile kimfano ulichotaka nigusie hapo juu!

Duh!
Basi bwanaaaaa..........ngojea niendelee kukupa dondoo tudanganyanazo.
  • Umependeza sana!
  • Hiyo nguo imekutoa sana!
  • Wewe mzuri!
  • Una akili wewe!
  • Nilivyokuona tu nikagundua kuwa malaika hawapo mbinguni tu!
  • Sijawahi kumpenda mwingine ila wewe tu!

AU?

Duh!
Tuendelee na viuongo...

  • Mjinga sana wewe!
  • Kichwa kama kachori!
  • Afrika Maskini sana!
  • Marehemu alikuwa mtu Mzuri sana!
  • Yule rafiki yangu sana tu!
  • Na kadhalika kadhaaaa.....
Duh!
Ngojea wakati unafikiria kuhusu hilo nimuache Eek a Mouse asimulie kuhusu swala ......


Katika sanaa ya kudanganya , hakuna mabingwa zaidi ya wapatikanao kwenye maeneo ya dini.

Nisikuficheee......!

Napenda kuona watu wanapenda dini. Kwa sababu naamini wanadamu wengi kwao, ni vigumu kuwa na misimamo ambayo inaendesha maisha yao na inajaza maisha yao maana. Majibu ya kwanini wako duniani, maskini,matajiri, wagonjwa hivi, mpaka pale kwenye, hivi kwanini imenitokea mimi na sio yule, ni maswali magumu ambayo akili ya binadamu ina ufinyu wake na mara nyingi kutokana na uvivu wa kibinadamu wa kufikiri, inashindwa kupatiwa majibu.Dini imesaidia sana kumfanya binadamu kuendeleza uvivu wakutafuta majibu, lakini imemsaidia mara nyingi kuweza kufurahia hali yake aliyonayo, kutokana na majibu dini iyatoayo yatulizayo ubongo na ...

Dondoo:
Dini ni bomba la kituliza ubongo. Lakini kumbuka kuna mengi binadamu ajihangaishayo nayo kajitungia mwenyewe.


Bila dini, naamini dunia ingekuwa iko navituko na majanga mengi zaidi yasababishwayo na binadamu na kaubongo kake, kuliko ilivyo sasa.
Duh!
Binadamu kiboko!Eti baadhi ya wenye akili wameamua kupigana vita iuayo watu Iraki, ilikuleta amani.(Kumbuka lakini kuwa dini hizi zihubirizo amani, mara nyingi zi chanzo, kati wala...kiini cha amani
)

Naamini binadamu anahitaji kupata maana ya maisha na kujua kwanini utamu na uchungu ni vitu vimzungukavyo kila siku.Asipojua vilevile, ni muhimu awe katika hali ya kutafuta kujua, kitu kimfanyacho apitishe siku akiwa anamategemeo fulani ya kesho na utulivu wa akili au akili iliyotawaliwa na fikira zimfanyazo kutoonyesha unyama wake.

Naamini binadamu aligundua dini kutokana na hii hali yakutaka kuelewa maisha na woga wakutojua maisha na baada ya maisha ayaelewayo.
Kuna watu nikiongelea dini wanafikiri naongelea Ukristo na Uislamu ambao ndio miongoni mwa dini chekibobu duniani.Dini chekibobu ,nikimaanisha zijionyeshazo na zisakazo wafuasi mpaka chini ya uvungu.Dini zipendazo kuwahakikishia wafuasi wake kuwa ndizo za kweli ingawa pia hutumia uongo pia kujiuza.

Ngojea nikutulize kidogo na kideo hiki....


Swali:
Hivi unajisikia vibaya kwenda kanisani bila pesa eeh?

Samahani , nilisahau kuwa inawezekana kuwa wewe si mkristo.

Basi tuendelee....

Hivi unataka niendelee kweli kukuelezea kuhusu sanaa ya uongo mpaka kwenye siasa?
Hivi ukisikia Wamarekani wanavyodai wanapigania demokrasia , si utafikiri ni kakitu fulani kazuri kweli eeh?

Swali:
Unajua maana ya demokrasia?
Simmesikia ikihubiriwa?
Umeshawahi kuona nchi yenye demokrasia?

Sawa , nimekuelewa.
Duh!
Hivi ulinielezea ka kitu eeh?:-)


Nafikiri unafikiri Rais Kikwete aliyepigiwa kura na Watanzania karibu wote waliopiga kura, ni matunda ya demokrasia.Lakini si unajua Watanzania waliowengi hawajui hata ni nini kinaendelea Tanzania zaidi ya danganya toto wanasiasa watoazo?
Unachotakiwa kudanganya ukitaka kupigiwa kura ni.......,
  • Ahidi lolote ufikirialo wanahitaji mtaani kwao.
  • Kama wananjaa, wape wali na kuku kwenye mikutano yako.
  • Waahidi hata helkopta, bila ya kusema utazinunuaje.
  • Waahidi utawasaidia wale chipsi mayai , pilau kila siku ukichaguliwa.
  • Waahidi utawawekea bomba la maziwa ingawa unajua hawana maji.
  • Kama wagumu kidogo, waahidi utatunza amani.Halafu usisite kuwadanganya kuwa mpinza wako ataleta vita kama ya Rwanda.

Duh!
Au ni George Bush nini unafikiria alichaguliwa kidemokrasia?
Lakini kafuzu katika Sanaa ya danganya toto.

Ngojea nikuache utulie basi!
Siku njema!
Nakuacha na Mark Morrison
, anayekupa kibao nilichokuwa napenda kusikiliza baada ya kudanganywa na mwanadada fulani.

Read more...

Vitu Nane Msivyovijua kuhusu mimi.

>> Tuesday, July 24, 2007

Duh!
Serina kanitagi......
Maswala ya kujieleza haya lakini.
Basi ngojea niseme.
Manane msiyojua kuhusu mimi ni:

1.Katika mitihani yangu yote shuleni, nilichowahi kufeli ni somo la lugha ya kiswahili.
2.Ningependa kuwa mrefu zaidi ya nilivyo.
3.Sipendi kunywa maziwa
4.Sipendi kusherehekea birthdays
5.I talk too much, ingawa nasifa ya ukimya.
6. Siamini katika dini yoyote, ingawa naamini Mungu
7.Mvivu kula
8.Mvivu kupanga nguo kabatini.

.......
Kuna mengi watu hawajui kuhusu mimi ingawa wanahisi wanajua.Naweza kuendelea mpaka kesho kutwa......:-)

Watu wanane naowatagi , watujulishe vitu nane tusivyojua ni:
1.Bwaya

2.Egdio.

3.Araway

4. Innocent

5.Sandra

6.Jeff

7.Chediel

8.Che

Read more...

Kwanini nampenda Hausigeli!

Dunia ni ya ajabu! Pamoja na mengine mengi, kaskazini, kusini, hata mashariki nilikofika, ni kawaida kukuta mwanamke akilipwa mshahara mdogo au akinyanyasika kuliko mwanamume.
Au akilazimika kufanya hata ambayo si lazima.
Lakini ni kawaida kusikia wanadamu wakimsififia MAMA.
Ngojea basi tufyekewe...


(usifikirie nasema mwanadada hapo kwenye kideo hafurahii kazi au kakosea)

Mhhh!

Kamusi kidogo!
Hausi=House
GELI=Girl
Hausigeli=Mwanamke akaaye kwenye nyumba.
AU?
Mnyonge, Mnyongeni, kuna watu wasema!
MIMI NASEMA MNYONGE MPENI NGUVU.
Kabla sijasema.......
Swali:
Unamjua mwanamke akaaye kwenye nyumba?
Mpate Sekouba Bambino


Lakiniii....!
Hausigeli akikataa, kazi kajifukuzisha.
AU?
Yule hausigeli kwa wale walionacho, na afanyaye kazi iliwale mahausi geli na mahausi boi , wengine , wenyejeuri ya kulipa mshahara, walio hata na nyongeza ya watu nyumbani, hunyanyasika.

Sasaaaaa....
Dunia ya sasa, ndio kwanza tumepata mwanamke wa kwanza Rais INDIA.
Dunia ya sasa ndio kwanza , Mrs Clinton anakuwa mwanamke wa kwanza USA kuchukuliwa siriasi kuwa ni mgombea wa Urahisi.

Katika jicho la wanaume katika jamii nyingi , mwanamke ni mzuri halafu anasehemu za siri wanamme watakazo kuzitafutia urafiki na sehemu zao za siri, na zaidi ya kazi za nyumbani, mwanamke hana cha zaidi.
AU unabisha?

Lakini........
Cha ajabu , katika jamii karibu zote wanaheshimu mama.
Na wanajua kuwa mambo mengi muhimu duniani yafanywa na mwanamke.....

Swali:
Hivi MAMA si ni mwanamke?
Mbona Unamheshimu?
(Au wewe huna heshima?)

Cha kusikitisha nikwamba....
Kizazi cha Arap Moi, akina PAPA Benedict ,mimi na wewe, ambao wananguvu za kudhoofisha wanawake, na wa dhoofishao wanawake, ndio bado tunao katika dunia ya sasa idhalilishayo wanawake na kuamini wanaume ni zaidi.

DUH!
Mheshimiwa samahani kama sija kutaja(Zaidi ya Arap na Benedict), kama unauhakika wanawake ni wanyonge.

Lakiniiii..........


Swali:

Ushawahi kufanya mapenzi ya kuibia?

Mapenzi ya siri ni matamu.
Duh!
Nahisi hakuna kitu ambacho ni mapenzi ya siri ambayo hutashikwa.
Nahisi unajua ni mapenzi ya siri kwa sababu unajua utashikwa au kunauwezekano wa kushikwa, halafu hutaki kudakwa.
DUH!
Samahani najua kuwa hausigeli, inamaanisha wanadada walio pewa kazi za nyumbani katika kona fulani,
.....za wenye maisha fulani,
....... hasa katika nchi fulani,
......hawa mahausigeli hutokea sana vijijini , kutokana na matatizo fulani,

.....Lakini ukilitazama hili jambo kwa jicho fulani,
.....na katika maeneo fulani......!
Hawa waliowengi maarufu kama mahausigeli fulani
...Wafanya tu kitu fulani
kwa kuogopa mambo fulani ...
ya....

Ok naaachaa basi kukuzingua!
AU?

Lakiniiii!
Kwa difinisheni yangu ya hausi geli hapo juu waweza kusema ....

MIMI NI HAUSI BOI fulani......
AU?

Kumbuka namzumgumzia mwanadada akaaye kwenye nyumba.....
Kumbuka namzungumzia mwanadada umfanyishaye kazi pale nyumbani........
Kumbuka namzungumzia mwanakaka umfanyishaye kazi pale nyumbani na mwanakaka umuitaye mpenzi.
Duh!

Swali:

  • Hivi ni kweli, kwako wewe ninakuchanganya kwa staili yangu yakuongea?Fikiria kidogo utanielewa.
AU?



Ngoja nikupatie picha za jana nilipokutana na Bloga maarufu wa Tanzania aitwaye MAGGID Mjengwa.




Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Maggid Mjengwa
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Rupia
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Aliko eeh?
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Tommy eeh?
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mtimkubwa eeh!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mjengwa na Aliko
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Rupia na Mjengwa
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Kaka Mjengwa na Mimi
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Tommy na Mimi

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Timu fulani
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Timu niliyomisi.


Kabla sijaanza!Namaanisha kabla sijaacha kukuzingua hapa leo......
Nilitaka kukuelezea tu kuwa ingawa kichwa cha habari kiliku....
Nampenda Hausigeli kwa sababu nampenda tu!
Au wewe ulikuwa unafikiria nini?

Lakini mwanadada , wampenda hausi boi?

Kama unasoma hapa U
sitishike!
Usipofikiria kinamna, huwezi kunielewa.
Endeleza siku basi.
Siku njema!
Nakuacha na.....Thandiswa Mazwai

Read more...

Haja Kubwa!

>> Saturday, July 21, 2007

Mahitaji yana mambo yake!Umuhimu wa haja kubwa na ndogo, inategemea na kasheshe ikuleteayo mshawasha katika muda.Haja ndogo ni kubwa kama umebanwa.Na kama unapata haja, inamaanisha umekula au kunywa.
Duh!Sijui kwanini nakumbushia mambo yaliyo wazi , ambayo haihitaji kukumbushwa wala...
Au?
Swali:
Hivi ukikumbushwa ulijualo ni noma?

Ngojea ni jaribu basi kukukumbusha ulijualo.
Unamkumbuka Mungu?
DUH!
Hebu tumcheki kidogo kwa jicho la Professor Robert Winston


Ngojea nikuache na picha za jana basi!

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mimi
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mzee Adam
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Edo na Peter
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Peter na Mimi
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mimi na Dr Mtafungwa
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
India Arie
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
India Arie ehh!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mimi na Edo tukiburudishwa na India Arie..
Ngojea umsikilize kidogo..

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Zubeda na Mimi
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Kenya na Tanzania
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Cuba,Tanzania,Tanzania,Brazil
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Redrama
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Redrama eeh!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
The Roots Kazini
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Q'love eeh?
Wapate basi kidogo The roots waliotuburudisha jana wakiwa na Jill Scott


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Maswala ya Sly na Familly Stone


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Sly
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Jioni
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Jioniiii!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Usiku
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Simon leo safarini
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Simon eeh?
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!
Mpate basi Sly na Familly..

Basi nimestukia kuwa nimeweka kideo cha zamani sana!
Samahani lakini! Napenda Arrested Development

walivyochezea kibao cha Sly kiitwacho People Everyday..
kisikilize basi....

Jumamosi Njema!

Read more...

Dume Zima Linafuatilia Mambo ya Wanawake!LOH!

>> Thursday, July 19, 2007

Swali:
Ushawahi kusutwa?

Kabla sija sema....Ngojea Mr Blue amzungumzie nani hiii.....

Inajulikana kuwa, wanawake na wanaume ni tofauti katika kufikiria maumbile nakadhalika nyingine kadhaa.Wengine wamefikia kufananisha wanaume na mbwa, wanawake na paka.Eti mwanamme anaweza kuwekwa mkononi kwa mbinu zilezile unazoweza kumzingua mbwa. Paka nafikiri unamjua mambo zake!
Duh!
Wengine hutofautisha tu sayari watokazo wanaume na wanawake.Eti wanaume hutoka Mars na Wanawake hutokea Venus. Hii yote ni katika kuonyesha jinsi gani jambo moja linavyoweza kuoneka katika kona mbili tofauti katikajicho la hawa binadamu wenye sehemu za siri tofauti.
Duh!
Swali:
Hivi wale wapendanao wenye sehemu za siri za aina moja inakuwaje vile?

Nikiliacha hilo....
Sasaaa......!
Tatizo linalojitokeza hasa katika jamii nyingi duniani , ni jinsi wanawake na wanaume wanavyotenganishwa na mila na desturi. Kitu kifanyacho ,kujuana kwa mwanamume na mwanamke kuwa sayansi ngumu sana.

Ni kawaida kabisa katika mila nyingi, mwanaume kukatazwa kusikiliza, kukaa na mwanamke ......, kuingia jikoni na mwanamke ndio kabisaaaa noma! Jikoni kunakuwa ni kwa wanawake, maongezi ya wanawake yanakuwa ni ya wanawake na kwa mwanamume si yakutilia maanani.Maongezi ya wanaume yanakuwa hayamuhusu sana mwanamke, hasa yakiwa hayahusiani na sentensi zimtakazo mwanamke kuleta chakula au kuja kidogo chumbani kwa dakika kadhaa za chapuchapu katika ku......

Ni kawaida kabisa kwa wanaume kukua bila kujua mambo yamuhusuyo mwanamke.Hata kuona chupi za kike kwa mwanamume ni nadra kwenye jamii nyingi.Kama mtu hana Televisheni, nafikiri yale maswala ya nyenzo mwanamke azitumiazo akiwa mwezini, yanakuwa kitendawili kwa mwanamume. Usisahau swala la kujua kuwa mwanamke huwa anasafiri kwenda mwezini kila mwezi ndio kabisaa halijulikani mpaka baadaye pale anapo.........

Mwanake yeye pia anakuwa anabunia yamhusuyo mwanamme, kwa kufananisha amjuavyo kaka , baba, na wale ndugu fulani wachache wafikao nyumbani, kisimani au pale... na yule mwanakaka ampendaye au aliyelazimishwa kuwa naye .Kumbuka!Mahusiano ya mwanadada na kaka,baba au ndugu ,hayagusishi sehemu fulani ya mahusiano yake na atakayeishi naye kama mpenzi,hawala, au yule tu aliyelazimika kuishi naye.


Tukiachana na maswala hayo...

Narudi katika swala lakujuana kwa mwanamke na mwanamume kifikira na kiutu.
Hili swala pamoja na mila na desturi kuchangia kuzoofisha majuano yake, naamini imefikia wakati wanamume na wanawake wenyewe kwa uhuru wao , bila kisingizio kingine, wanazidisha kudhoofisha ujuanaji huu wa jinsia hizi mbili zitamanianazo.

Ni kawaida kabisa kwa wanaume kusisitiza kuwa ; achana na hayo mambo ya wanawake wewe!
Au kumsikia mwanamke akiuliza; haya mambo yetu wanawake, wewe mwanamume unatafuta nini huku?
Najua mila na desturi na baoloji ya viumbe hawa wawili , hulazimisha mara nyingine ka-ukweli kasababishako , mwanaume aone maswala ya wanawake yanaboa, na mwanamke aone wanaume wanaongea ujinga pale kijiweni.

Swali:
Hivi ni kweli kuwa mawasiliano zaidi kati ya jinsia hizi mbili hayana umuhimu unaohitaji kuongeza mazungumzo na elimu ya kujuana kwa njia ya kuruhusu mabadilishano ya mitazamo na mawazo.......kati ya jinsia hizi mbili?


Kumbuka!
Hapa sijaribu kusema wanawake wasiwe na mambo yao au wanaume wasiwe na mambo yao binafsi.
Nakubali baadhi ya dini na watu wafuatao dini fulani , wao hawaruhusu mchanganyiko wa jinsia hizi mbili.Wao wanamafundisho yao kutoka vitabu fulani vitukufu ,viwapavyo maelezo ya jinsi ya kuwaweka hawa binadamu wawili wenye jinsia tofauti ndani ya ndoa wakaishi kwa amani furaha na upendo.
(Kumbuka!
Hapa naongelea umuhimu wakuongeza mawasiliano kati ya wanawake na wanaume, kwa maongezi....na si lazima kwa kuwakutanisha hawa binadamu wenye sehemu za siri tofauti uso kwa uso.)

Hivyo hapa nawalenga zaidi wale akina sisi ambao bado hatuja pata bahati ya kufungwa na maadili ya vitabu fulani.
Duh!
Nachojaribu kusema, ni kwamba....

  • Katika jamii inayotegemea wanaume na wanawake waishi kama mume na mke ndani ya nyumba, hainabudi hawa wanaume na wanawake wajuane vizuri . Na moja la jambo lisababishalo baadhi ya matatizo ndani ya maisha ya wapendanao wawili ndani ya uhusiano , ni kutoelewana kwa dhati kati ya mwanamke na mwanamume mapema katika maisha na pia ndani ya maisha.Hasa kutokana nakuwa na mawasiliano haba na yakwepayo mambo fulani muhimu yahusuyo binadamu hawa wenye jinsia hizi mbili tofauti (Samahani kidogo wasenge na wa saganaji hapa!)
Nakumbuka kuwa mila nyingi zilikuwa na mafundisho kama yale ya jandoni kwa wanaume na unyagoni kwa wanawake, ambayo yaliwafunza jinsi ya kuishi pamoja . Hili jambo halipo tena sana. Na lilipokuwepo, lilikuwa ni jambo la muda mfupi na kwa mtazamo wangu ,muda usiotosha kufundisha mtu jambo ambalo linatakiwa liwe muongozo wa kuishi na mwenzio wa jinsia tofauti kwa muda wote wa uhusiano wenu katika ndoa, ambao mara nyingi ilimaanisha mpaka kufa.

  • Nashukuru siku hizi kuna akina Dada kama DINAH wa DINAHICIOUS ambao hawana woga wakujadili maswala ya mapenzi , mahusiano na mengine mengi , kwa undani kwa kutoa mtazamo wa mwanamke katika maswala...., na kutoa baadhi ya mwanga kuhusu jinsi mwanamke afikiriavyo maswala haya.

  • Nasikitika kuwa kwa upande wa kina kaka, maswala ya mahusiano ya watu wa jinsia ...., tuyawekeayo umuhimu, sio swala zima la uhusiano.Mara nyingi hata tukiwatunaandika au kutafuta maswala ya mahusiano, tunajali kuweka au kutafuta picha na video za ngono ,zichocheazo mshawasha wa kufanya nanihii, lakini sio kumfunza mtu, yaambatanayo na kufanya nanihii na mahusiano ya wana jinsia hizi mbili kwa ujumla.


Swali:
Hivi hili swala la usawa wa wanaume na wanawake linawezekana kweli ?

Sasaa.......
Swala la nitakupenda mpakakufa na ndoa hii ni mpaka tufe, wote tunajua ni la busara sana.
Kusema ukweli linapendeza na ni tamu masikioni.
Swali:
Hivi unahisi watu wangapi katika ndoa wanapendana mpaka kufa na ndoa yao inadumu mpaka kufa?
Hivi ndoa kufa ni pale tu wanamahusiano wanapo saini karatasi kuwa wameachana?
Mpate D'Angelo basi...

Read more...

Heri ya Siku ya Kuzaliwa MANDELA!

>> Wednesday, July 18, 2007

Leo ni tarehe Mandela kafikisha miaka89!
Msikilize kidogo basi ....

Mzee huyu pamoja na mapungufu yake nakiri ni miongoni mwa viongozi wachache Afrika ambao unaweza kujivunia bila ya kuwa na wasiwasi sana.
Viongozi wengi waliohai watuendesheao hizi nchi zetu za Afrika , mara nyingine , wanajaribu kunifanya nitafute tafsiri nyingine ya wafanyayo.Kwa sababu asilimia ya hawa viongozi , hawatuongozi, wanachofanya kinahitaji tafsiri yake mpya!
Swali:
kama kiongozi anaongoza, unafikiri Viongozi wetu Afrika wanafanya haibridi gani ya uongozi?


Samahani kidogo!
Siku imenikumbusha kautani Chriss Rock alikowahi kusema kuhusu Mandela.
Hebu kasikilize.....

DUH!
Happy Birthday Mandela!

Read more...

Kigugumizi!

>> Tuesday, July 17, 2007

Kuongea ni kitukigumu na sio rahisi kama tunavyofikiria.

Kabla sijasema jambo hili , ngojea tujifunze kucheza Zouk kwanza....

Kama unaamini katika theories za Darwin za jinsi binadamu alivyotokea na kuvuka unyani, utagundua jinsi gani ilivyokuwa ngumu kwa wanyama wengine kuongea kama binadamu.

Lakini ....
Ukifuatilia anatomi ya wanyama waliokaribu na binadamu,hasa katika genes kama chimpanzii, utagundua jinsi gani binadamu uwezo wake wa kuongea ulimhatarisha sana kujipalia , kwa mate hata kwa kula.
Tuache baoloji basi, AU?
Samahani , nilisahau kuwa nakumbuka kuwa unaamini kuwa umeumbwa na Mungu.

Nachojaribu kusema ni kuwa, ingawa mwili mzima wa binadamu unaongea ukitaka kuwakilisha ujumbe, sauti na kupanga maneno yana saidia sana.
Halafu, kama maneno unayajua lakini huwezi kuyasema, ni kasheshe.
Si utani!Sisi binadamu hatuhesabu baraka tulizonazo.
Swali:
Hivi kama wewe unaweza kuongea na kutoa sauti, ushawahi kujiuliza inakuaje kushindwa kuongea?
Au unalalamika tu kuwa hujui Kichina?


Mcheki basi mshikaji hapa akitaka kumtajia mtu jina lake...


Tukiachana na kigugumizi cha sauti....
Unakumbuka kuwa kigugumizi kiko kwenye vitendo pia. Kimetuathiri tunashindwa kufanya matendo fulani yanayochelewesha kufikia hatua fulani na kutimiza mambo fulani.
Duh!
Lakini inasemekana kigugumizi cha kuongea kimetafutiwa dawa, ingawa mshikaji mmoja mwenye tatizo la kigugumizi cha kuongea, nimjuaye haijafanyakazi, ingawa kalipia kama £6000(Za Uingereza) , ilikutatua tatizo.

Sasa , angalau kuna watu wanaweza kuwa na pesa hizi , jiulize kwa mlalahoi ashindwaye kuongea kutokana na kigugumizi, ashindwaye kupata kazi kutokana na kigugumizi, hata kama kunamatibabu, anaujanjaa kama bei za matibabu ndio hizi?

Niliongea namdau mmoja akaniambia kuwa, kama ni magonjwa, kuna ukimwi, kama ni matatizo, kuna watu wanakufa njaa.
Hivi ndio tuyaruke matatizo mengine kwasababu kuna ukimwi na njaa?
DUH!

Najiuliza tu!Usitishike!
Hebu cheki hii basi...


Duh!
Chakusikitisha ni kwamba ile video ya mshikaji pale juu aliyekuwa kwenye simu akijaribu kutamka jina lake, inapatikana katika website za Wachekeshaji kama ile ya ebaumsworld
Lakini kama unamjua mtu mwenye tatizo hilo kisawasawa akuhusuyo, utagundua jinsi kagi haichekeshi.

Ndio, najua huwa tunawacheka watu wakianguka, nk. Kitendo ambacho ukigundua kafa alipoanguka roho inakusuta.

  • Lakini nasikitika sana kwamba jamii haikawii kuwafanya watu wenye matatizo kuwa vichekesho.Unaweza kucheka mheshimiwa akijamba kwa bahati mbaya hadharani ingawa unajua kijambo hakina lakuchekesha zaidi ya mategemeo ya kusambaza harufu mbaya.

Duh!
Ngojea niondoe jazba basi!
Kama ulijifunza kucheza Zouk pale juu , wimbo huu sasa,ulioandaliwa na DJ Beleza.

Tuchezee kama hunanoma na baraka ulizo nazo...!
AU?

Read more...

Kikojozi Huyooo.........!

Kuna wenye busara waliosema inachukua kijiji kizima kulea mtoto.
Kwa mtazamo wangu na hali halisi ya mambo siku hizi, maswala ya mtoto wako ni yako, jirani akiingilia inakuwa maswala ya jirani mbaya.AU?

Duh!Kabla sijaendelea kuna hili bezi gitaa la Fanki la Bootsy Collins linanizingua...Hebu lisikilize kipande kifupi basi.....


Swali:
Unakumbuka kusikia kale kawimbo alikokuwa anaimbiwa mtoto anayejikojolea kitandani?
Kale ka KIKOJOZI HUYOO .....na nguo tutazichoma moto....!
Jinsi ya kufundisha watoto, wazazi wengi wanastaili zao binafsi. Wengine huwatisha watoto, wengine huwapiga, kuwadekeza kumo, na hata......kuwakejeli,kuwadhalilisha nk.

Inasemekana pia kuwa, asilimia kubwa ya mafunzo ya mtoto, apewaye sifa yakufunza ni mama katika jamii ya Waafrika. Katika jamii ya Waafrika na Wamarekani weusi, inasemekana kuwa asilimia yakutosha tu ipo ya watoto waliokua na mama tu, kutokana na baba kuingia mtini baada ya kustukia mwanadada ana mimba.Pia jamii hii inasemekana kuongoza kwa kuamini vitisho, hofu hadi kejeli kwa mtoto ni moja ya njia bomba za kufundisha mtoto.

Mimi sikubaliani na hilo.

Juzi juzi tena nikajikuta katika mjadala uliobobea katika kuhalalisha hili kuwa , akina baba na mchezo wao wakutokuwepo nyumbani kwa kisingizio cha kazi, cha kunyoshanyosha miguu au kuwakimbia akina mama wakipata mimba unachangia sana kuondoa maadili ya familia katika familia.

Mimi bado na kaubishi kuwa siye akina baba bado tupo katika mstari wa mbele pia katika kulea watoto.Hapa naamaanisha si kama mleta chakula nyumbani kama zamani ilivyokuwa, bali kama mlezi wa makuzi mazuri ya mtoto akishirikiana na mamaa.
AU naota nini?

Swala hili
la malezi liko sana mawazoni leo.
Usistuke, sina mtoto bado!Siunajua tena uvivu:-)AU?
Lakini nawasifu nyie wote mliobarikiwa kupata watoto na mnawalea vyema ili wawe taifa zuri la kesho.
Swali:
Lakini kuna kaukweli kuwa akina baba sio msaada sana siku hizi katika malezi na makuzi ya mtoto?

Duh!
Katika kale kamjadala nilikokagusia hapo juu , kuna akina baba .... walitajwa sana.Baba yake Tiger Woods , Serena na Venus william,Beyonce wa Destiny Child na Baba yake Lewis Hamilton ambao walikuwa wananukuliwa kuwa ni akina baba Weusi ambao wameonyesha jinsi gani wanaweza kujitolea kwa yote kwaajili ya watoto wao.Wakapata sifa za kuwa ndio hasa wakuigwa. Waliolaumiwa wakawa mpaka Nelson Mandela ambaye mwenyewe alikiri kuwa katika malezi ya famili yake, alifeli.
Siunakumbuka haya ya Baba yake Tiger Woods?..
Jikumbushe basi..


Dondoo:(Kikaoni nilikuwa Muafrika kutoka Afrika peke yangu.Labda ndio maana jina la Nelson Mandela tu lilijitokeza kutoka Afrika)

Lakini.......
Baada ya kunukuliwa hao baadhi ya akina baba hapo, nikajiuliza , hivi kipimo kuwa wewe ni baba mlezi mzuri ni pale tu mwanao aoneshapo mafanikio duniani?

  • Je, haiwezekani wazazi wakawalea watoto vizuri, ila watoto wenyewe wakaanza kivyao na kuharibikiwa mbele ya safari, hivyo kutoonyesha dalili zozote za malezi mazuri?

Mimi binafsi naamini bado hatujaanguka sana katika malezi ya watoto, lakini naamini bidii lazima iongezeke.
AU?
Mpate Lewis Hamilton basi ambaye baba yake anasifiwa sana kwa kumlea na kuhakikisha anafanikiwa kwa aliwezalo.


Siku njema!
Lakini malizia na Ray Charles

Read more...

Maswala ya Utapeli ambayo na fikiri yamepitwa na wakati!

>> Saturday, July 14, 2007

Kuna Hii meseji niliyoipata kwa mara karibu ya mia sasa hivi.,
Kabla sijakusomesha...Ningependa umsikilize kidogo huyu Mkameruni, Richard Bona aki Improvaizi na Bobby Mcferrin
Sikiliza basi.....
AU?

Sasaa...
Pata ile barua nayotumiwa kila siku kuwa nawezakupata milioni fulani....

Hi, How are you doing today? My name is James Adamati I live in London and work in a financial institution here in United Kingdom. There is a potential transaction relating to a dormant account of one of our deceased customers, which I would like us to handle the fund actualization together. Secondly, I hope to relocate and acquire a home for my family with a view to establishing over there. I will be needing your assistance and co-operation in this endeavor. Let me know if I can trust you with the above and more information will be sent to you as quickly as possible.For further details,please contact me through my private email- Respectfully, James Adamati
Duh!
Ngojea basi upate CONCIOUS RAS DEM GWAN!!!!!
Mount Zion Medley
LMS,JAH CURE,BUSHMAN,RAS SHILOH,MORGAN HERITAGE & CAPLETON ndani ya nyumba...



Read more...

Rangi ya Moyo!

Watu kibao wakibaguliwa wanalalamika.
Lakini nahisi kuna watu wanaongelea ubaguzi wakati hawajawahi kubaguliwa.

Nikiongelea uzoefu wangu. Baada ya kubaguliwa na baada ya kubagua.
UBAGUZI HAUNA MPANGO.
Bongo...

....tunamchezo wa kulalamika, halafu..mchezo wakudai sisi ni watu wa amani...halafu kuwa ......nk

Mwisho wa siku , ikiwa kadude fulani, midude fulani haitimiliki, saa nyingine kwasababu ambazo hazihitaji kumlaumu mtu, mara nyingi kwa sababu tunataka kumlaumu mtu, kwasababu hatujui nini tatizo....
BADO HATUTIMILIZI.
Duh!

AU?
Lakini sisemi kuwa kulalamika nishai.Lakini nauhakika kuwa SISI WEUSI NI WABAGUZI NISHAI Kama tu WABAGUZI WENGINE.Najua kuwa unaweza Au HATA HUWEZI KUAMINI.Sisi kabla ya rangi, tushaanza wewe kabila gani, halafu weupe weupe wanapewadili kabla yetu weusi weusi
AU?
Swali:
Unafikiri Ukabila umeisha?
Unafikiria nini ukimuona mhindi yuko bomba ndani ya Tanzania?
Kabla sijauliza......
mpate Bunny Wailer.....


Duh!
Kabla sijasema sana , ngoja niache....

Mpate Sting akupe SURA YA MOYO

Swali :
Hivi roho inarangi gani?
Hivi kwanini nikisema unaroho nyeusi hufikirii kuwa nataka unisimamie Harusi yangu?
Hivi kwenye Harusi wanasimamianaga vipi?

Read more...

Pale Binadamu Wenye Busara, Wafanyapo Mavazi kuwa ni jambo lakuzungumzia!

>> Friday, July 13, 2007

Kama unaamini BIBLIA, ina maana unaamini kuwa
kabla Eva hajala lile tunda, na kumkaribisha kwa mapenzi Adamu ambaye alilishangilia lile tunda...... akina Armani,Gucchi na......Hamdala, Dizaina Zubeda.. .. na wengine watengenezao nguo pale chobisi, wasinge kuwa na kazi.
Duh!
Kabla
sijaongelea vibwaya, hebu tuliakidogo na Sunshine Reggae iliyoletwa na Laid Back



Tukirudi kwenye hoja...


Baada ya Eva na Adamu kufaidi tunda....
Inasemekana, sehemu za siri zikastukiwa. Lakini baada ya hapo , inasemekana ni sehemu za siri tu, kufichwa ndio ilikuwa muhimu.(Hii ni kama unaamini kulikuwa hakuna kiwinta katika bustani ya Eden).

Sasaaa...

Swali:
Hivi hizi suti , bichi koma, nepi na gwagulo ni utamaduni wa nani ?
Si wote tulianzia kuficha sehemu za siri tu?

Samahani lakini....!
Hebu pata picha za wanadamu wenye busara ndani ya nguo...




Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Maswala ya BIKINI.
Hivi ushawahi kufuatilia historia ya Bikini?
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Samahani kwa kuonyesha pale juu mwanadada mwenye busara pale akiinjoi kuwa nusu uchi .Wengine huficha kama mwanadada hapo juu na kuinjoi kubwa kuliko.
Au unabisha?
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Picha hii na Glenn Brock.
Ikionyesha jinsi wadada zetu Wakimasai wapendezapo na Kipara wakati akina kaka zao wakisuka.
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Samahani akina kaka......!
N
ajua pia nasisitunafichaga kama mdau Wakituareg aonyeshavyo hapo juu.

Duh!
Turudi kwenye hoja....

Swali:
Ushastukia kuwa, mavazi na ufichaji, ni vitu binadamu kabunia na kuvihalalisha kutokana na tamaduni na anduche yake iitwayo ubongo imruhusuvyo?
Labda utanibishia!
Usitishike!
Nawaza tu hapa!
Mpate Santana akiwa na Rob Thomas
Wakikupa kile kibao Smooth

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP