Kifo na Biashara ya Majeneza!
>> Tuesday, July 03, 2007
Inasemekana kuwa kila janga kwa mmoja , hunufaisha wengine.
Ukitazama habari kuhusu Afrika , hukawiii kusikia jinsi vifo vinavyo tawala karibu vyombo vyote vya habari.
Kama hivi vyombo vya habari vinaaminika, basi haitashangaza jinsi biashara zihusianazo na vifo zinavyozidi kushamiri Afrika.
Hebu angalia wafanyabiashara wa majeneza wa kabila la Ga huko Ghana wanavyokutengenezea majeneza kutokana na hobi zako, ujuzi wako hata umaharufu wako.
Cheki mwenyewe baadhi ya majeneza hapa.
Ukifa kama unapenda Coca cola utazikwa najeneza hili
Baadhi tu ya majeneza kadhaa kutokana na ukumbukwavyo...
SAHARAN VIBE aliandika zaidi kuhusu hawa jamaa.
Lakini...
Inasemekana huko Malawi biashara ya majeneza ni ya upinzani sana. Na watengeza majeneza wamefikia kuwa na sifa ya kuwa wafanyabiashara wasiopenda mzaa kabisa. Ukitembelea duka la majeneza bila kuwa na nia ya kununua jeneza unaweza kushambuliwa hata kupigwa. Inasemekana wengi wa watengeneza majeneza huuzunika sana wakisikia kuwa makadirio ya watu kufa yanapungua.
Swali:
Ulikuwa unafikiri kila mtu anafurahi watu wasipo kufa kwa wingi?
Duka la Majeneza Malawi
Ila nacho wasifu wafanyabiashara wa Malawi ni kwamba biashara ya majeneza inapopungua ,huwa wanaanza kuuza fanicha nyingine.Naamini huu ubunifu wa kubadili bidhaa kutokana na uwepo wa mahitaji , inafaa kuigwa na wafanya biashara wengi Afrika.
Tatizo linalojitokeza tu, ni jinsi inavyojidhihirisha kuwa kuanzia wafanyabiashara wa majeneza mpaka serikali zetu Afrika ni ngumu sana kubunia nini kinakuja mbeleni.Mara nyingi soko tuna liingia bila yakujua hata kujiuliza kuwa , hivi kama leo ndizi zina hitajika kwa wingi ndio ina maana hata na kesho zitahitajika hivyo?Matokeo yake hatukawii kuzidisha tusivyohitaji na kupungukiwa na tunavyovihitaji.
Duh!
Biashara ya kifo haiishii hapo katika mifano hiyo miwili.
- Chakusikitisha ni ukweli kuwa kifo kipo na baadhi wataendelea kuneemeka wakati wengine wakifa
- Chakusikitisha ni kwamba kutokana na tamaduni , mara nyingi mtu akifa anaweza kugharimu waishio zaidi hata ya jinsi alivyo kuwa hai
- Chakusikitisha ni vigumu kwa watu kujitoa katika mfumo ambao mara nyingine huumiza waliohai na bila ya uhakika kuwa aliyefariki kuwa anafaidika na gharama waliohai walizoingia kufanikisha mazishi ya aliyefariki.
Lakini .....!
Nashindwa kujizuia kugundua kuwa kumbe matatizo huzaa matatuzi.Na binadamu ahangaikiaye kutatua matatizo inasemekana hufanikiwa. Katika hoja ya hii, kifo huzalisha jinsi ya kuingiza pesa.
Sasa kama kifo kinasaidia baadhi ya wafanya biashara kuishi.
Umasikini uliotawala asilimia kubwa ya Waafrika unamfaidisha nani?
Au ndio hawa viongozi wetu nini?
Swali:
Hivi mimi na wewe tunafaidika na umasikini?
Au ndio tuseme umasikini hauna kauhaueni?
Usistuke niko Mawazoni tu!
Baadaye!
Nakuacha na James Brown
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment