Kwa Mtakatifu Ng'ombe, Msalaba, Sanamu na.........
>> Friday, July 27, 2007
Napenda binadamu anavyo tafuta na kupata maana ya maisha , imani....katika karibu kitu chochote.
Uhusiano wa binadamu na Vielelezo kama bendera , sanamu , msalaba nk.... hunionyesha kasiri kamoja ka ubongo wa binadamu ufanyavyo kazi.
- Ukimouona Mkristo aliyebobea aukodoleavyo msalaba...
- Mkatoliki akodoleavyo sanamu ya bikira Maria na.....
- Mmarekani mwanajeshi akodoleavyo bendera ya Marekani....
- Mwanasiasa ya ujamaa akodoleavyo sanamu ya Mwalimu Nyerere...
- Muislamu a.....
Kabla sijaendeleaa...
Hebu tu mcheki kidogo Mtakatifu Ng'ombe basi......ambaye analeta maana ya utakatifu kwa baadhi ya binadamu wenzetu.....
Duh!
Sikatai! Vielelezo hivi vinamaana kwa viwahusuvyo. Vinawajenga katika waaminiyo na kuwaunganisha waaminio. Huletea watu kujiamini, na kuwafanya wengine wajitume zaidi kufikia watakako kufikia.
Misri na Piramidi zao ni miongoni mwa baadhi ya vielelezo ambavyo , baada ya muda vimegeuka maana kutoka kuwa makaburi mpaka alama ya busara na ufundi wa wakale. Alama ya kujivunnia Umisri na hata Uafrika. Pia kuwa ni alama muhimu ya nchi ya Misri.
Picha ya Mandela wakati wa kugombea uhuru Afrika kusini ilikuwa ni kielelezo chakuwapa mori na moyo wapiganaji .
- Kwa hiyo nakubali kabisa kuwa kunavielelezo vingi viwezavyokutumiwa kusaidia watu kufanya vizuri zaidi, watu kufikia wajipangiayo, watu kujiamini nk.
Kwa Tanzania....
-Mbona hatuoni hata Sanamu za akina Filbert Bayi?
Naamini mtu kama yule angekuwa kielelezo kiwapacho matumaini wote watakao kuingia katika riadha.
-Mbona akina Hukwe Zawose, Mzee Nyunyusa hawana vielelezo vyao kama sanamu hata katika anga au nje ya mojawapo ya ofisi za sanaa?Naamini ingekuwa kielelezo kizuri kwa Wanasanaa.
Hivi ni Wanasiasa tu ndio muhimu kujengewa vielelezo hivi?Maana naona ni akina Nyerere , Sokoine nk. ndio tunawakumbuka kwa hilo.
Wengine Je?
Wote tunakubaliana asilimia kubwa ya wanasiasa wetu , wamekuwa si vielelezo vya kujivunia.
Swali:
Unafikiria Watanzania kama binadamu wanatambulika, ikiwa Tanzania inajulikana kwa kuhusianishwa na Mlima Kilimanjaro au mbuga za wanyama tu?
Binadamu , akili zao ,busara zao, uzuri wao viko wapi?
Najua kunamtu atataka kunikumbusha kuwa Watanzania ni watu wa amani na wakarimu.
LAKINI Unauhakika?
Chakusikitisha ni kwamba, bado Afrika kwa ujumla , kielelezo kitambulishacho bara ni matatizo.Njaa,umasikini, magonjwa, uvivu,ujinga na ugumu wa maisha.
Cha ajabu Afrika na watu wake ,hakuna sababu ya maana isababishayo tushindwe kujinasua katika jambo hili.Na ukweli vielelezo vitutambulishavyo hatuhusianinavyo.
Kazi kwetu!
Kwa sababu ni mimi na wewe tunahusika katika kugeuza mambo Afrika.
Sisemi kuwa ni rahisi!
Basi Ngojea Maxi Priest na Beres Hammond watuulize...
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment