Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UNAPOKOSA UHAKIKA KUHUSU MSIMAMO WAKO KWENYE....

>> Monday, July 30, 2007

Kabla sijasema, kuna haka kawimbo ka Eurythmics kanikumbushako ubinadamu . Hebu kasikilize maneno yake....


Sasaaaa......

Msimamo ni kitu cha ajabu sana kwa binadamu.
Inajulikana kabisa kuwa sifa mojawapo kuu ya binadamu ni kutokujua kila kitu.
Tofauti ya binadamu na malaika(kama unaamini kuna malaika)ni kwamba binadamu si malaika.
Binadamu ana sifa zote zimfanyazo asijue na kuwa na uhakika na kesho.
Kwa hiyo ungeweza kuamini kwanini ni kawaida kabisa kwa binadamu kukosa msimamo.
Swali:
Unafikiri utakuwa hai kesho?

Duh!
Cha ajabu binadamu hujihisi mapungufu pale astukiapo hajui kila kitu lakini anahitajika ..

  • Kufanya uamuzi na.....
  • Kufanya kitendo na...
  • Kusema jambo na...
  • Kukaripia jambo na....
  • Kumpiga mtu na....
  • Kula nyama ya nguruwe na...
  • Kutafuta malaya na...
  • Kuokoka na.....
  • Kuslimu na...
  • Ku...........
  • Nk.
Maswali:
  • Unauhakika umuitaye baba ni baba yako?
  • Mtu na ubinadamu wake, anahitaji kweli kujisikia vibaya akistukia kuwa hana uhakika?
  • Unauhakika na unachotaka kufanya baada ya kunisoma?
Duh!
Kuna watu hawana uhakika hata kwenye kitu ambacho hakina sababu kwao kukosa uhakika.Unaweza kumuuliza mara kadhaa mtu baada ya kula na kuweka sahani pembeni kama ameshiba, akaanza kukosa uhakika kuwa ameshiba.

Nahisi wengine hawana uhakika ili wenye uhakika wawahakikishie uhakika. Wengine wana uhakika kwa sababu wengine hawana uhakika. Wasio na uhakika mara nyingi huwa na imani na waonyeshao uhakika hata kama wenye uhakika hawana ujuzi wala cha zaidi kiwasababishiacho kuwa na uhakika.

Swali:
Unafikiri Nyerere alikuwa na Uhakika na ......,siasa ya ujamaa...., na...?
Je ni sahihi kwa binadamu kukosa uhakika na msimamo kwa kisingizio chakutokuwa na uhakika na msimamo?

Duh!
Basi bwana!
Jumatatu njema!
Nakuacha na Vybz Kartel


5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Serina 1:31 pm  

Hua hamna uhakika hadi tendo litendeke na kushuhudiwa... iwe kwenye maisha au kifo...

Simon Kitururu 4:09 pm  

@Serina: Sina uhakika kuwa mtu akifa anauhakika kafa:-)

Prettylyf 1:21 am  

jameni sielewi kiswahili changu kimegonga ukuta,nisaidieni *kicheko*

Simon Kitururu 2:34 am  

@Prettylyf:-)

Anonymous 7:20 pm  

hatuna uhakika kwa kila jambo uhakika tunautoa kwa awtu wengine kwa mfano simon huna uhakika kama blogu yako inavutia watu kwamba watu wanaipenda au la mpaka mwafrika akuambie ndio kidogo unaanza kuwa na kauhakika japo kadogo.hata wanawake warembo wanategemea sana watu wa nje wawaeleze kuhusu uzuri wao ndio waanze kujiamini kwani mwanzoni hawana uhakika wa hilo suala.kaka niishie hapa naweza kuongea mpaka kesho

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP