Dume Zima Linafuatilia Mambo ya Wanawake!LOH!
>> Thursday, July 19, 2007
Swali:
Ushawahi kusutwa?
Kabla sija sema....Ngojea Mr Blue amzungumzie nani hiii.....
Inajulikana kuwa, wanawake na wanaume ni tofauti katika kufikiria maumbile nakadhalika nyingine kadhaa.Wengine wamefikia kufananisha wanaume na mbwa, wanawake na paka.Eti mwanamme anaweza kuwekwa mkononi kwa mbinu zilezile unazoweza kumzingua mbwa. Paka nafikiri unamjua mambo zake!
Duh!
Wengine hutofautisha tu sayari watokazo wanaume na wanawake.Eti wanaume hutoka Mars na Wanawake hutokea Venus. Hii yote ni katika kuonyesha jinsi gani jambo moja linavyoweza kuoneka katika kona mbili tofauti katikajicho la hawa binadamu wenye sehemu za siri tofauti.
Duh!
Swali:
Hivi wale wapendanao wenye sehemu za siri za aina moja inakuwaje vile?
Nikiliacha hilo....
Sasaaa......!
Tatizo linalojitokeza hasa katika jamii nyingi duniani , ni jinsi wanawake na wanaume wanavyotenganishwa na mila na desturi. Kitu kifanyacho ,kujuana kwa mwanamume na mwanamke kuwa sayansi ngumu sana.
Ni kawaida kabisa katika mila nyingi, mwanaume kukatazwa kusikiliza, kukaa na mwanamke ......, kuingia jikoni na mwanamke ndio kabisaaaa noma! Jikoni kunakuwa ni kwa wanawake, maongezi ya wanawake yanakuwa ni ya wanawake na kwa mwanamume si yakutilia maanani.Maongezi ya wanaume yanakuwa hayamuhusu sana mwanamke, hasa yakiwa hayahusiani na sentensi zimtakazo mwanamke kuleta chakula au kuja kidogo chumbani kwa dakika kadhaa za chapuchapu katika ku......
Ni kawaida kabisa kwa wanaume kukua bila kujua mambo yamuhusuyo mwanamke.Hata kuona chupi za kike kwa mwanamume ni nadra kwenye jamii nyingi.Kama mtu hana Televisheni, nafikiri yale maswala ya nyenzo mwanamke azitumiazo akiwa mwezini, yanakuwa kitendawili kwa mwanamume. Usisahau swala la kujua kuwa mwanamke huwa anasafiri kwenda mwezini kila mwezi ndio kabisaa halijulikani mpaka baadaye pale anapo.........
Mwanake yeye pia anakuwa anabunia yamhusuyo mwanamme, kwa kufananisha amjuavyo kaka , baba, na wale ndugu fulani wachache wafikao nyumbani, kisimani au pale... na yule mwanakaka ampendaye au aliyelazimishwa kuwa naye .Kumbuka!Mahusiano ya mwanadada na kaka,baba au ndugu ,hayagusishi sehemu fulani ya mahusiano yake na atakayeishi naye kama mpenzi,hawala, au yule tu aliyelazimika kuishi naye.
Tukiachana na maswala hayo...
Narudi katika swala lakujuana kwa mwanamke na mwanamume kifikira na kiutu.
Hili swala pamoja na mila na desturi kuchangia kuzoofisha majuano yake, naamini imefikia wakati wanamume na wanawake wenyewe kwa uhuru wao , bila kisingizio kingine, wanazidisha kudhoofisha ujuanaji huu wa jinsia hizi mbili zitamanianazo.
Ni kawaida kabisa kwa wanaume kusisitiza kuwa ; achana na hayo mambo ya wanawake wewe!
Au kumsikia mwanamke akiuliza; haya mambo yetu wanawake, wewe mwanamume unatafuta nini huku?
Najua mila na desturi na baoloji ya viumbe hawa wawili , hulazimisha mara nyingine ka-ukweli kasababishako , mwanaume aone maswala ya wanawake yanaboa, na mwanamke aone wanaume wanaongea ujinga pale kijiweni.
Swali:
Hivi ni kweli kuwa mawasiliano zaidi kati ya jinsia hizi mbili hayana umuhimu unaohitaji kuongeza mazungumzo na elimu ya kujuana kwa njia ya kuruhusu mabadilishano ya mitazamo na mawazo.......kati ya jinsia hizi mbili?
Kumbuka!
Hapa sijaribu kusema wanawake wasiwe na mambo yao au wanaume wasiwe na mambo yao binafsi.
Nakubali baadhi ya dini na watu wafuatao dini fulani , wao hawaruhusu mchanganyiko wa jinsia hizi mbili.Wao wanamafundisho yao kutoka vitabu fulani vitukufu ,viwapavyo maelezo ya jinsi ya kuwaweka hawa binadamu wawili wenye jinsia tofauti ndani ya ndoa wakaishi kwa amani furaha na upendo.
(Kumbuka!
Hapa naongelea umuhimu wakuongeza mawasiliano kati ya wanawake na wanaume, kwa maongezi....na si lazima kwa kuwakutanisha hawa binadamu wenye sehemu za siri tofauti uso kwa uso.)
Hivyo hapa nawalenga zaidi wale akina sisi ambao bado hatuja pata bahati ya kufungwa na maadili ya vitabu fulani.
Duh!
Nachojaribu kusema, ni kwamba....
- Katika jamii inayotegemea wanaume na wanawake waishi kama mume na mke ndani ya nyumba, hainabudi hawa wanaume na wanawake wajuane vizuri . Na moja la jambo lisababishalo baadhi ya matatizo ndani ya maisha ya wapendanao wawili ndani ya uhusiano , ni kutoelewana kwa dhati kati ya mwanamke na mwanamume mapema katika maisha na pia ndani ya maisha.Hasa kutokana nakuwa na mawasiliano haba na yakwepayo mambo fulani muhimu yahusuyo binadamu hawa wenye jinsia hizi mbili tofauti (Samahani kidogo wasenge na wa saganaji hapa!)
- Nashukuru siku hizi kuna akina Dada kama DINAH wa DINAHICIOUS ambao hawana woga wakujadili maswala ya mapenzi , mahusiano na mengine mengi , kwa undani kwa kutoa mtazamo wa mwanamke katika maswala...., na kutoa baadhi ya mwanga kuhusu jinsi mwanamke afikiriavyo maswala haya.
- Nasikitika kuwa kwa upande wa kina kaka, maswala ya mahusiano ya watu wa jinsia ...., tuyawekeayo umuhimu, sio swala zima la uhusiano.Mara nyingi hata tukiwatunaandika au kutafuta maswala ya mahusiano, tunajali kuweka au kutafuta picha na video za ngono ,zichocheazo mshawasha wa kufanya nanihii, lakini sio kumfunza mtu, yaambatanayo na kufanya nanihii na mahusiano ya wana jinsia hizi mbili kwa ujumla.
Swali:
Hivi hili swala la usawa wa wanaume na wanawake linawezekana kweli ?
Sasaa.......
Swala la nitakupenda mpakakufa na ndoa hii ni mpaka tufe, wote tunajua ni la busara sana.
Kusema ukweli linapendeza na ni tamu masikioni.
Swali:
Hivi unahisi watu wangapi katika ndoa wanapendana mpaka kufa na ndoa yao inadumu mpaka kufa?
Hivi ndoa kufa ni pale tu wanamahusiano wanapo saini karatasi kuwa wameachana?
Mpate D'Angelo basi...
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Hupatikani kwa simu upo RAS? au SWEDEN? Nauliza pligrimage ya pori mwaka huu ipo j pili ziggy kiwanjani kama ni mwendaji text us
@Aliko:Nimeshafanya yearly piligrimeji ya Pori Jazz.jumapili niko na ubize fulani.Lakini najua mtainjoi.
Post a Comment