Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ASANTENI WOTE KWA KURA ZENU!

>> Tuesday, July 03, 2007


Asanteni kwa wote walionipigia kura.Naahidi kuwakilisha wanablogu Tanzania (JUMUWATA), kama katibu, kwa uwezo wangu wote.

Na ahidi kushirikiana na viongozi wenzangu wa jumuiya na wanablogu wote kujenga jumuiya hii iwe ya manufaa na ya kujivunia.

Kabla ya kusema mengi naamini mtapata kusikia hivi karibuni mwelekeo wa jumuiya kutoka kwetu.

Asanteni sana!
Tuko pamoja!
IDUMU JUMUWATA!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 2:45 pm  

Ndugu yetu Simon hongera saaana kwa kuchaguliwa kuwa katibu wa Jumuwata, tuna imani utautumia vizuri ukatibu wako ipasavyo na kwa kusherekea vizuri karibu nyumbani kwangu siku ya j´mosi 7july saa tisa mchana bila kukosa.Ronaldo

luihamu 6:32 pm  

Mzee Simon.Rastafarina inakupa hongera.nakutakia mafanikio mema ndani na nje ya jumuwata.


jah live.

Simon Kitururu 3:30 am  

@Ronaldo: Nitajitahidi kufika. Mzee Ronaldo ,najua hicho kikao cha .. si chakumisi. Mtu hawezi kumisi birthday ya Mzee wa London.Mimi nimebanwa kidogo.Lakini nitatanua na kudondokea hapo bila shaka.
@Rasta:Asante!
JUMUWATA inakuja.Ingawa karibu wote tuliogombea, na kuchaguliwa, anga hii tumebanwa kidogo na maswala. Ila wote tunahakikisha maswala yanaenda na tunayaweka sawa. Hata katika kipindi hiki ambacho zile kamati uzitakazo bado hazijaundwa.Halafu, nnisikufiche, tunahakikisha na tutahakikisha maswala ya JUMUWATA yanaenda kisawasawa.Kama unanielewa , utaelewa kwanini ni muhimu kuwa tunachukua ka muda fulani kuandaa. Kwa uzoefu wako mpaka sasa, naamini utaelewa si kwanini kuwa, ukienda haraka maana yake utafika chobisi.Nataka kusema vuta kasubira kidogo!Kumbuka ni timu na sio mtu mmoja anayesukuma JUMUWAT. Na kama ni timu inabidi mambo yafanyike ki timu. Kumbuka kila mtu katika timu hachezei mguu wa kulia.AU?

Unknown 2:46 am  

Simon nakupa hongera.nakutakia mafanikio mema ndani na nje ya jumuwata.

mungu ibariki Tanzania.

AFRICAN LIZ 10:17 pm  

Congrats for having been elected as the first JUMUWATA Katibu. JUMUWATA is a noble initiative and hereby wishing all the best to the JUMUWATA crew and patrons.
Liz

Simon Kitururu 9:10 am  

@Gerald
@Liz
Asanteni Wote!
Halafu nisiwafiche, Blogu zenu wote wawili nahisi ni miongoni mwa blogu zinazotakiwa kujulikana na kutembelewa zaidi ya sasa zinavyotembelewa. Lakini mimi niko hapo kila siku.Duh! Sasa nifanyeje wakati zimebobea katika shughuli na mabo babu kubwa:-)

Tuko pamoja!

Anonymous 3:14 pm  

Nimechelewa kukupa hongera lakini haikuwa dhamira yangu. Hongera kwa kuchaguliwa katibu Simon.

Simon Kitururu 4:02 pm  

@Serina:Asante!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP