Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mambo ya Kufananishwa ......

>> Saturday, July 28, 2007

Duniani kuna watu wanaamini kuwa Wachina wote wanafanana!
Watu weusi wote wanafana!

Nakumbuka kipindi cha miaka ya tisini, ukiwa mweusi ukakatiza nchi kama Finland, watu wanakuwa na uhakika kuwa wewe ni Msomali , halafu mkimbizi. Walikuwa hawawezi kutofautisha watu weusi. Na kutokana na uchumi wao miaka hiyo kuwa mbaya, basi hukawii kutupiwa jicho la chuki kuwa umekuja kuwaongezea shida.
Sasa hivi ukiwa unamandevu ,ukafananishwa na Bin Laden fulani,ukikatiza Airport hukawii kuitwa pembeni wakakucheki zaidi mizigo yako.

Swala la kufananishwa lina mambo yake....

Ngojea nikupe kastori kalikonitokea jana......


Nanukuu nilichoombwa jana....
`Sorry Brother!, I am desperetely in need of Ur help! I see U in this joint often and I am interested in a girl who is into Tracy chapman. I think U.......´

Ngojea nirudi kwenye kilugha........


Jana kuna mtu(hata simkumbuki jina) alikuwa anampa kauli mwanadada mmoja, ilikujiongezea pointi akaamua kumdanganya kuwa yuko na mimi, halafu eti mimi ni mdogo wa Tracy Chapman,nimekuja kumtembelea.Ilibidi niwe naitikia chochote asemacho kuhusu uhusiano wangu na wake na wangu na Tracy Chapman.Kwa bahati nzuri naijua historia ya Tracy, hivyo maswali fulani kuhusu yeye nilitoa majibu.
Hebu cheki picha zangu na Tracy.....

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Tracy Chapman(picha na Steve Granitz/WireImage.com)
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mimi
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mimi
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Tracy(Picha na David Atlas)
Duh!
Je tumefanana?

Ngoja nigusie na....
Kipindi nilichokuwa Tanzania, kuna watu walikuwa wanakuja kunisalimia wakifikiri mimi ni
Q Chifu.
Sasa naanza kuogopa kwa maana siku moja mtu atanifananisha na kibaka aliyemuibia ,halafu nitakula mkong'oto.

Kuhusu jana chakusikitisha ni kwamba ....nilikubali kufanya maigizo. Na si utani , aliyeambiwa hakujali hata kiswanglish changu, aliamini kabisa anachoambiwa kuhusu undugu wangu na Tracy.
Nasikitika kwa kusapoti uongo , lakini ilikuwa ni kaigizo fulani kanakochekesha na kaliniondolea ka-boredom fulani na.............vilevile kalinifikirisha.

  • Chakusikitisha ni kwamba kuna watu wanaweza wakakubali kufanya chochote wakihisi wewe ni mtu Maarufu.
Cha ajabu kumbe hata ukifanana na mtu fulani maarufu , unaweza kupata pointi anga fulani.

Lakini...

Watu maarufu , wanapata raha na pia kusulubiwa kwa kujulikana kwao.
Ukiniuliza mimi , naweza kusema , wale wa karibu na watu maarufu, au wenye kujuana na watu maarufu , mara nyingine ndio wafaidio kuliko hata wale watu maarufu wenyewe.

Kuna mshikaji wangu alitaka kujua kama ningependa kuwa katika nafasi ya Mandela!
Wote tunajua kuwa Mandela ni mtu maarufu, na aheshimikaye sana duniani.Lakini mimi nitakuambia, hata siku moja huwezi kunifanya nitamani kupitia na kuishi aishivyo yeye.Mzee kama yule hana nafasi hata ndogo ya kukosea. Siku akisikika katukana au kapitia mtaa gani sijui, dunia nzima itasimuliana hicho kitu. Na hadithi nyingine kemukemu zitazaliwa za kumpaka matope.
Lakini ukiniuliza kama nataka kuwa rafiki yake, hapo tutaelewana.

Nikirudi kwenye hoja.......

Tatizo ni moja tu!
Huwezi kuchagua nani utafanananaye. Kirahisi tu, unaweza kufananishwa na kibaka fulani.
Ushawahi kusikia kuwa mara nyingi mtu na mke wake hufanana?
Swali:
Kwanini watu huchukia kufananishwa na mtu nishai?
Mbona hatujiulizi ,hivi ni kibaka anafanana na mimi au ni mimi nayefanana na kibaka?
(Unajuatena yale maswala ya kuangalia glasi ya maji na kuiona imejaa nusu na sio imepungua nusu.)
Ee bwana ee Jumamosi njema!


Mpate basi Tracy Chapman na BB King


Najua leo ni Helsinki Vs Tampere kwenye mpira wa miguu!Samahani Ezza , nilipitiliza.Si unajua nilijidanganya kuwa ngoja nilale kidooogo.....Nilipoamka nimechelewa nikajua mchuma utakua umeshaondoka.

12 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 1:41 am  

huku algeria waarabu wanaamini waafrika wote tunafanana unaweza kutembea na passport au kitambulisho cha mwenzako.ila huyo dada umefanana nae sana

Anonymous 7:25 am  

Ndio maana tukaitwa Bin Adam (BINADAM)sio vibaya kufanana lakini ukifanana na kibaka ni soo

Anonymous 8:19 am  

SUPERB SITE!

Simon Kitururu 3:03 pm  

@Mwafrika:Nilikuwa sijui kwamba hata Waarabu wanaona Watu weusi kuwa wamefanana:-) Duh!
@Anony:Kweli kabisa , wote ni binadamu, lakini naamini kila mtu yuko kivyake ingawatunaunganishwa na ubinadamu.
@Kifimbocheza:Asante Mkuu!Karibu kijiwenin!

Egidio Ndabagoye 3:22 pm  

Tracy mmefanana nae sana.Wewe si matawi ya juu yule dada anakujua sasa.Inawezekana yule dada akakutafuta kaka zali hilo!

Tatizo ni pale unapofananishwa na mtu mwenye silka mbaya hapo ndio ugomvi unatokea

luihamu 3:42 pm  

Katibu sawa mkuu.
Katibu ninapata shida sana wakati wakusoma blogu yako Katibu,naomba ucheki hizo rangi tena Katibu.
Umecheki blogu ya Miriam?Moto wakuotea mbali.

Nuff,Nuff respect

Simon Kitururu 3:57 pm  

@Rasta: Kwangu inasomeka. Lakini blogu yangu iko katika matengenezo!Itabadilika sio muda mrefu.Naadha kujihisi kuwa nina Matatizo ya kuona rangi kinamna fulani.(Colour blindness)

luihamu 6:17 pm  

Mzee,Katibu Simon
Mzee Ndesanjo alianza
Babukadja Sankofa akafuata
Rasta nae kaandika leo

KISA CHA STELLA,MZEE Simon upo hapo?Tunasubiri kwa hamu.

Kwawale amboa ni wasichana na wangependa kushiriki itabidi tutunge jina moja la kiume nao watupe za kwao.

Simon Kitururu 7:16 pm  

@Rasta:Story ya Stella wangu inakuja:-)

Anonymous 7:29 pm  

Kitururu, mambo ya kufanana ni magumu, kweli. Kulikuwa na mtu mmoja maarufu hapa Dar, ambaye alipendwa na watu wengi, lakini pia alichukiwa na wengi pia. Hivi karibuni, aliingia mitini, haonekani kabisa.

Sasa, kuna watu ambao wanasema mimi na huyo tunafanana sana mpaka basi. Sasa mashabiki wake ambao walimpenda sana, hawataki kusikia hata jina lake. Na maadui wake wapo juu kama mkungu wa ndizi siku hizi.

Nifanyeje kaka?

Simon Kitururu 7:41 pm  

@kifimbocheza: Duh!Hapo unakasheshe!Usije ukapigwa tu kona fulani, wanaomchukia jamaa wakidhania wewe ndio yeye.

Anonymous 7:52 pm  

Ndiyo hofu yangu katibu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP