Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Pale Binadamu Wenye Busara, Wafanyapo Mavazi kuwa ni jambo lakuzungumzia!

>> Friday, July 13, 2007

Kama unaamini BIBLIA, ina maana unaamini kuwa
kabla Eva hajala lile tunda, na kumkaribisha kwa mapenzi Adamu ambaye alilishangilia lile tunda...... akina Armani,Gucchi na......Hamdala, Dizaina Zubeda.. .. na wengine watengenezao nguo pale chobisi, wasinge kuwa na kazi.
Duh!
Kabla
sijaongelea vibwaya, hebu tuliakidogo na Sunshine Reggae iliyoletwa na Laid Back



Tukirudi kwenye hoja...


Baada ya Eva na Adamu kufaidi tunda....
Inasemekana, sehemu za siri zikastukiwa. Lakini baada ya hapo , inasemekana ni sehemu za siri tu, kufichwa ndio ilikuwa muhimu.(Hii ni kama unaamini kulikuwa hakuna kiwinta katika bustani ya Eden).

Sasaaa...

Swali:
Hivi hizi suti , bichi koma, nepi na gwagulo ni utamaduni wa nani ?
Si wote tulianzia kuficha sehemu za siri tu?

Samahani lakini....!
Hebu pata picha za wanadamu wenye busara ndani ya nguo...




Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Maswala ya BIKINI.
Hivi ushawahi kufuatilia historia ya Bikini?
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Samahani kwa kuonyesha pale juu mwanadada mwenye busara pale akiinjoi kuwa nusu uchi .Wengine huficha kama mwanadada hapo juu na kuinjoi kubwa kuliko.
Au unabisha?
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Picha hii na Glenn Brock.
Ikionyesha jinsi wadada zetu Wakimasai wapendezapo na Kipara wakati akina kaka zao wakisuka.
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Samahani akina kaka......!
N
ajua pia nasisitunafichaga kama mdau Wakituareg aonyeshavyo hapo juu.

Duh!
Turudi kwenye hoja....

Swali:
Ushastukia kuwa, mavazi na ufichaji, ni vitu binadamu kabunia na kuvihalalisha kutokana na tamaduni na anduche yake iitwayo ubongo imruhusuvyo?
Labda utanibishia!
Usitishike!
Nawaza tu hapa!
Mpate Santana akiwa na Rob Thomas
Wakikupa kile kibao Smooth

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

mwandani 5:07 pm  

kuna mavazi mengine ni ya kusingizia tu hakuna yanachositiri. Sasa hivyo vijinyuzi vyeupe vinasitiri nini?

luihamu 6:53 pm  

This is what i have been trying to blog about(unajuwa Mzee Katibu Simon wakati mwingine ni vizuri kutumia hii lugha ili kuonyesha msisitizo)

Kidada zetu wanaiga,unajuwa kuiga kuna mambo mengi sana,kwanza unae mwiga haujui kipato chake,anafanya nini na nikwanini anafanya ivo.

Mimi na wewe hali yetu ndio kama hivyo then tunaiga duh.

Mzee Katibu,katika picha yako hapo juu naona kunakitu kimoja kinamiss AU

Simon Kitururu 7:02 pm  

@Mwandani na Rasta: Haya maswal ya mavazi na kujisitiri, acha tu!
@Rasta Nini hicho kina misi?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP