Kigugumizi!
>> Tuesday, July 17, 2007
Kuongea ni kitukigumu na sio rahisi kama tunavyofikiria.
Kabla sijasema jambo hili , ngojea tujifunze kucheza Zouk kwanza....
Kama unaamini katika theories za Darwin za jinsi binadamu alivyotokea na kuvuka unyani, utagundua jinsi gani ilivyokuwa ngumu kwa wanyama wengine kuongea kama binadamu.
Lakini ....
Ukifuatilia anatomi ya wanyama waliokaribu na binadamu,hasa katika genes kama chimpanzii, utagundua jinsi gani binadamu uwezo wake wa kuongea ulimhatarisha sana kujipalia , kwa mate hata kwa kula.
Tuache baoloji basi, AU?
Samahani , nilisahau kuwa nakumbuka kuwa unaamini kuwa umeumbwa na Mungu.
Nachojaribu kusema ni kuwa, ingawa mwili mzima wa binadamu unaongea ukitaka kuwakilisha ujumbe, sauti na kupanga maneno yana saidia sana.
Halafu, kama maneno unayajua lakini huwezi kuyasema, ni kasheshe.
Si utani!Sisi binadamu hatuhesabu baraka tulizonazo.
Swali:
Hivi kama wewe unaweza kuongea na kutoa sauti, ushawahi kujiuliza inakuaje kushindwa kuongea? Au unalalamika tu kuwa hujui Kichina?
Mcheki basi mshikaji hapa akitaka kumtajia mtu jina lake...
Tukiachana na kigugumizi cha sauti....
Unakumbuka kuwa kigugumizi kiko kwenye vitendo pia. Kimetuathiri tunashindwa kufanya matendo fulani yanayochelewesha kufikia hatua fulani na kutimiza mambo fulani.
Duh!
Lakini inasemekana kigugumizi cha kuongea kimetafutiwa dawa, ingawa mshikaji mmoja mwenye tatizo la kigugumizi cha kuongea, nimjuaye haijafanyakazi, ingawa kalipia kama £6000(Za Uingereza) , ilikutatua tatizo.
Sasa , angalau kuna watu wanaweza kuwa na pesa hizi , jiulize kwa mlalahoi ashindwaye kuongea kutokana na kigugumizi, ashindwaye kupata kazi kutokana na kigugumizi, hata kama kunamatibabu, anaujanjaa kama bei za matibabu ndio hizi?
Niliongea namdau mmoja akaniambia kuwa, kama ni magonjwa, kuna ukimwi, kama ni matatizo, kuna watu wanakufa njaa.
Hivi ndio tuyaruke matatizo mengine kwasababu kuna ukimwi na njaa?
DUH!
Najiuliza tu!Usitishike!
Hebu cheki hii basi...
Duh!
Chakusikitisha ni kwamba ile video ya mshikaji pale juu aliyekuwa kwenye simu akijaribu kutamka jina lake, inapatikana katika website za Wachekeshaji kama ile ya ebaumsworld
Lakini kama unamjua mtu mwenye tatizo hilo kisawasawa akuhusuyo, utagundua jinsi kagi haichekeshi.
Ndio, najua huwa tunawacheka watu wakianguka, nk. Kitendo ambacho ukigundua kafa alipoanguka roho inakusuta.
- Lakini nasikitika sana kwamba jamii haikawii kuwafanya watu wenye matatizo kuwa vichekesho.Unaweza kucheka mheshimiwa akijamba kwa bahati mbaya hadharani ingawa unajua kijambo hakina lakuchekesha zaidi ya mategemeo ya kusambaza harufu mbaya.
Duh!
Ngojea niondoe jazba basi!
Kama ulijifunza kucheza Zouk pale juu , wimbo huu sasa,ulioandaliwa na DJ Beleza.
Tuchezee kama hunanoma na baraka ulizo nazo...!
AU?
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kwanza , samahani juu kiswahikli changu sio kisafi kama chako. Lakini mimi hupenda sana Zouk and I would really like to learn how dnace it well.Thanks for that Link..
Kwanza , samahani juu kiswahikli changu sio kisafi kama chako. Lakini mimi hupenda sana Zouk and I would really like to learn how dnace it well.Thanks for that Link..
Bila samahani !Karibu Irena!Click the video it will take U to youtube where U can find more clips.
Post a Comment