WaAfrika Wagombanapo kuhusu Mipaka ya Nchi Zao!
>> Friday, July 06, 2007
Inasikitisha kuwa sisi Waafrika bado tunagombana kuhusu mipaka ya nchi.
- Hivi, si ni wakoloni walikaa pale Ujerumani wakagawana bara la Afrika?
- Hivi si ni sisi Waafrika tunatakiwa kujua baada ya miaka yote hii , na busara zetu hizi, kuwa hawa jamaa waliotugawa kwa mipaka na tamaduni, na wanaoendelea kutugawa, kua wao wanaungana?Au zile EU na... bado hatuzielewi?
Samahani......
Ila Mimi kama Mtanzania, na marafiki wengi Wakenya kuliko Watanzania katika chobisi niliyopo.
Mimi kama Mtanzania na marafiki WaTanzania kama akina Ogola ambao wameishi Tanzania nakusoma Kenya kwasababu shule ya karibu ilikuwa Kenya.
Mimi kama .........
Duh!
Swali:
Hivi sisi kama Waafrika, mipaka ni kitu kitusumbuacho zaidi ya matatizo mengine mengi, ambayo ndio sura ya unyonge wa Muafrika mweusi?
Samahani, hebu msikilize huyu Mpiga Rege (Innocent Galinoma) Mtanzania ambaye baadhi ya watu wana msahau ingawa yuko katika anga tokea enzi zileeeeeeeeeeeee.....!
Sasaaa............
Mpaka leo .......
- Tanzania na Malawi , wanagombania mpaka umepita wapi katika ziwa Nyasa(Malawi).
- Hivi , Wamasai na Waluo (Wajaluo)ni Wakenya na Watanzania ?Au kwasababu wako nchi zote , hawahitaji passport?
Duh!
Samahani niko mawazoni tu!
Kabla sija kuacha, ngojea nikuache na picha zangu leo...
Tulia basi na Sekouba Bambino
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Bwana Kitururu, haya mambo ya mipaka ni akili mbovu tu za baadhi yetu waafrika.Kufikiri kwetu si kupana, tuna upeo mdogo miongoni mwetu ndio maana unaona matatizo kila kukicha.
Pia bado tunawaza kikoloni ingawa tunadai tuko huru, ndio maana hata mipaka tuliyoachiwa na wazungu tunaitilia maanani sana.
Tunahitaji fikra mpya.
@Inno:Siutani Mzee!Lakini kubadili mawazo imepruvu kuwa ngumu kweli. Lakini lazima maswala haya tujadili
Post a Comment