Kikojozi Huyooo.........!
>> Tuesday, July 17, 2007
Kuna wenye busara waliosema inachukua kijiji kizima kulea mtoto.
Kwa mtazamo wangu na hali halisi ya mambo siku hizi, maswala ya mtoto wako ni yako, jirani akiingilia inakuwa maswala ya jirani mbaya.AU?
Duh!Kabla sijaendelea kuna hili bezi gitaa la Fanki la Bootsy Collins linanizingua...Hebu lisikilize kipande kifupi basi.....
Swali:
Unakumbuka kusikia kale kawimbo alikokuwa anaimbiwa mtoto anayejikojolea kitandani?
Kale ka KIKOJOZI HUYOO .....na nguo tutazichoma moto....!
Jinsi ya kufundisha watoto, wazazi wengi wanastaili zao binafsi. Wengine huwatisha watoto, wengine huwapiga, kuwadekeza kumo, na hata......kuwakejeli,kuwadhalilisha nk.
Inasemekana pia kuwa, asilimia kubwa ya mafunzo ya mtoto, apewaye sifa yakufunza ni mama katika jamii ya Waafrika. Katika jamii ya Waafrika na Wamarekani weusi, inasemekana kuwa asilimia yakutosha tu ipo ya watoto waliokua na mama tu, kutokana na baba kuingia mtini baada ya kustukia mwanadada ana mimba.Pia jamii hii inasemekana kuongoza kwa kuamini vitisho, hofu hadi kejeli kwa mtoto ni moja ya njia bomba za kufundisha mtoto.
Mimi sikubaliani na hilo.
Juzi juzi tena nikajikuta katika mjadala uliobobea katika kuhalalisha hili kuwa , akina baba na mchezo wao wakutokuwepo nyumbani kwa kisingizio cha kazi, cha kunyoshanyosha miguu au kuwakimbia akina mama wakipata mimba unachangia sana kuondoa maadili ya familia katika familia.
Mimi bado na kaubishi kuwa siye akina baba bado tupo katika mstari wa mbele pia katika kulea watoto.Hapa naamaanisha si kama mleta chakula nyumbani kama zamani ilivyokuwa, bali kama mlezi wa makuzi mazuri ya mtoto akishirikiana na mamaa.
AU naota nini?
Swala hili la malezi liko sana mawazoni leo.
Usistuke, sina mtoto bado!Siunajua tena uvivu:-)AU?
Lakini nawasifu nyie wote mliobarikiwa kupata watoto na mnawalea vyema ili wawe taifa zuri la kesho.
Swali:
Lakini kuna kaukweli kuwa akina baba sio msaada sana siku hizi katika malezi na makuzi ya mtoto?
Duh!
Katika kale kamjadala nilikokagusia hapo juu , kuna akina baba .... walitajwa sana.Baba yake Tiger Woods , Serena na Venus william,Beyonce wa Destiny Child na Baba yake Lewis Hamilton ambao walikuwa wananukuliwa kuwa ni akina baba Weusi ambao wameonyesha jinsi gani wanaweza kujitolea kwa yote kwaajili ya watoto wao.Wakapata sifa za kuwa ndio hasa wakuigwa. Waliolaumiwa wakawa mpaka Nelson Mandela ambaye mwenyewe alikiri kuwa katika malezi ya famili yake, alifeli.
Siunakumbuka haya ya Baba yake Tiger Woods?..
Jikumbushe basi..
Dondoo:(Kikaoni nilikuwa Muafrika kutoka Afrika peke yangu.Labda ndio maana jina la Nelson Mandela tu lilijitokeza kutoka Afrika)
Lakini.......
Baada ya kunukuliwa hao baadhi ya akina baba hapo, nikajiuliza , hivi kipimo kuwa wewe ni baba mlezi mzuri ni pale tu mwanao aoneshapo mafanikio duniani?
- Je, haiwezekani wazazi wakawalea watoto vizuri, ila watoto wenyewe wakaanza kivyao na kuharibikiwa mbele ya safari, hivyo kutoonyesha dalili zozote za malezi mazuri?
Mimi binafsi naamini bado hatujaanguka sana katika malezi ya watoto, lakini naamini bidii lazima iongezeke.
AU?
Mpate Lewis Hamilton basi ambaye baba yake anasifiwa sana kwa kumlea na kuhakikisha anafanikiwa kwa aliwezalo.
Siku njema!
Lakini malizia na Ray Charles
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment