Kwanini nampenda Hausigeli!
>> Tuesday, July 24, 2007
Dunia ni ya ajabu! Pamoja na mengine mengi, kaskazini, kusini, hata mashariki nilikofika, ni kawaida kukuta mwanamke akilipwa mshahara mdogo au akinyanyasika kuliko mwanamume.
Au akilazimika kufanya hata ambayo si lazima.
Lakini ni kawaida kusikia wanadamu wakimsififia MAMA.
Ngojea basi tufyekewe...
(usifikirie nasema mwanadada hapo kwenye kideo hafurahii kazi au kakosea)
Mhhh!
Kamusi kidogo!
Hausi=House
GELI=Girl
Hausigeli=Mwanamke akaaye kwenye nyumba.
AU?
Mnyonge, Mnyongeni, kuna watu wasema!
MIMI NASEMA MNYONGE MPENI NGUVU.
Kabla sijasema.......
Swali:
Unamjua mwanamke akaaye kwenye nyumba?
Mpate Sekouba Bambino
Lakiniii....!
Hausigeli akikataa, kazi kajifukuzisha.
AU?
Yule hausigeli kwa wale walionacho, na afanyaye kazi iliwale mahausi geli na mahausi boi , wengine , wenyejeuri ya kulipa mshahara, walio hata na nyongeza ya watu nyumbani, hunyanyasika.
Sasaaaaa....
Dunia ya sasa, ndio kwanza tumepata mwanamke wa kwanza Rais INDIA.
Dunia ya sasa ndio kwanza , Mrs Clinton anakuwa mwanamke wa kwanza USA kuchukuliwa siriasi kuwa ni mgombea wa Urahisi.
Katika jicho la wanaume katika jamii nyingi , mwanamke ni mzuri halafu anasehemu za siri wanamme watakazo kuzitafutia urafiki na sehemu zao za siri, na zaidi ya kazi za nyumbani, mwanamke hana cha zaidi.
AU unabisha?
Lakini........
Cha ajabu , katika jamii karibu zote wanaheshimu mama.
Na wanajua kuwa mambo mengi muhimu duniani yafanywa na mwanamke.....
Swali:
Hivi MAMA si ni mwanamke?
Mbona Unamheshimu?
(Au wewe huna heshima?)
Cha kusikitisha nikwamba....
Kizazi cha Arap Moi, akina PAPA Benedict ,mimi na wewe, ambao wananguvu za kudhoofisha wanawake, na wa dhoofishao wanawake, ndio bado tunao katika dunia ya sasa idhalilishayo wanawake na kuamini wanaume ni zaidi.
DUH!
Mheshimiwa samahani kama sija kutaja(Zaidi ya Arap na Benedict), kama unauhakika wanawake ni wanyonge.
Lakiniiii..........
Swali:
Ushawahi kufanya mapenzi ya kuibia?
Mapenzi ya siri ni matamu.
Duh!
Nahisi hakuna kitu ambacho ni mapenzi ya siri ambayo hutashikwa.
Nahisi unajua ni mapenzi ya siri kwa sababu unajua utashikwa au kunauwezekano wa kushikwa, halafu hutaki kudakwa.
DUH!
Samahani najua kuwa hausigeli, inamaanisha wanadada walio pewa kazi za nyumbani katika kona fulani,
.....za wenye maisha fulani,
....... hasa katika nchi fulani,
......hawa mahausigeli hutokea sana vijijini , kutokana na matatizo fulani,
.....Lakini ukilitazama hili jambo kwa jicho fulani,
.....na katika maeneo fulani......!
Hawa waliowengi maarufu kama mahausigeli fulani
...Wafanya tu kitu fulani
kwa kuogopa mambo fulani ...
ya....
Ok naaachaa basi kukuzingua!
AU?
Lakiniiii!
Kwa difinisheni yangu ya hausi geli hapo juu waweza kusema ....
MIMI NI HAUSI BOI fulani......
AU?
Kumbuka namzumgumzia mwanadada akaaye kwenye nyumba.....
Kumbuka namzungumzia mwanadada umfanyishaye kazi pale nyumbani........
Kumbuka namzungumzia mwanakaka umfanyishaye kazi pale nyumbani na mwanakaka umuitaye mpenzi.
Duh!
Swali:
- Hivi ni kweli, kwako wewe ninakuchanganya kwa staili yangu yakuongea?Fikiria kidogo utanielewa.
Ngoja nikupatie picha za jana nilipokutana na Bloga maarufu wa Tanzania aitwaye MAGGID Mjengwa.
Maggid Mjengwa
Rupia
Aliko eeh?
Duh!
Tommy eeh?
Mtimkubwa eeh!
Duh!
Mjengwa na Aliko
Rupia na Mjengwa
Kaka Mjengwa na Mimi
Tommy na Mimi
Timu fulani
Timu niliyomisi.
Kabla sijaanza!Namaanisha kabla sijaacha kukuzingua hapa leo......
Nilitaka kukuelezea tu kuwa ingawa kichwa cha habari kiliku....
Nampenda Hausigeli kwa sababu nampenda tu!
Au wewe ulikuwa unafikiria nini?
Lakini mwanadada , wampenda hausi boi?
Kama unasoma hapa Usitishike!
Usipofikiria kinamna, huwezi kunielewa.
Endeleza siku basi.
Siku njema!
Nakuacha na.....Thandiswa Mazwai
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Hii safi sana,hii ninjia moja ipo siku tutakutana wote.
Hausigeli!
Kuna siku nilikuwa nasogoa na swahiba wangu Dennis Londo kuhusu hausigeli. Dennis akaniambia "..Nadhani hausigeli ndiyo ajira ya chini kuliko zote..Unajua mabaamedi pia wana mahausigeli?..Na siyo rahisi kukuta hausigeli ana hausigeli!" Sikumbuki tulihitimisha nini lakini tangu siku hiyo nikaanza kuwazia juu ya uhausigeli.
Palikuwa na kiongozi mmoja wa Afrika ambaye simulizi zinasema Mama yake alikuwa hausigeli kwenye kasri la Mfalme. Mmoja wa ndugu za Mfalme alimpa mimba Mama yake. kwa sababu ya usheha wa Kifalme uhusiano wa ndugu wa Mfalme na Hausigeli hali kadhalika mtoto aliyezaliwa ulidhibitiwa.
Yule mtoto alipokua na kujua historia yake akashikwa na uchungu sana. Pamoja na kuwa usheha wa Kifalme ulimuweka mbali na nduguze wa upande wa Baba lakini ulimpa matunzo ya namna fulani. Yule mtoto alijiunga na jeshi na kupandishwa vyeo. Baadaye alipindua utawala wa Kifalme na kuweka utawala wa kijeshi. Kwa hasira na ghadhabu akamuua Mfalme. Akamchimbia kaburi ndani ya kasri. Juu ya kaburi hilo akajenga choo ambacho alikuwa akikojolea, kunyea, na kutemea mate.
Wakati mwingine hausigeli pia humpindua mama mwenye nyumba na kuchukua umama mwenye nyumba.
Custo, sasa cheza hii rekodi upande wa pili: HAUSIBOI. Hausigeli huwa wanadhalilishwa lakini kuna watoto wengine ukiwaangalia hufanana sura na wajihi wa hausiboi kuliko wa baba mwenye nyumba.
Tafiti zinasema mahausigeli wanaongoza kwamaambukizi ya ukimwi.
1.Hausigeli akiaanza kupendezapendenza tuu mama mwenye nyumba huotesha nyasi ajira fasta fasta,nakubalishwa kuleta hausi boi.
2.Hausigeli anatakiwa atoke shamba aka vijijini na always awe mchafuchafu hivii iliasiwatamanishe mamen ndani ya nyumba, nyumba yenye wanawake wengi basi hausiboi mwiko viseversor
3. kuna familia nyingi tanzania zimewaendeleza sana wafanyakazi wa ndani ikiwa na kuwasomesha, kuwatafutia ajara tofauti nk.
4. hivi huu utamaduni wa mahausi geli umetokoa wapi... UK wajamaika walivyoletewa kutengeneza underground tunnels za metros wakua na swali mmoja wapi HAUSIBOY KOTA? maanke hakuamini kukabidhiwa nyumba zao wenyewe za kuishi
la ajabu siku hizi nchi karibu zote za Ulaya huyu hausi geli hayupo.. ni adimu labda kwa matajiri wachache
5.TUWAHESHIMU HAWA WAFANYAKAZI WA NDANI KWANI WENGI WETU TUMELELEWA NA HAWA WAKATI WAZAZI WANALITUMIKIA TAIFA.
Post a Comment