Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mtoto wa Mwenye Nyumba afananapo na hausiboi!

>> Friday, July 27, 2007

Swali:
Hivi Butler si ni hausiboi?

-Mbona sasa hausi boi akiitwa butler watu wanamchukulia kuwa yeye babu kubwa?
Unamkumbuka butler wa Princess Diana?

Tuache hilo.....
Namsikiliza Erick Wainaina hivi sasa wakati naandika. Kuna wimbo mmoja naupenda jaribu kuusikiliza nyuma ya mahojiano yake hapa....

Nikirudi kwenye hoja.....

Uhausiboi ni kazi fulani watu huidharau Bongo ingawa inampatia mtu kitu kidogo.
Lakini nawakumbuka mahausiboi fulani enzi hizo, wa jirani zangu, ambao karibu sisi wengine wote mtaani tulikuwa tunawaonea wivu.

Pata stori fupi basi....

Enzi hizo, mimi, pamoja na karibu kundi langu lote, tulikuwa ni wanafunzi.Pesa usipopewa na wazazi basi kasheshe. Kulikuwa na jamaa aitwaye Joseph, hausiboi wa Daktari fulani na mwingine Laurent, hausiboi wa Mfanyabiashara tajiri fulani, walikuwa wanatufanyia maswala ambayo kwetu ilikuwa miujiza.Hawa jamaa walikuwa na mshahara halafu watundu. Lililoongeza tatizo na wivu kwetu,ilikuwa ukweli kuwa wengi wetu tulikuwa katika umri fulani ambao ,kwetu wanavulana , kulikuwa hakuna kingine cha maana au kipitiacho akilini zaidi ya mademu. Karibu wake za watu wote mtaani wasiokwenda kazini, hawa jamaa walikuwa wanawaneemesha.Halafu wote wawili walikuwa ni chaguo la mama mwenye nyumba, ambaye alihakikisha wanapata kazi. Moja ya shughuli yao ilikuwa ni kuwa wasafi na kunukia vizuri. Tulikuwa tunakaa karibu na hosteli ya wasichana tupu(Hostel ya Moro Sec).Na kwa kawaida wanafunzi hawana pesa sana kama ijulikanavyo. Hivyo hawa jamaa walikuwa wanatumia fursa hiyo kujichagulia yeyote wamtakaye ambaye anashida na pesa na hanatatizo na kuchukuliwa na hausiboi, na afanyaye watakayo. Walikuwa hawafi njaa ya nanihii! Mpaka leo sijui walikuwa wanafanyaje! Kwasababu hawa jamaa pamoja na uhausiboi ambao ulimuhakikishia baba mwenye nyumba kuwa wanafanyakazi, waliweza kumtosheleza mama mwenye nyumba, na wengine wote watakao mtaani. Baadaye nikaja kugundua pia walikuwa na maumbo ambayo wanadada fulani huyapendelea.Ingawa inasemekana wanadada mtaani walisimuliana pia kuhusu nanihii, hivyo kila mmoja akawa anamaswali ambayo hawajamaa walikuwa tayari kuyajibu kwa vitendo.

Tuachane na hako kastori basi.......

Niliwahi kuandika kuhusu hausigeli na kasheshe zake. Leo nilitaka kugusia Hausiboi na kasheshe zake ingawa nime....

Watu tunajijengea kasumba kuwa nani ni zaidi na nani sio. Wengine wengi tunapata maana yakua sisi ni nani au kujitambua, kupitia nini tunafanya.Lakini kumbuka hiyo ni kasumba ya kujijengea tu.
Utasikia mtu akisema, kuwa yule hafai kwa sababu hana kazi, kazi yake ya kipuuzi, mshahara wake mdogo, nk. Lakini huyu bomba kwa sababu........

Kumbuka , mwisho wa siku, mahusiano ya watu na kuvutiana kwa watu kiini chake ni jinsia ya akuvutiaye. Kama waliowengi waaminivyo ilivyo kawaida ,kiini cha kuvutiwa kwao ni lazima kitakuwa mtu wa jinsia tofauti afikiaye mizani ya matamanio na kutimiza yale ya msibuyo kimatamanio katika kipindi hicho.Kama Msenge au msagaji, utavutiwa tu na mwenye jinsia yako, hapa hakuna cha mshahara , kazi yako wala nini kama kiini cha jambo hilo.

Swali:
Unafikiri ,wote uwatamanio cha kwanza kikujiacho akilini ni wanafanya kazi gani?

Nakubali pia kuwa unaweza kuvutiwa na afanyacho mtu au baikeli yake gari na........
Lakini....

Kutokana na baadhi ya utafiti uliofanywa na wanasayansi kibao, unaambiwa kuwa mwanadada ni rahisi kuonja nje pale awapo katika zile siku mayai yako tayari kupokea mbegu za kiume. Inasemekana kipindi hiki vile vile huvutiwa zaidi na wanaume wenye sura za kiume zaidi.Ukiwa na sura fulani ambayo unaweza kufananishwa zaidi na mama au dada yako, halafu hausiboi wako kafanana na babayake, basi kasheshe kama mambo fulani mwanadada uliyenaye huumtimizii.Wanaume wengi wanasababu zao kwa nini wanaweza kuwa na nguvu nje ya ndoa, mahusiano kuliko ndani ya ndoa.
Tafuta kazi za Professor Robert Winston kuhusu Human Instinct kwa stori zaidi kuhusu huu utafiti.
(Kumbuka niongeavyo hapa, sio ndio ukweli asilimia zote kwa wote)

Lakini jiulize, wakati hutimizi, una hausiboi?
Ndio , mamaa ni bomba la mdini, kwa hiyo atajizuia. Si wote tunajua yeye ni Swala tano, sala zote na........ anahudhuria.
DUH!

Lakini........

Duh!
Nisikutishe!

Najaribu kuweka hili wazi kwa mara nyingine.......

Kazi ni kazi.
Jamii tu ndio inatabia mbaya ya kupendelea baadhi ya mambo na kutafsiri nyadhifa za watu kama vile ni muhimu kuliko mengine katika maisha ya binadamu.
Kama unapata kitu kidogo kwa shughuli zako zozote, mimi nakupa tano.
Binadamu kabla ya yote atakutambua wewe kama binadamu , na kwa ubinadamu wako.

Usishangae ni kwanini mtoto wa jirani anafanana na hausiboi lakini!
Kumbuka kabla ya yote , utu wake ndio kigezo cha mama mwenye nyumba kuvutiwa naye, ingawa ni siri.
Lakini, si ni baba mwenye nyumba mvivu au ana kazi nyingi zimfanyazo awe amechoka awapo nyumbani kuwakilisha yahitajiwayo katika mahusiano?

Lakini timiza utakiwacho kwenye mahusiano yako basi!
Wiki Mwisho njema!
Nakuacha na Slum Village wakiwa na Dwele

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 7:23 pm  

Mzee Katibu Simon,upande mwingine nakubaliana na wewe,upande mwingine si kubaliani na wewe kuhusu swala zima la HOUSEBOYNA HOUSEGIRL.

Naomba kukuuliza,leo hii ubahatike kuwa na houseboy au housegirl utakubali kweli akufulie,avipige viatu vyako rangi,akupikie,anyooshe nguo zako na bila kusahau akufungie Tai yako?

Kwamtazamo wa Rasta,jina house girl au boy linaniumiza kiakili kwasababu naona kama ni utumwa.

Katibu,tajiri anamaana ipi anaposema,hata house boy wangu anasuti na viatu vipya?Inaamna ya kwamba hata mtumwa wangu anasuti mpya na viatu vipya.

Naomba tutumie jina,kaka au dada kama ni mkubwa wako kiumri au mdogo wangu kama nimdogo wako kiumri.

Anonymous 9:19 pm  

Simon..Samawati hiyo duh!Na nyekundu juu yake!andika makala kuhusu rangi za blogu:)Pole nimekuzoea sana.

Simon Kitururu 10:09 pm  

@Rasta: Mimi nimezoea sana kujitegemea. Na kuhusu kazi za nyumbani kama unavitendea kazi, huhitaji sana mtu mwingine.Katika baadhi ya mambo ambayo naweza kukuambia kuhusu mimi, Mara nyingi napenda chakula nikipikacho mwenyewe, siamini mtu mwingine anaweza kunipigia pasi ngu zangu vizuri. Kufua nina miaka sijawahi kufua , kwahiyo labda hapo.
Ila Hili swala la jina la mahausiboi au kaka, baba, mjinga, Rais , kwangu ni maneno tu , hayaniumizi kichwa. SIchukii hata ukinitukana mbwa wee au ....Kwa hiyo hili swala naona sensibilities zetu zinatofautiana.
@Serina: Hii blogu niongeapo iko kwenye matengenezo. Itakuwa poa si muda mrefu. Kuhusu rangi, nahisi labda nina U colour blind fulani , kwani sehemu zote niichekipo blogu yangu naiona poa tu. Ni wewe na Aliko mlinistua kuwa haionekani poa.Inakarabatiwa lakini.
Na mimi nimekuzoea:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP