Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NI NINI SAHIHI KUONGELEA?

>> Sunday, July 29, 2007

Kabla sijasema......
Hebu cheki jamaa wakikufuru kutokana namtazamo fulani.......


Tuna mila na desturi zitufundishazo, ziwekeazo mipaka ya nini ni sahihi na nini si sahihi.
Kuna tamaduni zituhakikishiazo kuwa tufanyayo ni sahihi na wafanyayo si sahihi.

Samahani stori kidogo......

Nakumbuka nilipokuwa katika kozi moja ihusianayo na jinsi ya kukabiliana na watu wa tamaduni tofauti, ambapo ikafikia wakati karibu kila mtu akawa hajiamini kuwa asemacho au akiongea kwa kutumia saini , hamkorofishi mwenzie.Ilifikia pia kuogopa kusema au kuongelea topiki fulani kutokana na ngazi tofauti za uwashawasha wa toki hizi katika tamaduni nyingine. Katika baadhi yatopiki watu wakastukia kuwa nimetahiriwa. Hiki ni kitu ambacho Warusi na Wazungu wengine wengi waliokuwepo kwenye kozi walikishangaa sana.Ukiwatoa wayahudi kwa Wazungu wengi kuwa na govi ni kitu ambacho ni kawaida sana .
(Nakumbuka lakini tuna makabila mengi tu Afrika na duniani, yaonao kitendo hiki ni cha ajabu .Kumbuka katika tamaduni nyingi ni mwiko kufanya govi na vipengele vingine vihusianavyo na sehemu za siri kuwa topiki yakuongelea.)

Duh!
Samahani kwa wale wanaoweza kukwazwa na lugha niitumiayo kijiweni....!


Basi bwana...

  • Tukagundua kuwa kwa Wajapani saini ya kuonyesha pesa , kwa Waperu ni tusi.
  • Uitaji mtu wa kawaida kwa Wafini, Kwa mtanzania ukiitwa hivyo na kidole kimoja, maana yake akuitaye anakudharau.
  • Kitendo cha kupungia gari ilikulisimamisha kwa Mtanzania, sehemu kibao ndio kupungia Kwaheri!
  • Kukataa kwa kichwa Watanzania tulikokuzoea kwa wengine ndio kukubali.
  • Nakadhalika kadhaaa......
Dini nazo zinatufundisha ni nini sahihi.
Tatizo ni kwamba nini sahihi katika dini moja , sio lazima ni sahihi katika dini nyingine.
Ukiwa Muislamu, nguruwe haramu. Ukiwa Mhindu, ng'ombe haliki....nk
Halafu madoido ya binadamu, unaweza kukutana na Vegan mpagani lakini kwake nyama yoyote haramu.
Swali:
Kila mwenye dini , dini yake inamwambia hiki akifanyacho ndio sahihi,
Sasa nani ni sahihi kikweli kweli?
Ushawahi kukutana na asiyeamini dini mpaka kutoamini kwake dini inakuwa dini?

Maswala ya tamaduni nyingi yamekataza sana mambo mengi , lakini kuongelea ngono ni mojawapo. Naamini swala hili limekuwa jambo likwepwalo kuanzia ndani ya famili.

Stori kidogo.....

Nakumbuka baba yangu siku moja alivyokuwa anajaribu kutaka kuongelea swala hili na mimi. Alikuwa anataka kunionya kuhusu kujiadhari na ngono na tatizo la UKIMWI hasa baada ya Zubeda fulani kuwa anakuja sana kunitafuta nyumbani. Jasho lilimtoka , na mimi ingawa nilikuwa najua anataka kuongelea nini, nikawa simsaidii kumpa jinsi ya kutoa somo kirahisi. Lakini alifanikiwa baada ya kutoa jasho kunipa statistics za Ukimwi na jinsi gani nijiadhari nk. Nafikiri kungekuwa na maswala yakupelekwa jandoni angeweza hata kunipeleka huko ingekuwa somo hili liko katika silabasi ya jandoni.

Ombi:
Kama kunamtu alifanikiwa kupelekwa jandoni au unyagoni, ningeomba atushushie silabasi ya masomo ya jandoni au unyagoni.Kwa sababu nina wasiwasi na ufupi wa muda shule hizo zinavyotumia kutoa krashi kozi ya maisha.

Hebu Mcheki Alexyss K. Tylor akiwa na mama yake ayaongeayo....(tafadhani lugha atumiayo yaweza kuwakwaza baadhi na sina uhakika kama uko chini ya miaka yaukubwa ni vizuri kwako kumsikiliza)



Katika tamaduni kibao jambo afanyalo Alexyss haliwezekani.
  • Chakusikitisha ni kwamba maswala haya ya ngono kutokana nakutoongelewa sana na kiuwazi , imefikia kuwa ndio yanayoongoza kwa kutafutwa mtandaoni.
  • Cha ajabu asilimia kubwa ya mambo ya ngono yapatikanayo mtandaoni, hayamfundishi kitu cha muhimu mtafutaji wake, zaidi yakumsaidia katika swala la tule tuhamu.
  • Chakusikitisha maswala haya , kutokana nakutofundishwa vyema, au kutokana na kuwepo habari nyingi potofu juu yake, yamekuwa ni chanzo kikubwa cha uenezaji UKIMWI na ukosaji furaha ya mahusiano ndani yamahusiano ya watu(Iwe ndoa au nanihiii...).
Eti mpaka sasa kunao wanaoamini kuwa ukifanya ngono na bikira unapona UKIMWI, kitu kifanyacho watu hasa kusini mwa Afrika kubaka watoto.

Swali:
Hivi kweli ni sahihi kukaa kimya kutokana na ukweli mambo mengine hatakutamka ni jambo litutialo kinyaa?

Hebu nikukumbushe ule wimbo wa Boku wa .... Wimbo wa doli....



Sasaaa....
  • Hivi ni nini sahihi kuongelea?
  • Je, hayo maongezi ni muhimu kama hakuna yafundishayo jamii kupiga hatua yakimaendeleo, kiakili, kifikira....nk ?
Naamini maongezi yasiyojenga nikupoteza muda, hasa ukifikiria maisha ya binadamu yalivyo mafupi hata kabla hujafikiria muda binadamu autumiao kulala nk..
  • Lakini hivi ni maongezi gani ndio sahihi na yanayojenga na kuchangia kumuendeleza binadamu?
  • Nani yuko sahihi kuliko mwingine ambaye ana haki yakuamulia wengine ni nini sahihi kuongelewa?
Duh!
Ngojea nikuache basi!
Jumapili njema!
Nakuacha na Maroon 5

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP