Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Sanaa ya Danganya Toto!

>> Wednesday, July 25, 2007

Ukifikiri sana, karibu kila kitu ni uongo.
Binadamu anaakili mpaka imefikia kiasi cha kuudanganya ubongo wake kuwa yamzungukayo ni ukweli.

Swali:
Hivi Uongo ni nini?
Ushawahi kudanganya?

Kuhusu mimi, nahisi unajibu:-)
Kabla sijasema msikilize huyu...


Mtoto anapozaliwa, kabla hatuna uhakika kuwa anaelewa, mimi naamini kuwa anastaili zake za kudanganya.Nilikuwa na mcheki mtoto mmoja wa rafiki yangu juzi. Huyu mtoto anaweza kudanganya kuwa anausingizi ili apelekwe chumbani. Akishaachwa chumbani hafanyi kelele wala nini, lakini baada ya muda utasikia TV imewashwa, ukifika huko unakuta nguo zote kabatini ziko chini, na karaha kibao. Yeye anapenda kuchezea nguo. Hivyo kagundua akiachwa pekee ndio anazichezea bila kubughuziwa.Hivyo akagundua mchezo wa kujifanya amechoka iliapelekwe chumbani ambako anapata uhuru wake.Umri wake mwaka mmoja lakini anajua jinsi ya kuwadanganya wazazi wake ili wampe nafasi. Kuna mifano mingi tu!Nasikia hata mimi nilivyokuwa mdogo , nilistukia kuwa nikiumwa, napewa chakula kizuri zaidi nikipendacho kirahisi.Nafikiri unajua maswala ya kuletewa chakula kizuri ukiwa mgonjwa halafu siku nyingine inabidi ule kile wenzio wanacho kula. Nafikiri unajua kautundu gani kanatakiwa hapo ili upate msosi mwingine bomba!

Sasaaaa....

Si umecheki hiyo video hapo juu? Tunashauriwa eti tuwadanganye watoto, wapenzi wetu, hata ....

  • Lakini kuna yale maswali fulani!Nafikiri unayajua yale........!AU?
Utayajibuje kiukweli ?
Lakini kudanganya si ni dhambi eeh?

Ee Bwana ee!
Kumbe kumdanganya mpenzi wako pia mali sana, kama unajua kuwa ukweli utamzingua tu.

SASAAAA!
  • Wewe mwanadada ukiniuliza kuwa tokea nikonawe simtamani mwanadada mwingine unatarajia nijibu nini?
  • Hivi wewe mwanadada ukinisimulia story zako za mwanamume uliyekuwa naye kabla yangu na jinsi alivyokuwa bomba na alivyokuwa anaku.... unafikiria nini?Hatakama nimekuuliza..! -Si unidanganye tu kuwa alikuwa uchwara au hujawahi kuwa na mwingine kabla yangu, yaishe?
  • Hivi wewe mwanakaka utakapo kujua sana kwanini leo Mamaa anaenda sokoni tu lakini katilia mavazi na pafyumu ile baabu kubwa , unategemea jibu gani?
  • Na kadhalika kadhaa.......
Samahani sijagusia kile kimfano ulichotaka nigusie hapo juu!

Duh!
Basi bwanaaaaa..........ngojea niendelee kukupa dondoo tudanganyanazo.
  • Umependeza sana!
  • Hiyo nguo imekutoa sana!
  • Wewe mzuri!
  • Una akili wewe!
  • Nilivyokuona tu nikagundua kuwa malaika hawapo mbinguni tu!
  • Sijawahi kumpenda mwingine ila wewe tu!

AU?

Duh!
Tuendelee na viuongo...

  • Mjinga sana wewe!
  • Kichwa kama kachori!
  • Afrika Maskini sana!
  • Marehemu alikuwa mtu Mzuri sana!
  • Yule rafiki yangu sana tu!
  • Na kadhalika kadhaaaa.....
Duh!
Ngojea wakati unafikiria kuhusu hilo nimuache Eek a Mouse asimulie kuhusu swala ......


Katika sanaa ya kudanganya , hakuna mabingwa zaidi ya wapatikanao kwenye maeneo ya dini.

Nisikuficheee......!

Napenda kuona watu wanapenda dini. Kwa sababu naamini wanadamu wengi kwao, ni vigumu kuwa na misimamo ambayo inaendesha maisha yao na inajaza maisha yao maana. Majibu ya kwanini wako duniani, maskini,matajiri, wagonjwa hivi, mpaka pale kwenye, hivi kwanini imenitokea mimi na sio yule, ni maswali magumu ambayo akili ya binadamu ina ufinyu wake na mara nyingi kutokana na uvivu wa kibinadamu wa kufikiri, inashindwa kupatiwa majibu.Dini imesaidia sana kumfanya binadamu kuendeleza uvivu wakutafuta majibu, lakini imemsaidia mara nyingi kuweza kufurahia hali yake aliyonayo, kutokana na majibu dini iyatoayo yatulizayo ubongo na ...

Dondoo:
Dini ni bomba la kituliza ubongo. Lakini kumbuka kuna mengi binadamu ajihangaishayo nayo kajitungia mwenyewe.


Bila dini, naamini dunia ingekuwa iko navituko na majanga mengi zaidi yasababishwayo na binadamu na kaubongo kake, kuliko ilivyo sasa.
Duh!
Binadamu kiboko!Eti baadhi ya wenye akili wameamua kupigana vita iuayo watu Iraki, ilikuleta amani.(Kumbuka lakini kuwa dini hizi zihubirizo amani, mara nyingi zi chanzo, kati wala...kiini cha amani
)

Naamini binadamu anahitaji kupata maana ya maisha na kujua kwanini utamu na uchungu ni vitu vimzungukavyo kila siku.Asipojua vilevile, ni muhimu awe katika hali ya kutafuta kujua, kitu kimfanyacho apitishe siku akiwa anamategemeo fulani ya kesho na utulivu wa akili au akili iliyotawaliwa na fikira zimfanyazo kutoonyesha unyama wake.

Naamini binadamu aligundua dini kutokana na hii hali yakutaka kuelewa maisha na woga wakutojua maisha na baada ya maisha ayaelewayo.
Kuna watu nikiongelea dini wanafikiri naongelea Ukristo na Uislamu ambao ndio miongoni mwa dini chekibobu duniani.Dini chekibobu ,nikimaanisha zijionyeshazo na zisakazo wafuasi mpaka chini ya uvungu.Dini zipendazo kuwahakikishia wafuasi wake kuwa ndizo za kweli ingawa pia hutumia uongo pia kujiuza.

Ngojea nikutulize kidogo na kideo hiki....


Swali:
Hivi unajisikia vibaya kwenda kanisani bila pesa eeh?

Samahani , nilisahau kuwa inawezekana kuwa wewe si mkristo.

Basi tuendelee....

Hivi unataka niendelee kweli kukuelezea kuhusu sanaa ya uongo mpaka kwenye siasa?
Hivi ukisikia Wamarekani wanavyodai wanapigania demokrasia , si utafikiri ni kakitu fulani kazuri kweli eeh?

Swali:
Unajua maana ya demokrasia?
Simmesikia ikihubiriwa?
Umeshawahi kuona nchi yenye demokrasia?

Sawa , nimekuelewa.
Duh!
Hivi ulinielezea ka kitu eeh?:-)


Nafikiri unafikiri Rais Kikwete aliyepigiwa kura na Watanzania karibu wote waliopiga kura, ni matunda ya demokrasia.Lakini si unajua Watanzania waliowengi hawajui hata ni nini kinaendelea Tanzania zaidi ya danganya toto wanasiasa watoazo?
Unachotakiwa kudanganya ukitaka kupigiwa kura ni.......,
  • Ahidi lolote ufikirialo wanahitaji mtaani kwao.
  • Kama wananjaa, wape wali na kuku kwenye mikutano yako.
  • Waahidi hata helkopta, bila ya kusema utazinunuaje.
  • Waahidi utawasaidia wale chipsi mayai , pilau kila siku ukichaguliwa.
  • Waahidi utawawekea bomba la maziwa ingawa unajua hawana maji.
  • Kama wagumu kidogo, waahidi utatunza amani.Halafu usisite kuwadanganya kuwa mpinza wako ataleta vita kama ya Rwanda.

Duh!
Au ni George Bush nini unafikiria alichaguliwa kidemokrasia?
Lakini kafuzu katika Sanaa ya danganya toto.

Ngojea nikuache utulie basi!
Siku njema!
Nakuacha na Mark Morrison
, anayekupa kibao nilichokuwa napenda kusikiliza baada ya kudanganywa na mwanadada fulani.

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

eddiie 10:08 am  

am not really good at Swa but i liked your dreadlocks...they certainly look first class......

eddiie 10:09 am  

i have deadlocs hoping so much to have to put dreadlocs......

Egidio Ndabagoye 10:58 am  

Uongo ni dhambi?.lakini vitabu vinatuambia hivyo "Usiseme uongo".Lakini nasikia kuna uongo wa kuweza kukusaidia.Sasa sijui huo ni dghambi au la.
Umenikumbusha wakati nachukua mafundisho ya dini,kuna store f'lani kuwa wakati wa vita vile vya "dunia" padri mmoja ambae sasa hivi anaesabika kama "mtakatifu" alikuwa anawindwa na jamaa wale ili auawe.lakini jamaa wale hawakuwa wakimjua kwa sura.

Ila walikuwa wanajua ni sehemu ganui anaishi walimzukia wakiwa njiani wakakutana na yeye mwenyewe kwa kuwa walikuwa hawamjui walimuuliza kama anamfahamu padri huyo akasema anamfahamu na kamuacha kanisani mida hiyo kwa hiyo akawaambia wawahi ili wamkute.
Jamaa walitoka baruti na kumuacha yeye na ndio ikawa pona pona yake.

Sasa na huo ni dhambi?? Nilimuuliza katekista siku izo akaniambia sio dhambi!.Kazi ipo hapo

Simon Kitururu 1:50 pm  

@Eddiie:Thanx!Get them dreads soon man!It aint difficult.U are welcome here man!
@Egdio:Kazi kwelikweli

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP