Ashki Ya Michango!Lakini Ushachangia Nanihii?
>> Wednesday, February 28, 2007
Swali:
Hivi Tanzania tunaweza kurudia michango tuihitajio au waihitajio kikweli?
Sisi binadamu tunamapungufu yetu! Ni vigumu kila siku kuweza kufanya yote tutakayokufanya kwa nguvu zetu wenyewe. Tunahitaji misaada mara kwa mara. Tuna matatizo mengi.Na kwa bahati mbaya matatizo haya hayawezi kuisha.
Lakini.....
Naamini mara nyingine sisi wenyewe hutengeneza baadhi ya matatizo. Kwa bahati mbaya au nzuri, kitu kingine kitufanyacho sisi kuwa binadamu ni jinsi tunavyoweza kujijengea mazoea ya vitabia vyetu. Moja ya tabia ambayo ni rahisi kuzoeleka ni ile ya michango.
SISEMI KUWA MICHANGO NI KITU KIBAYA!
NAKUBALI KUNAMICHANGO NI MUHIMU KWETU KUCHANGIA.
Lakini.......
Je, hii michango tuipayo kipaumbele na yenyewe inatupakipaumbele ?
Je, hii michango inasaidia kuendeleza au inabomoa?
Je, hii michango inasaidia tuchangiapo?
Katika baadhi ya vitu binadamu afanyavyo , vimejijenga ndani ya binadamu kwa muda mrefu. Kama unamkumbuka Maslow na kile kielelezo chake cha ngazi za matakwa ya jamii na binadamu.......
......utaona kuwa, tunanasa katika ngazi nyingi tu.
Ukiniuliza kwanini tunachanga sana hata pale ambapo hatuna ujanja tunajihisi ni lazima tutoe michango, kwa kutumia Jicho la mitazamo ya Maslow,
.....nitasema kwasababu:
- Kupata amani(ngazi ya pili, kwenye jeduali):tunafarijika kuwa iposiku tutasaidiwa pia na watu tuwachangiao.Iwe ni familia, wafanyakazi wenzetu, nk
- Kukubalika/kupendwa(ngazi ya tatu):kwa kawaida usipokuwa mchangiaji hukawii kuitwa bahiri na sio mtu safi
- Staha(ngazi ya nne hapo juu kwenye jeduali): kuheshimika, inatusaidia kuwa na uhakika, na tunajisikia hali ya kufanikiwa.
- Tunajisikia tunafanikisha maswala, tunajisikia kunakitu ambacho tunafanya .
Tukiachana na Maslow na mitazamo yake , mimi naweza kusema kuwa hii hali ya michango haiko katika binadamu tu bali hata katika wanyama karibu wote wa kinyaninyani.
Kama wewe ni mfuatiliaji wa tabia za wanyama kama Chimpanzee, na hata bonobo utakuta wanakamtindokao kakushughulikia maswala ya michango. Chimps katika mengi wafanyayo , hukumbuka nani alimfadhili mwingine.Chimps aliyekuwa anamkuna mwenzie na kumtoa vidudu , huwa ni rahisi kwake kupewa chakula na aliyemkuna iwapo atakosa chakula. Bonobo wao imefikia mpaka mwanamke ndio ananguvu katika kundi kutokana na kutengeneza uhusiano kwa kupeana michango. Ndio nakubali hawatoi pesa, lakini unafikiri michango ya pesa inanunulia nini?
Ngoja niwakumbushe tofauti za hawa wanyama wawili niwazungumziao.
Huyu ndio Chimp
Huyu ndio Bonobo.
Yeye huwa mwembamba kuliko Chimp wa juu. Halafu anamidomo ya denda.
Kwanini nimewakukumbusha hawa wanyama?
Duh!
Tuache tu!
Lakini usijisikie mpweke! Si wewe wala mimi pekee katika kamchezo haka ka-maisha tunajikuta tumebanwa kona fulani, hata manyani pia.
SASA lakini.....
Kumbuka michango mingine ukweli wake ni kwamba haukusaidii wala kumsaidia yeyote yule!
Halafu kwa kuzidi kuiendekeza unajiumiza tu!
Naamini msemakweli na afanyaye kutoka moyoni ,hustukiwa tu na jamii!Sasa kama kale kamchango ka-filigisi za sikukuu ya...... hukawezi , achananako.
Ukikaendekeza kanakuumiza tu !
Halafu kumbuka haka kamchezo ka-maisha kana mambo yake mengine.Ukijiumiza kwa kufanya mambo usiyoyaweza ipo siku utaonekana mbaya na umeumia zaidi. Halafu ukionekana mbaya au umeumia zaidi , watu wanakamchezo kakukukwepa. Wataobaki ni wale tu rafiki zako wa kweli ambao,wangekuelewa hata usingechangia.
Tuchange tu tuwezapo, lakini tuangalie tusiibe tu jamani kwa kujaribu kutunza sura!
Hivi michango na minyoo vinauhusiano?
Halafu kwanini ghafla tu, michango imekuwa ndio lifestyle Tanzania?
Mimi sielewi kama nisivyoelewa hapa chini ,Franco akiwa na TP Ok anasemanini.....
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kitururu!
Umenikumbusha kozi moja pale UDSM ya Psychology. Tulimchambua vizuri sana Abraham Maslow. Kwa ujumla inasikitisha kumuona mtu anakimbilia kutimiza mahitaji ya level ya nne il-hali ya level ya kwanza yamemshinda. Maslow's hierachy of needs inashauri kwamba tunatakiwa tufanye mambo ngazi kwa ngazi.
@Mtanzania: si ndio hapo basi!
Post a Comment