Davos!-Hivi hii sio shoo ya pembeni tu?
>> Thursday, February 01, 2007
Kila ninapozidi kusikia maswala yanayosemekana kufanyika Davos katika WEF(World Economic Forum) , nashindwa kujizuia kufananisha mkutano huu na sideshows zilizokuwa maarufu katika circus. Nashindwa kuacha kufikiria kuwa hawa viongozi wetu wa nchi maskini hualikwa hapo kuwa kama vituko kwa matajiri kuangalia.
Huu mkutano uwekao kiwanja kwa wafanyabiashara maarufu na wanasiasa kutoka nchi tajiri kujadili maswala kwa kigezo cha kupata muelekeo tofauti katika dunia ,mimi naona ni kigezo tu kitumikacho kuwaunganisha wenyenavyo . Kwa maskini aalikwaye ni kama kituko cha kukodolewa macho tu.
Unakumbuka lakini sideshows za zamani? Zile ambazo zilibobea kwa kuwaweka binadamu kwenye show kwa ajili ya wengine kuwa kodolea macho ilikuwa na furaha? Zile zilizomfanya Sara Baartma , the Hottentot Venus maarufu.
Bila kumsahau Prince Radian na wengine wengi.
Kama kwenye sideshow muda ukapita na watu wakastukia kuwa hakuna mpango kuwa kituko tu katika onyesho ili mradi kunapesa inaingia. Sasa ningependa tuone viongozi hawa watuwakilishao wanaendesha shoo na sio kuwa vituko vya kukodolewa macho tu.
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Nimependa jina hilo: shoo za pembeni.
Hizo ni shoo za pembeni za kupamba shoo kuu. Wasindikizaji toka miaka hiyo na tutaendelea kuwa wasindikizaji, watumbuizaji wa pembeni kwa miaka mingi ijayo tusipofumbua macho.
Post a Comment