Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ayaan Hirsi Ali

>> Wednesday, February 07, 2007


Maswala ya kidini ni magumu sana. Lakini kunabaadhi ya watu wanavyoyakabili huniacha mimi mdomo wazi. Huyu mwanadada Ayaan Hirsi Ali aliyezaliwa Somalia na kukulia Kenya kabla ya kujilipua Uholanzi ni miongoni mwa watu hawa ambao huniacha mdomo wazi.
Niliangalia akihojiwa siku moja nikaamini kuwa kama Salman Rushdie aliwekewa fatwa sitashangaa kuona huyu akiwekewa hivi karibuni.Baadhi ya ayasemayo ni haya....




Pamoja na kutengeneza sinema itwayo submission iliyofanya director wake auawe na kumfanya yeye awe kwenye listi ya kuuawa, haachi wala kupunguza kusimamia ayaaminiyo.
Sehemu ya sinema hii ni hii hapa...


Nachojiukiza ni kwamba hivi mpaka wa kusimamia uaminicho ni upi?


Je, msimamo kama wa Martin Luther King Jr aliyekuwa anaamini mtu asiyeweza kufia kitu hafai kuishi ni sahihi?
Unaikumbuka misemo ya Martin Luther King Jr?

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 7:12 pm  

Nyongeza: ukiacha Rushdie, kuna Taslima Nasreen wa Bangladesh ambaye naye Fatwa ilipitishwa dhidi ya kichwa chake kwa kutumia kalamu kujieleza. Aliwahi kusema kuwa kurani inahitaji kuhaririwa upya kwa ufasaha zaidi!
Msome hapa: http://tinyurl.com/2sehxb

Na tovuti yake: http://taslimanasrin.com/

Simon Kitururu 10:34 am  

Duh!Sikuwahi kumsoma huyu. Asante!

Egidio Ndabagoye 12:07 pm  

Da! Simon huyu mwanamama Ayaan nimemuona hivi majuzi katika kipindi cha Hard Talk BBC ni moto wakuotea mbali hoja zake ni kali nilikuwa na Ustaadh mmoja alitamani kumfuta kwenye TV na kumnyongelea mbali.

Simon Kitururu 1:07 pm  

@Egdio. hakutaka kukunyonga weye?

Egidio Ndabagoye 8:29 pm  

We acha Simon hawa washakaji nimeshawazoea sana.
Kipindi nakaribia kufanya mtihani wa kidato cha sita nilikuwa nakaa gheto pale Upanga na washikaji wa Tambaza.Kuna kisa nikikumbuka huwa nacheka sana peke yangu.

Simon Kitururu 8:38 pm  

Nipe hícho kisa !Egdio, umenitamanisha kuja Uhindini.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP