Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wauaji!

>> Wednesday, February 07, 2007

Nyerere aliua.
Mkapa akaua.
Bush Anaua.
Blair anaua.
Papa John Paul aliua.
Ayatollah Khomeini alikuwa muuaji.
Mandela aliua.

Hivi hawa viongozi wakitoa amri watu waende vitani wanasahau kuwa amri hiyo niyakuruhusu kuua? Wakitoa amri watu wauawe inamaanisha sio wao walioua kwa sababu si wao walioshika bunduki au kitanzi kuua?


Hivi muuaji ni nani?
Hivi muuaji ni yule tu ambaye amejistukia kaua au jamii imetafsiri kitendo chake ni uuaji?

Kwa nini wapiga wezi Tanzania hawajisikii kuwa ni wauaji hata kama wamempiga mwizi mpaka akafa?

Hivi kwanini binadamu wanachagua nani wakumuita muuaji?

Je mimi na wewe si wauaji?

Usitishike najiuliza tu!

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MTANZANIA. 5:17 am  

Duh!! kaka Simon hili ni jambo zito. Kimsingi ukweli unabaki palepale ya kwamba kwa namna moja au nyingine na ww mtoa amri ni muuaji pia na kama ni kufunguliwa mashtaka basi yafaa kabisa ujumuishwe.Kama hivyo ndivyo basi wauaji ni wengi!

Mija Shija Sayi 8:11 am  

Kuua ni kuua tu, ila sijui kwanini mambo huenda tofauti kwa wauaji wengine.

Na mimi naungana na wewe katika kujiuliza.

mwandani 2:50 pm  

Nasikia Mandela hakuwahi kukamua risasi, na bastola yake aliyoichimbia kwenye shimo kabla ya kwenda lupango ndio imefukuliwa juzi juzi tu - anyway. Ukiua katika kujihami kuna ubaya? yaani ukimuona adui kashika shoka analishusha upande wako, ukahepa ikesha ukamfanyia tukio...

Saa nyingine huwa nafikiria juu ya visasi vya kikabila - watu wa kabila hili walivamia kambi ya adui na kubaka dada, sasa nikiona mwanya kabla adui hajabaka mama na mke wangu - nikimpiga shaba adui na kuua nitalaumiwa pia?

luihamu 5:52 pm  

Mzee Simon,ngoja niulize swali,kwa mfano tuchukuwe amri moja kati ya zile kumi tulizopewa na nabii Musa
USIUWE
Je usiuwe inamaana tu ya kutenda lile tendo la kutoa maisha ya binadamu duniani au?Kwa mtazamo wangu yeyote yule ambaye hajishuhulishi na kuwajali yatima na wajane katenda kosa la kuuwa.

Kwa upande mwingine amri kumi zimefupishwa lakini zina maana nzito sana kwa mfano hakuna amri inayosema usivute sigara au usinywe bombe lakini utakuta mambo yote haya katika moja ya amri hizo.

Anonymous 1:35 am  

Hii ni philosophy kali sana ndugu. Umetupa kitu cha kufikilia.

Simon Kitururu 11:11 am  

@Wote-Duh!

Anonymous 11:28 am  

je utoaji wa mimba unauchukuliaje? mwanafalsafa weye mfano madenti wa shule za msingi na secondari(minors) wanapoabort je nao ni makiller?,yule dk anaendesha hio surgery nae ni killer? boyfriend asietumia vikinga mimba nae ni serial killer?
aliko

Simon Kitururu 11:31 am  

@Aliko- Duh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP