Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kloning Sokoine!

>> Tuesday, February 20, 2007

Sijasikia habari za kloning ziigusavyo Tanzania.
Hivi kama kuna-Watanzania ambao tungeweza kutengeneza kopi zao. Yupi ungependa kloni wake arudishwe?

Kuna wadau kibao waliniambia hiki kitu kingekuwa kimekubalika na jamii ,basi wangewarudisha kloni wa ndugu zao wengi tu. Katika wanasiasa wa Tanzania, kuna watu kibao walimtaja Sokoine.

Leo imebidi nijiulize kuwa hivi ni kitu gani cha zaidi kinachomfanya Sokoine aonekane alikuwa tofauti?

Katika majibu machache niliyopata nikashangaa kuwa kwanini yalionekana ni tofauti(special).

Sifa za Sokoine kuu zilizomfanya awe maarufu ni:

  • Mfanyakazi kwa bidii.
  • Hapendi rushwa na anaipiga vita rushwa.
  • Kiongozi asiye na makuu.
  • Anajivunia mila yake.

Labda unaweza ukaongezea sifa zake. Lakini hizo nilizozitaja ndio zilijulikanazo sana. Sasa huhisi hizi ni sifa ambazo kila kiongozi wa Tanzania anatakiwa awenazo?

Sasa jiulize kwanini kila mtu akamstukia Sokoine kuwa bomba?

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mjengwa 6:38 pm  

Sokoine aliwaheshimu wakubwa wake lakini hakuwaogopa. Alikuwa na ujasiri wa kumwambia mkubwa wake HAPANA.

MTANZANIA. 11:50 pm  

Kitururu! Hii mada umeitoa wakati muafaka kwani muda si muda atatimiza miaka kadhaa tangu atangulie kunako haki. Bila shaka huyu angefaa kuwa Presidaa wa awamu ya pili. "R.I.P MORINGE"

luihamu 6:44 am  

Simon,kwa mtanzamo wangu ningependa Moringe afufuke leo.Kati ya viongonzi wa dunia naweza kumlinganisha na Martin Luther King au Patrice Lumumba au Nelson Mandela.

Simon unakumbuka wimbo wa BOB jah live children?anasema hivi

the truth is always an offence.

Simon Kitururu 12:34 pm  

@Luihamu: naujua! Unakusuta eeh?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP