Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mwezi wa Historia ya mtu mweusi

>> Monday, February 12, 2007

Marekani na Canada mwezi huu wa pili huenzi historia ya watu weusi. Kutoka mwaka 1926 wakati ilikuwa ni wiki moja, mwaka 1976 kuanza kuenziwa kwa mwezi mzima , na mpaka leo, twaweza kusema mambo mengi yamebadilika.

Swali:
Hivi mambo yamebadilika kweli?

Bado ni kawaida kuitana majina ya ajabu ajabu , kuuana na mambo mengine kibao.
halafu ishaanza kuwa kawaida kusikia vita kati ya Walatino na weusi Marekani. Sasa ikiwa mwanzo tatizo lililokuwa likizungumziwa kuwa ni la weusi na weupe tu, inakuaje sasa hivi weusi na walatino wanapigana vikumbo mtaani?Je , ule ugomvi wa wazungu na weusi hautoshi?

Halafu kale kamchezo kakuitana majina kati ya watu weusi na weupe masharti yake huwa yananizingua sana.
Hebu mcheki huyu mwalimu akijitetea..


Ni sawa kuwa watu weusi sio wenye matatizo peke yao. Ukisikia ya Wapalestina wanavyo bwengana sasa hivi kwa sababu wengine ni Hamas na wengine fatah unaweza ukaingia dhambi ya kupata uahueni kwa kuona matatizo si ya watu weusi tu. Lakini kunakitu nadhani utakuwa unakisahau au hutakiwi kukisahau hivi sasa. Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu weusi wanakosa kujiamini. Watu weusi bado tunaaminishwa kuwa hatuna thamani kutokana na rangi. Karibu kila kona ya dunia tunajaribu kuaminishwa kuwa hatuwezi maswala.

Ukweli ni kwamba ni mimi na wewe ndio tutakiwao kubadili hii mitazamo ya watu. Katika mwezi kama huu ambao huenziwa Marekani na Canada, sioni ni vibaya kujikumbusha na kukumbuka kuwa mapambano yanaendelea.Watu wote weusi duniani ni muhimu kukumbuka kutosahau hili.Na kivyetu vyetu kujitahidi kuwa mchango chanya.Bado tunahitaji watu wamifano wengi. Akina Mandela hawatoshi.

Swali:
Lakini ni kwanini tuenzi historia ya watu weusi kwa mwezi tu? Je, sio siku zote tuishizo ni za kuenzi historia yetu?




Je, unasemaje kuhusu mwanamume mweusi huyu anavyoenzi mwezi huu wa kukumbuka historia ya mtu mweusi?Hebu msikilize......

Ingawa tukiliangalia swala hili katika kona tofauti , unaweza kuona kuwa labda kunatofauti ya unyonge kati ya mwanamke mweusi na mwanaume mweusi. Lakini naamini tukizidi kuimarisha timu zote mbili - wanawake weusi na wanaume weusi- ikawa timu moja isiompendelea mwanamme, timu yetu itakuwa babu kubwa.Kwani bado naamini kuwa kunatabia ya kutowashirikisha wanawake katika maswala kwa kuamini kuwa wao wanapendeza nyumbani tu. Naamini tunapoteza baadhi ya vichwa muhimu kwa kufanya hivyo.

Dondoo:
Unakumbuka hii filamu aliyoitengeneza Kiri Davis, ionyeshavyo mpaka sasa jinsi gani watoto weusi hujisikia wamepitwa uzuri na weupe?

Au icheki hapa basi tena....


Ukiangalia hiyo filamu hapo juu utaweza kusema kuwa hilitatizo ni la watoto wazaliwao na kukulia nje ya Afrika. Lakini nauhakika lawezakuwepo popote kama watoto watakua wakiwa hawana mifano ya kujivunia ifananayo nao.
AU?

Haya ndugu zanguni!
Baadaye!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Unknown 12:52 am  

labda wangeuita mwezi wa kukumbuka biashara ya utumwa na jinsi ilivyokidhalilisha kizazi cha watu weusi na sio mwezi wa kuwaenzi watu weusi,wanawaenzi kwani watu weusi hawapo tena?harakati za kuwafundisha watu weusi kujiamini ni lazima ziambatane na kukuza jira miongoni mwa watu weusi,iwapo kina queen latifah,will smith na watu wengine weusi waliofanikiwa wataendelea kuwa na mameneja wazungu fikra zitaendelea kuwa mtu mweusi lazima asimamiwe na mtu mweupe.wakati mwingine huwa nashangaa nikiangalia basketball naona timu nzima ni ya watu weusi lakini mwalimu wao ni mzungu!sipendi tuishi kwa kubaguana ila ni vyema mwingiliano uwe na uwiano sawa.

Simon Kitururu 12:02 pm  

Zemarcopolo leo nimekuona hapa.Asante kwa kunitembelea.Huwa napenda jinsi unavyochambua maswala.Karibu tena na tena

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP