Hivi kama Afrika sisi ni masikini haturuhusiwi kucheka?
>> Saturday, February 03, 2007
Mapambano yanaendelea!
Kabla sija sema......
Kassav
Nashangaa kwamba nimekutana na watu wanashangaa, itakuwaje Afrika ina matatizo bwelele lakini Waafrika bado wanatabasamu.Mwingine akaniambia kuwa Afrika iko nyuma kwasababu Waafrika tunatabasamu wakati tuna shida. Mimi naamini hii ni kurahisisha mambo. Furaha na kilio si siri ya kwenda mbele kimaendeleo.Ni siri iishiyo ndani ya binadamu. Naamini kuwa Waafrika, hata kwenye kucheka hatusahau kilio. Au?
Swali:
Hivi maendeleo ni nini?
Halafu.....
Mory Kante
WIKIENDI NJEMA!
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Nashukuru kukuta umepitia pale nyumbani. Karibu tena. Kuhusu hii mada nina mambo mawili;
Mosi, Mungu ameweka kitu sahau ili kumfanya bin-adam asiwe mwenye huzuni muda wote.Hii inasaidia kuweza fanya mambo mengine. Waafrika bila kujali yanayotusibu katika nyanja mbalimbali tumejaliwa furaha."Wacha tucheke"
Pili, nilihudhuria tamasha la muziki wa kiafrika na hakika kundi la Mandika family toka Guinea Conakry lilitia fora baada ya kuigiza kibao cha YEKE2 hali iliyoamsha shamra2 ukumbi mzima. Ni kibao kizuri kusema kweli.
Post a Comment